Tuesday 20 January 2009

Liverpool wakabwa, washindwa kutwaa uongozi LIGI KUU!!!

Watani wa jadi, watoto wa mjini Liverpool, Timu za Liverpool na Everton, jana usiku uwanjani Anfield zilitoka suluhu kwa kufungana bao 1-1 na hivyo kuifanya Liverpool iwe pointi sawa na Mabingwa Manchester United lakini Man U anaongoza kwa kuwa na tofauti ya magoli bora kuliko Liverpool ambao, hata hivyo, wamecheza mechi moja zaidi ya Manchester United.
Baada ya kwenda mapumziko wakiwa hawajafungana, Liverpool walipata bao lao kupitia Nahodha Steve Gerrard aliefumua shuti la mbali dakika ya 68.
Zikiwa zimesalia dakika 3 mechi kwisha frikiki ya Mikel Arteta ilimaliziwa kifundi na Tim Cahill kwa kichwa na kuisawazishia Everton.
Timu hizi zitakutana tena Jumapili kwenye uwanja huohuo wa Anfield safari hii kwenye mechi ya Raundi ya 4 ya Kombe la FA.
Liverpool: Reina, Carragher, Hyypia, Skrtel, Aurelio, Kuyt, Gerrard, Alonso, Riera (Babel 89), Keane (Benayoun 67), Torres (Leiva Lucas 85).
Akiba hawakucheza: Cavalieri, Dossena, Arbeloa, Mascherano.
Goli: Gerrard 68.
Everton: Howard, Hibbert, Lescott, Jagielka, Baines, Osman, Arteta, Neville, Pienaar, Cahill, Anichebe.
Akiba hawakucheza: Nash, Van der Meyde, Castillo, Rodwell, Jutkiewicz, Gosling, Kissock.
Kadi: Pienaar, Arteta.
Goli: Cahill 87.
Watazamaji: 44,382
Refa: Howard Webb (S Yorkshire).

Kaka agoma kuhamia Man City!!

Sasa dunia haitoshuhudia uhamisho wa bei mbaya katika historia baada ya kuthibitishwa Kaka amekataa kuhama AC Milan na kwenda Manchester City.
Iliripotiwa Kaka atahamia Man City kwa dau la Pauni Milioni 100 ambalo lingemfanya awe Mchezaji alieuzwa kwa bei mbaya kupita yeyote kwenye historia ya soka la kulipwa.
Mpaka sasa rekodi ya Mchezaji alieuzwa bei mbaya inashikiliwa na mauzo ya Zinedine Zidane alieuzwa Julai, 2001 kutoka Juventus kwenda Real Madrid kwa Pauni Milioni 46.
Klabu ya AC Milan ilitoa taarifa rasmi kuwa: KAKA ANABAKI AC MILAN na Silvio Berlusconi, Rais wa Klabu hiyo, alikiambia Kituo cha TV kimoja cha Italia: 'Huo ni mwisho wa hadithi hii! Kaka anabaki na nimefurahi sana!
Katika mechi ya Jumamosi ambayo AC Milan waliifunga Fiorentina bao 1-0 kwenye pambano la SERIE A, Mashabiki walibeba mabango na kuimba kumtaka Kaka asiondoke.

BAADA YA KUMKOSA KAKA, MAN CITY YAMNUNUA CRAIG BELLAMY!!!

Klabu ya Manchester City imemsaini Mshambuliaji Craig Bellamy, umri miaka 29, kutoka West Ham kwa ada ya Pauni Milioni 14.
Bellamy alijiunga West Ham kwa Pauni Milioni 7.5 msimu uliokwisha na mpaka sasa ameshawahi kuchezea Klabu za Norwich, Coventry, Newcastle, Celtic, Blackburn na Liverpool.

No comments:

Powered By Blogger