Saturday 16 January 2010

LIGI KUU: Everton 2 Man City 0
Walisema leo ndio mtihani wa kweli kwa Meneja wa Manchester City, Roberto Mancini, ambae tangu achukue hatamu ameshinda mechi kadhaa za Ligi Kuu lakini Wadau walidai alicheza na Timu ‘dhaifu’ kama Stoke na Wolves na leo kukutana na Everton ndio kigingi chake.
Na kweli, ndani ya Goodison Park, Everton walifanya kweli nyumbani kwao na kumpa Mancini na Man City yake somo kali la kandanda pale walipoifunga bao 2-0 na pengine mabao hayo ni salama yao kwani Everton walitawala kabisa na kukosa lundo la magoli.
Wafungaji wa Everton walikuwa Steven Pienaar dakika ya 36 kwa frikiki murua na Saha dakika ya 45 kwa penalti baada ya Micah Richards kumvuta jezi Saha.
Katika mechi hii Robinho alianza benchi lakini akaangizwa dakika ya 8 tu ya mchezo baada ya Santa Cruz kuumia na cha kushangaza ni kule kutolewa kwa Robinho kipindi cha pili na kuingizwa Shaun Wright-Philipps kitendo ambacho inaelekea kilimkera Robinho kwani alipotolewa tu Robinho hakwenda kukaa benchi bali alitoka na kwenda moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilisha jezi.
Pengine huu ndio mwanzo wa mwisho kwa Robinho hapo Man City.
Vikosi vilivyoanza:
Everton: Howard, Neville, Heitinga, Distin, Baines, Donovan, Fellaini, Pienaar, Bilyaletdinov, Cahill, Saha.
Akiba: Nash, Vaughan, Forshaw, Coleman, Duffy, Baxter, Mustafi.
Man City: Given, Zabaleta, Richards, Kompany, Garrido, Petrov, De Jong, Barry, Bellamy, Tevez, Santa Cruz.
Akiba: Taylor, Onuoha, Sylvinho, Wright-Phillips, Robinho, Mwaruwari, Boyata.
Refa: Andre Marriner
KOMBE LA AFRIKA: Nigeria 1 Benin 0
Bao la penalti ya Yakubu Ayegbeni dakika ya 42 limewapa ushindi Nigeria dhidi ya Benin wa bao 1-0 na hivyo kufufua matumaini yao hasa baada ya kushindiliwa 3-1 na Misri katika mechi ya kwanza.
Nigeria watacheza mechi yao ya mwisho na Msumbiji wakati Benin watamaliza na Misri.
Mechi nyingine ya Kundi hili itakayoanza punde ni Misri v Msumbiji.
LIGI KUU: Ni mvua kubwa Darajani- Chelsea 7 S'land 2; Man U 3 Burnley 0; Spurs wabanwa mbavu!!!
Huko Stamford Bridge, Chelsea waliangusha kipigo kikubwa walipoibamiza Sunderland mabao 7-2.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Anelka, bao 2, Lampard, bao 2, na Ashley Cole, Malouda na Ballack bao moja kila mmoja.
Mabao ya Sunderland yalifungwa na Zenden na Darren Bent.
Mpaka mapumziko, Chelsea walikuwa mbele kwa bao 4.
Huko Old Trafford, baada ya kuwa suluhu 0-0 hadi mapumziko, Manchester United walishusha kipigo cha bao 3 kipindi cha pili.
Mabao ya Man U yalifungwa na Rooney, Berbatov na Diouf.
Mchezaji Mame Biram Diouf aliingizwa kipindi cha pili na hii ni mechi yake ya pili kuingizwa lakini ni ya kwanza kwa Uwanja wa Old Trafford na aliwainua Mashabiki wa Man U pale alipofunga bao tamu dakika ya 90.
Huko White Hart Lane, Tottenham ililazimishwa sare ya 0-0 na Hull City.
Nao Wolves walilambwa 2-0 na Wigan wakiwa nyumbani kwao kwa mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na McCarthy na N'Zogbia.
Wachezaji Stearman wa Wolves na Thomas wa Wigan walitolewa nje kwa nyakati tofauti baada ya kupewa Kadi Nyekundu.
MATOKEO KAMILI:
Stoke 1 v Liverpool 1
Chelsea 7 v Sunderland 2
Man United 3 v Burnley 0
Portsmouth v Birmingham [IMEAHIRISHWA]
Tottenham 0 v Hull City 0
Wolves 0 v Wigan 2
[INAANZA saa 2 na nusu usiku]
Everton v Man City
MECHI ZA KESHO Jumapili, 17 Januari 2010
[saa 10 na nusu jioni]
Aston Villa v West Ham
[saa 12 jioni]
Blackburn v Fulham
[saa 1 usiku]
Bolton v Arsenal
Ligi Kuu: Stoke 1 Liverpool 1
Goli la kipindi cha pili dakika ya 67 alilofunga Beki Kyrgiakos baada ya vurumai golini kufuatia frikiki, liliwapa matumaini Liverpool na pengine kumpa ahueni Meneja wao Rafa Benitez aliekuwa ameandamwa kila kona baada ya Timu hiyo kutupwa nje ya Kombe la FA ilipofungwa 2-1 hapo Jumatano na Reading lakini Stoke walikuwa na lengo lingine kwani walisawazisha dakika ya 89 Mfungaji akiwa Beki Huth baada kona iliyoleta kizaazaa.
Mechi hii iliyochezwa Uwanja wa Britannia, nyumbani kwa Stoke, haikuwa ya kuvutia na ilionekana wazi ni mechi ya Timu mbili zilizo kwenye matatizo na suluhu ni kitu bora kwa Timu zote.
Vikosi vilivyoanza:
Stoke: Sorensen, Huth, Abdoulaye Faye, Shawcross, Higginbotham, Delap, Whitehead, Diao, Etherington, Sidibe, Sanli.
Akiba: Simonsen, Whelan, Lawrence, Fuller, Pugh, Collins, Wilkinson.
Liverpool: Reina, Carragher, Kyrgiakos, Skrtel, Insua, Degen, Lucas, Mascherano, Aurelio, Kuyt, Ngog.
Akiba: Cavalieri, Aquilani, Riera, Maxi, Spearing, Darby, Pacheco.
Refa: Lee Mason
Kanisa kulishitaki Vuvuzela Afrika Kusini
Habari zitokazo huko Kwa-Shangase, Kwa Zulu-Natal, zimesema kuna Madhehebu ya kale huko Afrika Kusini yaitwayo Kanisa la Kibaptisti ya Nazareth, jina la kiasili ni ‘Shembe’, yamo njiani kufungua kesi Mahakamani kupinga matumizi ya ‘Vuvuzela’ kwenye Viwanja vya Soka na hasa kwenye Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Afrika Kusini kuanzia Juni 11 hadi Julai 11.
