Sunday 18 January 2009

Baba yake Dodi, Al-Fayed, aitaka FA kudhibiti viwango vya madau ya uhamisho na mishahara ya Wachezaji!!!

Baada ya kuibuka stori za uhamisho wa Kaka kutoka AC Milan kwenda Manchester City timu inayomilikiwa na Koo ya Kifalme tajiri sana ya huko Abu Dhabi, Falme ya Nchi za Kiaarabu, Mohamed Al-Fayed, ambae ni Mmisri mmiliki wa Klabu ya Fulham na pia ni Baba Mzazi wa Dodi aliekufa kwenye ajali ya gari pamoja na Princess Diana huko Paris mwaka 1997, amewataka viongozi wa LIGI KUU England na FA kudhibiti madau ya uhamisho Wachezaji pamoja na mishahara yao.
Inaaminika Kaka anaweza kuhama AC Milan kwa dau la Pauni Milioni 100 na atapewa mshahara wa Pauni Laki 5 kwa wiki zote zikiwa ni rekodi za dunia.
Mohamed Al-Fayed alitamka: 'Ni wenda wazimu! Hilo dau ni Mchezaji mmoja tu, je wengine kwenye timu hiyo? Ni habari mbaya kwa soka, lakini Viongozi LIGI KUU na FA wana uwezo kudhibiti haya! Mimi silipi zaidi ya Pauni Milioni 15 kwa Mchezaji! Kuna vyuo vizuri kwenye klabu nyingi vinavyo kuza vipaji vya watoto na vijana na hiyo ndio njia bora kuliko kulipa Mamilioni!'
Mchezaji alienunuliwa kwa bei mbaya na timu ya Al-Fayed Fulham ni Steve Marlet mwaka 2001 kwa Pauni Milioni 11.


WACHEZAJI WALIOVUNJA REKODI YA KUNUNULIWA BEI MBAYA:

-Pauni Milioni 46 Zinedine Zidane (Juventus - Real Madrid)

-Pauni Milioni 37 Luis Figo (Barcelona - Real Madrid)

-Pauni Milioni 34 Hernan Jorge Crespo (Parma - Lazio)

-Pauni Milioni 33 Gianluigi Buffon (Parma - Juventus)

-Pauni Milioni 32.5 Robinho (Real Madrid - Man City)

-Pauni Milioni31 Christian Vieri (Lazio - Inter Milan)

-Pauni Milioni 30.75 Dimitar Berbatov (Tottenham - Manchester United)

West Ham 3 Fulham 1 huku Bellamy akiwa nje ya uwanja!!

Mshambuliaji wa West Ham Craig Bellamy hakuwepo kwenye kikosi ambacho leo kimeshinda 3-1 dhidi ya Fulham kwenye LIGI KUU mechi iliyoanza saa 10 na nusu bongo taimu.
Inasadikiwa Bellamy jana alisusa mazoezi baada ya West Ham kukataa ombi lake la kuhamia Tottenham waliotoa ofa ya Pauni Milioni 12 kumnunua.
David de Michele aliipatia West Ham bao la kwanza lakini Paul Konchesky alisawazisha kwa shuti kali sana.
Mark Noble aliifungia West Ham bao la pili kwa penalti baada ya Mshambuliaji Carlton Cole
kuchezewa rafu wakati akienda kufunga.
Carlton Cole akawapachikia West Ham bao la 3.


Joe Cole nje ya uwanja msimu wote!!

Mchezaji wa kutumainiwa wa Chelsea, Joe Cole, atalazimika kukaa nje ya uwanja msimu wote uliobaki baada ya kuumia goti kwenye mechi ya Kombe la FA iliyochezwa Jumatano kati ya Chelsea na Southend.
Joe Cole alifanyiwa upasuaji wa goti hilo jana na sasa anaungana na mwenzake wa Chelsea Michael Essien ambae pia aliumia goti na kupasuliwa kwa kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu
.

Joe Kinnear awalaumu Sam Allardyce na Kevin Keagan kwa matatizo ya Newcastle!!

Joe Kinnear, Meneja wa Newcastle, mara baada ya kubandikwa 3-0 kwenye mechi ya LIGI KUU jana na Blakburn Rovers amewarukia Mameneja waliokuwa nyuma yake hapo Newcastle na kuwabebesha zigo la lawama za kuwa na timu mbovu.
Kabla ya Kinnear, Meneja alikuwa Keagan ambae nae alirithi kutoka kwa Sam Allardyce.
Kinnear alilalama: 'Hawa si Wachezaji wangu! Nimewarithi! Tatizo kubwa timu haina Wachezaji wengi na wa maana! Sijui kwa nini Mameneja wa nyuma yangu hawakuona hilo!


UHAMISHO

Dirisha la Uhamisho wa Wachezaji lilifunguliwa tarehe 1 Januari na litafungwa mwisho wa mwezi na wafuatao ni baadhi tu ya Wachezaji waliohama au kuhamia kwenye Vilabu vya LIGI KUU:
-Manucho [Man U kwenda Hull kwa mkopo]
-Javan Vidal [Stoke kwenda Tranmere kwa mkopo]
-Kevin Kilbane [Wigan kwenda Hull kwa ada ambayo haikutajwa]
-Liam Miller [Sunderland – QPR mkopo]
-James Beattie [Sheffield United – Stoke kwa ada haikutajwa]
-Lee Bowyer [West Ham – Birmingham nkopo]
-Jermaine Defoe [Portsmouth – Tottenham ada Pauni Milioni 15]
-Sebastian Puygrenier [Zenit St Petersburg - Bolton mkopo]
-Hameur Bouazza [Fulham – Birmingham mkopo]
-Ritchie De Laet [Stoke – Man U ada haikutajwa]
-Mathew Etherington [West Ham – Stoke Pauni Milioni 2]
-Scott Sinclair [Chelsea – Birmingham mkopo]
-Wayne Bridge [Chelsea – Man City ada haikutajwa]
-Adem Ljajic [Partizan Belgrade – Man U ada haikutajwa]
-Adem Ljajic [Man U – Partizan Belgrade mkopo hadi mwisho wa msimu huu]
-Zoran Tosic [Partizan Belgrade – Man U ada haikutajwa]

MAREFA WA LIGI KUU WANAOONGOZA KWA KADI

1] Mike Riley Mechi 14 Kadi: Nyekundu 3 Njano 61 Wastani: kadi 4.57 kwa mechi
2] Mike Dean Mechi 16 Nyekundu 6 Njano 62 Wastani kadi 4.25
3] Howard Webb Mechi 18 Nyekundu 5 Njano 70 Wastani 4.17
4] Andre Mariner Mechi 14 Nyekundu 4 Njano 54 Wastani 4.14
5] Michael Jones Mechi 5 Nyekundu 2 Njano 17 Wastani 3.8

No comments:

Powered By Blogger