Msemaji wa Shembe, Enoch Mthembu, anadai Vuvuzela ni mali ya Kanisa lao na limeibiwa na Washabiki wa Soka na wameahidi kufungua kesi Mahakamani kupinga matumizi yake mipirani.
Shembe hulitumia Vuvuzela katika Mtembezi yao makubwa ya kila mwaka wakizifuata nyayo za Mwanzilishi wa Kanisa lao Isaiah Shembe alipotembea kwenda Mlima Mtakatifu wa Nhlangakazi huko Kaskazini ya Mji wa Durban, Kwa Zulu-Natal mwaka 1910.
Matembezi hayo matakatifu ambayo kila mwaka huwa na Wafuasi zaidi ya 300,000 huandamana na milio ya Vuvuzela.
Shembe wanadai kuna Shabiki mmoja wa Kaizer Chiefs, ambayo ndiyo Klabu kubwa Afrika Kusini, alilitembelea Kanisa lao kwenye miaka ya mwanzoni 1990 na ‘kuiba’ hilo Vuvuzela.
Vuvuzela limevuta hisia nyingi katika ulimwengu wa Soka huku baadhi ya Nchi zikitaka lipigwe marufuku kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa kuwa na kelele nyingi na kusumbua Wachezaji, Watazamaji na Makampuni yanayopeperusha matangazo ya moja kwa moja ya TV.
Hata hivyo FIFA imesema Vuvuzela litaendelea kwa sababu ni utamaduni wa Soka ya Afrika Kusini.
LIGI KUU England: Portsmouth v Birmingham yaenda na maji!
Mechi ya Ligi Kuu kati ya Portsmouth na Birmingham iliyokuwa ichezwe leo saa 12 saa za bongo imefutwa baada ya Uwanja wa Fratton Park, nyumbani kwa Portsmouth, kujaa maji.
Mechi hii itapangiwa tarehe nyingine hapo baadae.
KOMBE LA AFRIKA: Leo Nigeria v Benin na Misri v Msumbiji
Mjini Benguela, Angola, Uwanja wa Taifa wa Ombaka, leo kutakuwepo na mechi mbili za Kundi C zikiwa ni mechi za pili kwa kila Timu.
Leo lazima Nigeria washinde baada ya kufungwa mechi ya kwanza na Misri mabao 3-1.
Benin walitoka suluhu 2-2 na Msumbiji katika mechi ya kwanza.
Ushindi kwa Misri utawaingiza Raundi ya Pili baada ya kushinda mechi ya kwanza 3-1 dhidi ya Nigeria.
Mechi za mwisho kwa Kundi hili ni Benin v Misri na Nigeria v Msumbiji.
Zaki njiani kurudi England!!
Amr Zaki huenda akarudi tena kucheza Ligi Kuu England safari hii na Klabu ya Hull City endapo mipango ya kwenda huko kwa mkopo itakamilika.
Amr Zaki ni Mchezaji wa Zamalek ya Misri na Msimu uliokwisha alikuwa na Wigan kwa mkopo na aliifungia Klabu hiyo mabao 11 lakini akakorofishana na Meneja wa Wigan wa wakati huo Steve Bruce na hivyo akakosa Mkataba wa kudumu hapo Wigan.
Zaki, miaka 26, hayupo kwenye Kikosi cha Misri kilichopo Angola kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kuwa ni majeruhi.
Owen kupata namba Man U!!!
Sir Alex Ferguson amemhakikishia Michael Owen kuwa mechi zijazo atakuwa anachezeshwa mara nyingi kupita siku za nyuma.
Ferguson amesema kutokucheza mara kwa mara kwa Owen ni tatizo la mbinu na mikakati kwenye fomesheni ya Man U na hasa kwa vile staili ya uchezaji ya Rooney na Owen inawafanya wao kuona ugumu wa kuwapanga kucheza pamoja.
Ferguson ametamka: “Owen inabidi apate mechi na hilo tunalitafutia ufumbuzi! Rooney hawezi kucheza kila mechi, inabidi apumzike na tutabadili mfumo wetu na
Owen atacheza tu!”
Pia, kuibuka kwa taarifa kuwa Dimitar Berbatov anauguza goti ambalo atafanyiwa operesheni mwishoni mwa Msimu na hivyo kumfanya apunguziwe mechi za kucheza, bila shaka kutaongeza nafasi kwa Owen kucheza.
Babel nje Kikosi cha Liverpool cha leo na Stoke!!
Inaelekea kibarua cha Ryan Babel huko Liverpool kinafikia ukingoni baada ya Winga huyo kutoka Uholanzi kutupwa nje ya Kikosi cha Liverpool kitakachocheza LigI Kuu leo na Stoke City licha ya Liverpool kutokuwa na Mafowadi wa kutosha kufuatia kuumia kwa Torres, Gerrard, Benayoun na kuuzwa kwa Voronin kwa Dynamo Moscow.
Hivi karibuni, Babel aliwahi kutangaza ni bora ahame Liverpool kwa vile hana namba ya kudumu na bora aende Timu ambayo atakuwa na namba ili aboreshe nafasi yake ya kuitwa Kikosi cha Uholanzi kitakachokwenda Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia mwezi Juni.
LIGI KUU: TATHMINI YA MECHI ZA WIKIENDI HII
Wikiendi hii inategemewa Timu zote 20 za Ligi Kuu zitashuka dimbani na kucheza tofauti na wikiendi iliyopita wakati mechi zote ziliahirishwa kwa sababu ya barafu na baridi kali isipokuwa mechi mbili tu.
RATIBA:
[saa za bongo]
Jumamosi,
[saa 9 dak 45 mchana]
Stoke v Liverpool
[saa 12 jioni]
Chelsea v Sunderland
Man United v Burnley
Portsmouth v Birmingham
Tottenham v Hull City
Wolves v Wigan
[saa 2 na nusu usiku]
Everton v Man City
Jumapili,
[saa 10 na nusu jioni]
Aston Villa v West Ham
[saa 12 jioni]
Blackburn v Fulham
[saa 1 usiku]
Bolton v Arsenal
Uhondo huu utaanza kwa mechi ya Jumamosi ya mapema kupita zote, ile ya saa 9 dakika 45 mchana, saa za bongo, Stoke City itakapoikaribisha Liverpool.
Baada ya kutolewa nje ya Kombe la FA hapo juzi walipofungwa 2-1 na Reading, Meneja wa Liverpool Rafa Benitez amewaahidi Washabiki wao kuwa katika mechi hii watabadilika na kuwaletea faraja.
Lakini mbali ya Stoke City kuwa wagumu wakiwa nyumbani kwao, Liverpool watakuwa na upungufu mkubwa kwani watawakosa Nyota wao Fernando Torres, Steven Gerard na Yossi Benayoun ambao ni majeruhi.
Vinara Chelsea watakuwa nyumbani Stamford Bridge kucheza na Sunderland na hii ni mechi ya kwanza kwa Chelsea bila ya Mastaa Didier Drogba, Michael Essien na Salomon Kalou ambao wako Angola na Nchi zao kwa Kombe la Afrika.
Burnley, baada ya kuondokewa na Meneja wao Owen Coyle aliehamia Bolton, watakuwa chini ya Meneja mpya Brian Laws huko Old Trafford kucheza na Mabingwa Watetezi Manchester United ambao waliikimbia barafu ya Uingereza wiki yote hii na kujichimbia Doha, Qatar kwa kambi ya mazoezi. Katika mzunguko wa kwanza, Burnley iliipiga Man U bao 1-0.
Portsmouth, Timu iliyo mkiani Ligi Kuu na yenye uhaba mkubwa wa fedha hadi Wachezaji kukosa Mishahara kwa wakati, watakuwa nyumbani kuwakaribisha Birmingham, Timu ambayo kwa sasa ina maendeleo mazuri mno Ligi Kuu. Mechi iliyopita Birmingham ilitoka sare 1-1 na Man U.
Hull City walio nafasi ya pili toka mkiani wanasafiri hadi White Hart Lane kukumbana na Tottenham.
Uwanjani Molineux, Wolves watakuwa wenyeji wa Wigan na Timu zote hizi ziko nafasi ya chini kwenye msimamo wa Ligi hivyo hii ni vita kuu kati yao.
Mechi ya mwisho Jumamosi itakayoanza saa 2 na nusu usiku saa za bongo ni ile ya Goodison Park kati ya wenye uwanja Everton na Manchester City na mechi hii Wadau wanasema ndio mtihani mkubwa kwa Meneja wa Man City Roberto Mancini tangu aanze kazi.
Jumapili, Aston Villa wanawakaibisha West Ham na Villa watapigana washinde mechi hii hasa baada ya kupoteza mechi mbili za mwisho za Ligi. Kwa West ham, Msimu huu ni mgumu sana kwao na Meneja wao Gianfranco Zola ataomba Timu yake ijitutumue.
Mechi nyingine za Jumapili ni Blackburn Rovers v Fulham na Bolton v Arsenal.
Kwa Bolton, hii ni mechi ya kwanza chini ya Meneja mpya Owen Coyle aliehamia hapo kutoka Burnley.

Friday 15 January 2010

Ivory Coast yatinga Raundi ya Pili!!
• Ivory Coast 3 Ghana 1
Ivory Coast ndio Timu ya kwanza kuingia Raundi ya Pili ya Kombe la Afrika baada ya kuifunga Ghana iliyochezesha Vijana wadogo wengi mabao 3-1.
Mpaka mapumziko, Ivory Coast ilikuwa mbele ka bao 1-0 Mfungaji akiwa Gervinho baada ya krosi tamu ya Salomon Kalou.
Kipindi cha pili kilianza kwa Ghana kumuingiza Michael Essien na kwa Ivory Coast haikuchukua muda pale Emmanuel Eboue alipowashwa Kadi Nyekundu na Refa Damon baada ya kucheza rafu mbaya kwa Opoku Agyemang.
Lakini, Ivory Coast hawakutetereka na Siaka Tiene akawapatia bao la pili kwa frikiki nzuri sana na Didier Drogba akafunga bao la 3 kwa kichwa kufuatia krosi ya Kader Keita.
Ghana walipata bao lao moja kwa njia ya penalti waliyopewa baada ya Soulemane Bamba kumwangusha Asamoah Gyan na Gyan akafunga mwenyewe hiyo penalti.
Sasa Ghana inabidi waifunge Burkina Faso katika mechi yao ya mwisho ili kusonga Raundi ya Pili na wakitoka suluhu Burkina Faso watafuzu na Ghana nje.
Mechi hiyo itachezwa Jumanne Mjini Luanda, Angola badala ya Cabinda ambako Kundi hili lilicheza mechi zake.
Vikosi vilivyoanza:
Ivory Coast: 1-Boubacar Barry; 17-Siaka Tiene, 4-Kolo Toure, 21-Emmanuel Eboue, 22-Soulemane Bamba; 5-Didier Zokora, 6-Yaya Toure, 9-Cheik Tiote, 8-Salomon Kalou; 10-Gervinho, 11-Didier Drogba.
Ghana: 22-Richard Kingson; 18-Eric Addo, 7-Samuel Inkoom, 15-Isaac Vorsah, 11-Moussa Narry; 19-Emmanuel Agyemang-Badu, 9-Opoku Agyemang, 13-Dede Ayew, 17-Rahim Ayew, 14-Mathew Amoah, 10-Kwadwo Asamoah.
Refa: Jerome Damon (South Africa)
MECHI ZA Januari 16:

[saa za bongo]
[KUNDI C]
Nigeria v Benin [saa 1 usiku]
Egypt v Mozambique [saa 3 na nusu usiku]
KISANGA CHA LIVERPOOL: Ligi Kuu valuvalu, FA Cup…Nje , Carling Cup…Nje, Ubingwa UEFA…Nje, na je Benitez…..NJE??
• Mwenyewe Benitez aomba radhi Mashabiki!!!
Huku kukiwa na kitendawili kikubwa kuhusu ajira yake hapo Liverpool, Meneja Rafa Benitez amewaomba radhi Mashabiki wa Liverpool kwa Timu yake kutofanya vizuri kwenye mechi na mashindano mbalimbali Msimu huu.
Siku ya Jumatano, Liverpool wakiwa nyumbani Uwanjani Anfield, walibwagwa nje ya Kombe la FA baada ya kufungwa na Reading, Timu inayojikongoja Daraja la chini ya Ligi Kuu, kwa bao 2-1.
Benitez, akisoma kutoka kwenye kikaratasi, alisema: “Hatuchezi vizuri na kila mtu kwenye Kikosi chetu anawaonea imani Mashabiki wetu! Kwenye Soka vitu hubadilika haraka na tuamini Jumamosi tutakapocheza na Stoke tutashinda!”
Msimu uliokwisha Liverpool walimaliza nafasi ya pili nyuma ya Mabingwa Manchester United na wakati kila mtu alitegemea watakuwa tishio Msimu huu, mambo yameenda kombo na wamekuwa wakifungwa mechi nyingi na kutupwa nje ya Makombe makubwa.
Kwenye Ligi wako nafasi ya 7 wakiwa pointi 12 nyuma ya vinara Chelsea.
Mpaka sasa wameshatolewa kwenye Vikombe vya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, FA na Carling.
Wamebaki kwenye kinyang’anyiro cha EUROPA Ligi tu na walitupwa huko baada ya kumaliza nafasi ya 3 kwenye Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Wadau wengi wa Liverpool, wakiongozwa na Wachezaji wa zamani wa Klabu hiyo, wametaka aondolewe lakini hilo kwa uongozi wa Liverpool limekuwa zito ikizingatiwa Klabu hiyo iko kwenye hali mbaya kifedha na inakabiliwa na madeni makubwa.
Kumtimua Benitez ni kuiingiza Klabu hiyo kwenye deni kwani Benitez amesaini Mkataba mpya na Klabu hiyo mwezi Machi 2009 utakaomweka hapo 2014 na ukimtimua tu inabidi umlipe pesa nyingi.
Swali linakuja: Timu ikiendelea kufungwa na hata mwishoye kuikosa nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE Msimu ujao, nini hatima ya Benitez?
Fergie: 'Rooney atawika Kombe la Dunia'
Sir Alex Ferguson anaamini Wayne Rooney ana uwezo wa kuwa nyota kwenye Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Afrika Kusini mwezi Juni.
Wayne Rooney, miaka 24, alianza kuchezea michuano mikubwa ya Kimataifa pale alipoichezea England kwenye Euro 2004 na kufunga bao 4 lakini akashindwa kuendelea kucheza Mashindano hayo baada ya kuvunjika mfupa kwenye kidole cha mguu wake kwenye Robo fainali walipocheza na Ureno.
Mwaka 2006, huku akitoka kwenye majeruhi, aliichezea England kwenye Kombe la Dunia lakini akatwangwa Kadi Nyekundu kwenye Robo Fainali walipocheza na Ureno.
Lakini Ferguson anasema: “Rooney ana uwezo wa kuwa shujaa wa Kombe la Dunia. Miaka yote kila Kombe la Dunia anaibuka Staa na Rooney ana uwezo huo. Nimeshuhudia jinsi anavyozidi kuboreka!”
Msimu huu, baada ya kuondoka kwa Ronaldo, Rooney ndie amekuwa Mfungaji mkuu wa Manchester United akiwa ni mmoja wa Wafungaji bora wa Ligi Kuu akiwa na bao 14.
Lakini Ferguson anakiri pengo la Ronaldo.
Ferguson anasema: “Ni kweli tunamkosa! Alikuwa ni mtu bora! Mchezaji bora! Alikuwa na sisi miaka 6! Tunamkumbuka!”
Ni wikiendi ya Ligi Kuu tena!!
Baada ya kutibuliwa na barafu wikiendi iliyokwisha na kubakisha mechi mbili tu za Ligi kuchezwa, wikiendi hii inayokuja, mpaka sasa, Ratiba imesimama palepale kama ilivyopangwa awali na hivyo kuwakikishia Wadau uhondo wa mechi kedekede.
Msimamo wa Ligi Kuu ni kama ifuatavywo:
[Timu zimecheza mechi 20 isipokuwa inapotajwa]
1 Chelsea pointi 45
2 Man Utd pointi 44 [mechi 21]
3 Arsenal pointi 42
4 Man City pointi 38
5 Tottenham pointi 37
6 Aston Villa pointi 35
7 Liverpool pointi 33
8 Birmingham pointi 33 [mechi 21]
9 Fulham pointi 27
10 Stoke pointi 24
11 Sunderland pointi 23
12 Everton pointi 23
13 Blackburn pointi 21 [mechi 21]
14 Burnley pointi 20
15 Wolves pointi 20
16 Wigan pointi 19 [mechi 19]
17 West Ham pointi 18
18 Bolton pointi 18 [mechi 18]
19 Hull pointi 20
20 Portsmouth pointi 14
WAFUNGAJI BORA:
1 Jermaine Defoe 14
2 Didier Drogba 14
3 Wayne Rooney 14
4 Darren Bent 13
5 Fernando Torres 12
6 Carlos Tevez 12
7 Louis Saha 10
8 Cesc Fabregas 9
9 Gabriel Agbonlahor 8
10 Carlton Cole 7
RATIBA MECHI ZA LIGI KUU England
[saa za bongo]
Jumamosi, 16 Januari 2010
[saa 9 dak 45 mchana]
Stoke v Liverpool
[saa 12 jioni]
Chelsea v Sunderland
Man United v Burnley
Portsmouth v Birmingham
Tottenham v Hull City
Wolves v Wigan
[saa 2 na nusu usiku]
Everton v Man City
Jumapili, 17 Januari 2010
[saa 10 na nusu jioni]
Aston Villa v West Ham
[saa 12 jioni]
Blackburn v Fulham
[saa 1 usiku]
Bolton v Arsenal
Jumatano, 20 Januari 2010
[saa 4 dak 45 usiku]
Arsenal v Bolton
[saa 5 usiku]
Liverpool v Tottenham
Leo ni Ivory Coast v Ghana!!!!
Huko Uwanja wa Taifa wa Chiazi, Cabinda, Angola, Ivory Coast wakiongozwa na Nahodha wao Supastaa Didier Drogba, leo wanatupa karata yao ya mwisho watakapojimwaga uwanjani kupambana na Ghana, Timu ambayo wengi wameibatiza jina la “Brazil ya Afrika”.
Ivory Coast walitoka suluhu na Burkina Faso 0-0 katika mechi yao ya kwanza na kujitoa kwa Togo kufuatia maafa ya kuuliwa wenzao kumelifanya Kundi hili liwe na Timu tatu tu na hivyo, wakati Ivory Coast wanamaliza mechi zao leo, Ghana ndio kwanza wanaanza.
Ni lazima Ivory Coast ashinde leo ili ajihakikishie ushindi bila ya kungojea kujua matokeo ya mechi ya mwisho kati ya Burkina Faso na Ghana.
Hali hiyo imemfanya Kocha wa Ivory Coast, Vahid Halilhodzic kutoka Bosnia, akiri mambo ni magumu kwao, na amesema: “Tupo pagumu lakini kila kitu kipo mikononi mwetu na tutapigana!”
Nae Dede Ayew, Mtoto wa Nyota wa zamani Ghana, Abedi Ayew Pele, amenena: “Uzuri wa Kundi hili ni kuwa ukishinda mechi moja tu umesonga Raundi inayofuata! Ivory Coast ni timu nzuri na ndio wanapewa nafasi kubwa lakini uwanjani timu zote ni sawa tu!”
Timu ya Ghana imekumbwa na majeruhi kadhaa huku Veterani wao Stephen Appiah yuko nje pamoja na Kiungo Anthony Annan lakini watafarijiki na kuwasili kwa Nyota Michael Essien kujiunga na wenzake baada ya kubaki Klabuni kwake Chelsea kutibiwa misuli iliyokuwa ikimsumbua.
Mechi hii itaanza saa 3 na nusu usiku saa za bongo.
Mechi ya mwisho ya Kundi hili Ghana v Burkina Faso imehamishiwa Mji Mkuu Luanda na itachezwa Uwanja wa Novemba 11 Jumanne ijayo.
Carling Cup: Blackburn 0 Villa 1
Wakiwa ugenini Uwanja wa Ewood Park, Aston Villa wamewafunga wenyeji wao Blackburn Rovers bao 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Carling iliyochezwa Alhamisi usiku Januari 14.
Timu hizi zitarudiana tena Januari 20 huko Villa Park nyumbani kwa Aston Villa na Mshindi atakutana Fainali na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine kati ya Mahasimu Manchester City na Manchester United watakaokutana Januari 19 City of Manchester Stadium na kurudiana Old Trafford Januari 27.
Bao la ushindi la Aston Villa lilifungwa na James Milner dakika ya 23.
Vikosi vilivyoanza:
Blackburn: Robinson, Jacobsen, Samba, Nelsen, Chimbonda, Salgado, Emerton, Nzonzi, Pedersen, Dunn, Kalinic.
AKIBA: Brown, McCarthy, Reid, Olsson, Hoilett, Di Santo, Jones.
Aston Villa: Guzan, Cuellar, Collins, Dunne, Warnock, Ashley Young, Milner, Petrov, Downing, Heskey, Agbonlahor.
AKIBA: Friedel, Luke Young, Sidwell, Carew, Delph, Reo-Coker, Beye
REFA: Mark Clattenburg
Redknapp kwa Pilato!!!
• Ashitakiwa kwa kukwepa kodi!!
Aliekuwa Meneja wa Portsmouth, Harry Redknapp, ambae sasa ni Meneja Tottenham, atasimama kizimbani Februari 11 kujibu mashitaka mawili ya kudanganya umma na kutolipa kodi makosa yanayodaiwa kutendeka kati ya Aprili 1, 2002 na Novemba 28, 2007 alipokuwa Meneja wa Portsmouth.
Harry Redknapp alikuwa Meneja wa Portsmouth kwa vipindi viwili, cha kwanza kikiwa kati ya Machi 2002 hadi Novemba 2004 na cha pili kati ya Desemba 2005 hadi Oktoba 2008.
Mashitaka hayo yanafuatia uchunguzi wa Polisi na Mamlaka za Kodi uliodumu miezi 26 na inadaiwa unahusiana na malipo ya jumla ya Pauni 183,000 kutoka kwa aliekuwa Mwenyekiti wa Portsmouth Milan Mandaric kupitia akaunti ya Benki huko Monaco na hivyo kukwepa ulipaji kodi.
Redknapp ameshitakiwa pamoja na Mandaric.

Thursday 14 January 2010

KOMBE la Afrika: Angola 2 Malawi 0
• Angola juu Kundi A!!
Watoto wa nyumbani, Angola, leo wamewapa furaha kubwa Raia wao baada ya kuilaza Malawi 2-0 katika mechi ya Kundi A la Kombe la Mataifa ya Afrika iliyochezwa leo Mjini Luanda, Angola.
Flavio ndio alieungua ufungaji kwa kufunga bao la kwanza na Manucho akapachika bao lapili.
Kwa ushindi huo, Angola ni vinara wa Kundi A na wana pointi 4, wanafuata Malawi pointi 3, kisha Algeria pointi 3 na Mali pointi 1.
Mechi za mwisho Kundi hili ni Angola v Algeria na Mali v Malawi.
MECHI ZA Januari 15: [saa za Bongo]
[KUNDI B]
Burkina Faso v Togo [hamna Togo wamejitoa]]
Ivory Coast v Ghana [saa 3 na nusu usiku]
KOMBE la AFRIKA: Mali 0 Algeria 1
• Kundi A linazidi kuwa hekaheka!!!
Algeria leo wameibuka kidedea baada ya kipigo cha mechi ya kwanza walipowashwa 3-0 na Malawi na leo kuwafunga Mali waliotoka suluhu na Wenyeji Angola 4-4 kwa bao 1-0.
Bao la dakika ya 43 la Haliche ndilo limefufua matumaini ya Algeria.
Sasa baada ya mechi mbili kwa Timu hizi, Algeria wana pointi 3 na Mali pointi moja na Timu hizi zitamaliza mechi zake kwa kucheza Januari 18 Algeria watakapocheza na Angola na Mali watakutana na Malawi.
Mechi inayofuata leo ya Kundi A ni Angola v Malawi.
Pigo Kuu kwa Liverpool!!!
Licha ya kutandikwa 2-1 na “Timu ndogo” Reading hapo jana mbele ya Mashabiki wake nyumbani Anfield na hivyo kutupwa nje ya Kombe la FA, imethibitika kuwa Liverpool itawakosa Mastaa wake watatu kwa wiki kadhaa baada ya wote kuumizwa katika kipigo hicho cha jana.
Fernando Torres, alieshindwa kumaliza mechi ya jana baada ya kutolewa nje kwa maumivu katika muda usiozidi nusu kwenye mechi hiyo ya jana na Reading, inabidi afanyiwe operesheni goti lake la kulia na atakuwa nje kwa muda usiopungua wiki 6.
Nahodha Steven Gerrard yeye alidumu hadi mapumziko kwenye mechi hiyo na imethibitika ana tatizo la musuli na atakuwa nje hadi wiki mbili.
Mchezaji mwingine nyota Msimu huu, Yossi Benayoun, yeye amevunjika mbavu na atakuwa nje hadi miezi miwili.
Hayo ni mapigo makubwa sana kwa Liverpool na yanamzidishia presha kubwa Meneja Rafa Benitez huku zikiibuka tena kelele afukuzwe toka kwa baadhi ya Mashabiki wakidai kutolewa nje kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE, FA Cup, Carling Cup na kusuasua kwenye Ligi ni aibu kubwa kwao.
Leo ni Nusu Fainali ya kwanza Carling Cup
Blackburn Rovers na Aston Villa leo zinapambana kwenye mzunguko wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Carling huko Ewood Park nyumbani kwa Blackburn baada ya mechi hii kuahirishwa wiki iliyopita kutokana na barafu.
Mechi ya pili ya marudiano ya Nusu Fainali kati ya Aston Villa v Blackburn itachezwa Villa Park tarehe 20 Januari.
Nusu Fainali nyingine ni Manchester City v Manchester United na itachezwa Januari 19 huko City of Manchester Stadium na marudio ni Januari 27 huko Old Trafford.
Fergie: “Safari ya Qatar ni ya mafanikio!!”
Manchester United leo wanarudi kwao England baada ya ziara ya mazoezi ya siku 4 huko Doha, Qatar ambako walikuwa wageni wa Chuo cha Aspire.
Ziara hiyo pia ilikuwa kulikimbia baridi na barafu zilizoiandama Uingereza na kufanya mazoezi ya Timu yawe ni kwenye Jimu tu kwani nje hakuchezeki.
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, ameisifia ziara hiyo na kudai itaisaidia sana kwenye matayarisho yao ya mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu huko Old Trafford dhidi ya Burnley.
Ferguson amesema: “Ni mafanikio kuwa Qatar! Chuo cha Aspire ni cha kisasa kabisa na kinaendeshwa kitaalam na vizuri sana!”
Ferguson alimalizia kwa kusema kuwa ziara hiyo imefungua milango kwa safari nyingine na watadumisha urafiki wao na Aspire.
Jana, mazoezi ya Man U yalikuwa wazi kwa Washabiki kwenda kuyatazama na watu wengi walifurika kwenda kuwaona Mabingwa hao hapo Chuono Aspire.
Chuo cha Aspire hukuza vipaji vya Vijana toka kila pembe ya Dunia na huendeshwa na Wataalam wa hali ya juu.
Mali v Algeria
[saa 1 usiku, bongo taimu]
Leo Uwanjani Novemba 11 huko Luanda, Angola, Algeria watakuwa wakipagania kubaki kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuchapwa 3-0 na Malawi katika mechi yao ya kwanza ya Kundi A watakapocheza na Mali iliyotoka sare na Wenyeji Angola kwa bao 4-4 baada ya kuwa nyuma 4-0 huku zikiwa zimebaki dakika 12 mchezo kumalizika.
Mali leo inategemewa kumchezesha Kiungo wa Juventus Mohamed Sissoko ambae hakucheza mechi ya kwanza kwa sababu ya maumivu lakini Kocha wa Mali Stephen Keshi hakuthibitisha hilo.
Algeria, waliopigwa 3-0 na Malawi, ilibidi waiombe Nchi yao radhi kwa kipigo hicho na Mchezaji wao wa Rangers ya Scotland, Beki Madjid Bougherra ameahidi maajabu leo.
Angola v Malawi
[saa 3 na nusu, bongo taimu]
Mara baada ya Mechi ya leo kati ya Mali na Algeria kwisha ndani ya Uwanja wa Novemba 11 huko Luanda, Angola, Wenyeji Angola watajimwaga humo kuivaa Malawi na Kocha wao Manuel Jose ameahidi mchezo tofauti na ule walioiruhusu Mali kufunga bao 4 katika dakika 12 za mwisho.
Nae Kocha wa Malawi Kinnah Phiri amesema Timu yao haina wasiwasi na watatulia uwanjani.
Adebayor hajui lini ataweza kucheza!
Straika wa Manchester City ambae ni Nahodha wa Togo, Emmanuel Adebayor, alienusurika baada ya Basi la Timu ya Togo kushambuliwa kwa risasi likiwa njiani kutoka Congo na kuelekea Mjini Cabinda huko Angola na kuwaua Kocha Msaidi na Afisa Habari wa Togo na pia Dereva wa Basi hilo, amesema hana uhakika lini ataweza kucheza tena Soka baada ya kupata mstuko mkubwa.
Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amesema wao watampa muda wowote anaotaka ili kupumzika na kujijenga upya kifikra.
Mpaka wakati huu, Adebayor bado yuko kwao Lome, Togo.
Barca nje Copa del Rey!!
Licha ya kuifunga Sevilla 1-0 hapo jana, Mabingwa Watetezi wa Copa del Rey, FC Barcelona, wametupwa nje ya Kombe hilo kwa sheria ya goli la ugenini kwa vile Sevilla iliifunga Barca 2-1 huko Nou Camp nyumbani kwa Barcelona.
FA CUP: Liverpool kilio!!!
Liverpool imebwagwa nje ya Kombe la FA baada ya kuchapwa 2-1 na Reading hapo jana tena wakiwa nyumbani Anfield na machungu ya kipigo hicho yamezidishwa baada ya Mastaa wao wakubwa wanaowategemea, Steven Gerrard na Fernando Torres, kuumizwa na kulazimika kutoka na hivyo kuleta wasiwasi mkubwa huenda maumivu yao yakawa ya muda mrefu.
Liverpool walipata bao la kuongoxza kibahati pale krosi ya Steven Gerrard ilipoingizwa wavuni na Mchezaji wa Reading Ryan Bertrand.
Reading walisawazisha bao kwa penalti baada ya Liverpool kufanya madhambi ndani ya boksi.
Ndipo mechi ikapelekwa dakika 30 za nyongeza na Reading wakapata bao la pili na la ushindi kupitia Shane Long.
Mechi hii ilikuwa marudiano baada ya Timu hizi kutoka sare huko Reading kwa bao 1-1 na sasa Reading wameingia Raundi ya 4 ya Kombe hili na watacheza na Burnley.
KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA:
Chipolopolo sare na Tai wa Tunisia
Zambia na Tunisia jana zilitoka sare ya 1-1 huko Lubango, Angola katika mechi ya Kundi D.
Zambia walipata bao la kuongoza dakika ya 18 Mfungaji akiwa Jacob Mulenga lakini Tunisia walisawazisha dakika ya 40 kwa bao lilotengenezwa na Youssef Msakni na kufungwa na Souheil Dhaouadi.
Suluhu hii ya Zambia na Tunisia imewafanya Cameroun waliofungwa na Gabon 1-0 hapo jana katika mechi ya awali washike mkia kwenye Kundi hili.
Hapo Jumapili, Januari 17, Zambia wataivaa Cameroun na Tunisia watacheza na Gabon.
Cameroun yazama!!!!
Katika Uwanja wa Taifa wa Tundavala huko Lubango, Angola, Cameroun, moja wa Vigogo wa Afrika, walitolewa nishai na Gabon ambayo licha ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mara 6 haijawahi kushinda hata mechi moja katika Fainali zote hizo.
Goli la Straika wa Hull City ya Ligi Kuu England, Daniel Cousin, la dakika ya 17 ndilo liliimaliza Cameroun.
Baada ya bao hilo, Gabon, wakiongozwa na umahiri wa Kipa wao Ovono walimudu kuyazima mashambulizi yote ya Cameroun yaliyokuwa yakiongozwa na kina Samuel Eto’o, Geremi, Webo, Song na Mastaa wengineo.
VIKOSI:
GABON: Ovono, Ambouronet, Apanga, Moro Mve, Moubamba, Copa, Ndoumbou, Fabrice, Aubameyang, Cousin.
CAMEROUN: Kameni, Song, N’Koulou, Bedimo, Song Billong, Emana, Geremi, Makoun, N’Guemo, Webo, Eto’o.
Mechi zinazofuata za Timu hizi ni Januari 17 Cameroun v Zambia na Gabon v Tunisia.
MECHI ZA Januari 14: [saa za bongo]
[KUNDI D Mjini Luanda]
Mali v Algeria [saa 1 usiku]
Angola v Malawi [saa 3 na nusu usiku]
Burnley yapata Meneja mpya
Brian Laws, miaka 48, ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa Klabu iliyomo Ligi Kuu England, Burnley, kuchukua nafasi ya Owen Coyle aliehama wiki iliyokwisha kwenda Bolton Wanderers.
Laws, kabla ya uteuzi huu, alikuwa Meneja wa Sheffield Wednesday lakini alitimuliwa kazi hiyo Mwezi Desemba mwaka jana.
Kibarua cha kwanza cha Laws akiwa Burnley kitakuwa ni mpambano wa huko Old Trafford watakapowavaa Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Manchester United siku ya Jumamosi.

Wednesday 13 January 2010

‘Babu’ Sol Campbell arudi Arsenal!!!!
Sol Campbell, miaka 35, yuko katika hatua za mwisho za kurudi kuichezea tena Arsenal baada ya kukichezea Kikosi cha Akiba cha Arsenal kwa dakika 45 hapo jana kilipocheza na Kikosi cha Akiba cha West Ham.
Campbell aliichezea Arsenal kwa mara ya mwisho mwaka 2006 katika Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na kisha akahamia Portsmouth.
Alipotoka Portsmouth alikwenda Notts County lakini huko kukatokea mtafaruku na akajiondoa bila kucheza mechi hata moja na sasa ni Mchezaji huru.
Mwenyewe Campbell amesema ameshasaini Arsenal ila kumebakia kukamilisha taratibu chache na Mkataba wake utamweka hapo mpaka mwishoni mwa msimu.
Campbell amesema Arsene Wenger alimruhusu kufanya mazoezi na Arsenal kwa miezi miwili sasa na baada ya kumchunguza aliridhika kiwango bado kipo cha kucheza Arsenal na ndio maana amepewa mkataba.
KOMBE LA AFRIKA:
Leo Kundi D ni Cameroun v Gabon na Zambia v Tunisia!!
Leo saa moja usiku katika Uwanja wa Taifa wa Tundavala huko Lubango, Angola, Cameroun, moja wa Vigogo wa Afrika, watashuka dimbani kuivaa Gabon katika mechi ya Kundi D ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Cameroun, wakiongozwa na Supastaa wao Samuel Eto’o anaecheza huko Italia Klabu ya Inter Milan, ndio wanategemewa kuibuka kidedea lakini Gabon wana Wachezaji wazoefu kama vile Straika Daniel Cousin anaecheza Ligi Kuu England na Klabu ya Hull City.
Mara baada ya mechi ya Cameroun v Gabon, hapo hapo Uwanjani Tundavala, saa 3 na nusu usiku, saa za bongo, Zambia watapambana na Tunisia.
Mechi hii inategemewa kuwa ngumu kama alivyokiri Kocha wa Tunisia Faouzi Benzarti na kuungwa mkono na Nahodha wa Zambia Christopher Katongo.
Matokeo jana: Mozambique 2-2 Benin
Jana usiku, katika mechi ya pili ya Kundi C ya kugombea Kombe la Mataifa ya Afrika, Benin waliumwaga mchezo huo baada ya kuongoza 2-0 kwa mabao ya Razak Omotoyossi anaechezea FC Metz ya Ufaransa aliefunga kwa penalti dakika ya 15 na Msumbiji kujifunga wenyewe kupitia Dario Khan.
Lakini Msumbiji walijitutumua na kusawazisha kupitia mabao ya Lobo na Goncalves na kuifanya mechi iishe sare ya 2-2.

Katika mechi ya awali ya Kundi hili C, Misri ambao ndio mabingwa Watetezi, waliibwaga Nigeria 3-1.
Mechi zinazofuata kwenye Kundi hili ni Januari 16 wakati Msumbiji watakapocheza na Mabingwa Watetezi Misri na Benini kukutana na Nigeria.
KOMBE LA FA: Coventry 1 Portsmouth 2
Aaron Mokoena, Mchezaji kutoka Afrika Kusini, alifunga bao sekunde za mwisho za muda wa nyongeza na kuipa ushindi wa 2-1 Portsmouth dhidi ya Coventry katika mechi ya marudiano ya Kombe la FA hapo jana.
Leon Best aliipa Coventry bao la kuongoza lakini katika dakika ya 90, Nahodha wa Coventry Stephen Wright alijifunga mwenyewe na kuwapa sare ya 1-1 Portsmouth na hivyo mechi kuingia nusu saa ya nyongeza.
Timu hizi zilitoka sare katika mechi ya kwanza iliyochezwa Fratton Park nyumbani kwa Portsmouth na bao la Mokena limeiingiza Timu hiyo Raundi ya 4 ya FA Cup na itakutana na Sunderland.
Leo saa 4 dakika 45 usiku, saa za bongo, Liverpool watarudiana na Reading katika mechi ya Raundi ya 3 ya Kombe la FA baada ya kutoka sare katika mechi ya kwanza na mechi hii ipo nyumbani kwa Liverpool Uwanjani Anfield.
Mshindi ataingia Raundi ya 4 na atacheza na Burnley.

Tuesday 12 January 2010

Misri waibutua Nigeria!!!
Mabingwa Watetezi wa Afrika, Misri, leo wameanza kampeni yao ya kutetea taji lao murua baada ya kuibamiza Nigeria mabao 3-1 Uwanja wa Taifa wa Ombaka Benguela, Angola katika mechi ya Kundi C.
Ni Nigeria walioanza kwa kufunga bao zuri la Straika wa Hoffenheim ya Ujerumani, Chinedu Obasi, aliefumua shuti ambalo liliuparaza mkono wa Kipa hodari wa Misri El Hadari na hiyo ilikuwa ni dakika ya 12.
Mshambuliaji wa Misri Emad Moteab alisawazisha dakika ya 33 na Timu zilienda mapumziko zikiwa sare 1-1.
Kipindi cha pili, Misri iliongeza kasi na kupata bao mbili kupitia Nahodha Ahmed Hassan dakika ya 53 na Mchezaji alietoka benchi Gedo dakika ya 88.
Mechi zijazo za Timu hizi ni Januari 16 na ni Misri v Msumbiji na Nigeria v Benin.
Muda mfupi ujao, hapo hapo Ombaka, mechi ya pili ya Kundi C kati ya Msumbiji na Benin itaanza.
VIKOSI:
Egypt: El Hadari, Fathallah, Said, Moawad, Gomaa, Fathi, Abd Rabou, Ghaly, Hassan, Zidan, Moteab.
Akiba: Abdoul-Saoud, El Mohamady, Salem, El Sakka, Eid, Tawfik, Gedo, Wahid,
Shikabala, Abdelshafy, Raouf, Hamdy.
Nigeria: Enyeama, Yobo, Taiwo, Nwaneri, Mohammed, Mikel, Yussuf, Uche, Etuhu, Obasi Ogbuke, Yakubu.
Akiba: Ejide, Apam, Echiejile, Kaita, Kanu, Martins, Obinna, Odemwingie, Odiah, Olofinjana, Shittu, Aiyenugbu
MECHI ZA KESHO Januari 13: [saa za bongo]
[KUNDI D Mjini Lubango]
Cameroun v Gabon [saa 1 usiku]
Zambia v Tunisia [saa 3 na nusu usiku]
LIGI KUU England: Msongamano wa Ratiba, kiwewe cha Mameneja!!!
Waendeshaji wa Ligi Kuu wametamka kuwa watamudu kukabiliana na kutibuliwa kwa Ratiba ya mechi na baridi kali iliyoambatana na barafu nyingi iliyoikumba Uingereza na kusababisha kuahirishwa kwa mechi 7 za Ligi.
Mpaka sasa Ratiba mpya ya mechi zisizochezwa haijatoka na Ligi Kuu imesema inafanya kazi na Vilabu vinavyohusika ili kupanga upya mechi hizo.
Mbali ya mechi hizo 7 za Ligi Kuu kukumbwa na kuahirishwa, pia mechi za Nusu Fainali za Kombe la Carling nazo ziliahirishwa.
Lakini mechi hizo za Carling tayari zimeshapangwa upya na mzunguko wake wa kwanza utachezwa Jumanne na Jumatano ijayo.
Licha ya kutamka kuwa itamudu kupanga Ratiba upya, Ligi Kuu inabanwa na makubaliano yao na FA, UEFA na Wadhamini wa Makombe ya FA na Carling yanayohusu Ratiba ambayo yanawataka kutoa kipaumbele kwa mechi za UEFA CHAMPIONS LEAGUE, EUROPA LIGI na Makombe ya FA na Carling na hivyo kutokupanga mechi za Ligi Kuu siku ambazo mechi za UEFA, FA Cup na Carling Cup zinachezwa.
Ugumu mwingine wa kuipanga upya Ratiba ya Ligi Kuu unakuja kwa vile Msimu huu Ligi Kuu inatakiwa imalizike wiki moja kabla ya kawaida yake ili kuipa nafasi Timu ya Taifa ya England kufanya matayarisho mazuri kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza Juni 11 huko Afrika Kusini.
Kwa hilo, Ligi Kuu haiwezi kuongezwa mbele ya tarehe 9 Mei ambayo inatakiwa kwisha.
Mechi pekee zitakazochezwa na Klabu za England baada ya tarehe 9 Mei ni Fainali ya Kombe la FA hapo Mei 15 na, pengine, Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE hapo Me1 22 endapo Klabu ya England itaingia hiyo Fainali ambayo kwa mara ya kwanza itachezwa Jumamosi badala ya Jumatano tuliyoizoea.
Mkanganyo huu wa Ratiba kupangwa upya umewatia kiwewe baadhi ya Mameneja wa Klabu za Ligi Kuu ambao wanahofia kupangiwa kucheza hadi mechi 5 ndani ya siku 14.
Meneja wa Tottenham Harry Redknapp amesema: “Huwezi kujua. Ratiba inaweza kukupendelea na kukubeba au kuua Msimu wako wote!”
Wasiwasi kama huo pia umeonyeshwa na Arsene Wenger wa Arsenal ambae alitaka mechi zote zilizotakiwa kuchezwa wikiendi ambayo baadhi ya mechi ziliahirishwa zisichezwe ili kuleta usawa kwa Timu zote.
Fergie afurahishwa na Kambi yake Doha


Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambae yuko pamoja na Kikosi chake chote Mjini Doha, Qatar kwa ajili ya Kambi ya Mazoezi kwenye Chuo cha Aspire [pichani] amekisifia sana Chuo hicho kwa mapokezi mazuri na pia kwa kuwa na vifaa vya kisasa vya mazoezi.
Manchester United wapo Doha tangu juzi na watakaa huko kwa siku 4 na hii imekuwa ni nafasi nzuri sana kwao kufanya mazoezi katika hali ya hewa ya joto kidogo ukilinganisha na England ambako sasa ni barafu tu iliyotanda kila sehemu ambayo imefanya mazoezi kwenye Viwanja vya nje kutofanyika.
Kikosi hicho cha Man U kitaondoka Doha Alhamisi na Jumamosi kitaingia Uwanjani kwao Old Trafford kucheza na Burnley kwenye Ligi Kuu.
Misri v Nigeria
Mechi hii ya Vigogo wa Afrika itachezwa leo saa 1 usiku, saa za bongo, Uwanja wa Taifa wa Ombaka Mjini Benguela, Angola.
Hii ni mechi ya Kundi C na Mabingwa Watetezi wa Afrika, Misri, wataanza utetezi wa taji lao dhidi ya Timu ngumu Nigeria huku wakiwa na upungufu mkubwa kwenye Kikosi chao kwa kuwakosa Mastaa Mido, Amr Zaki na Mohammed Aboutrika ambao wameachwa kwa vile ni majeruhi.
Kumekuwa na utata kuhusu Kambi ya Nigeria, yenye Mastaa wakubwa kina Yakubu Ayegbeni , Obafemi Martens, Kanu na wengineo, huku kukiibuka minong’ono kuwa kuna mtafuruku mkubwa kambini lakini Kanu amezikanusha vikali taarifa hizo.
Msumbiji v Benin
Mara baada ya patashika ya Misri v Nigeria, Uwanjani hapo hapo Ombaka, Msumbiji wataingia kupambana na Benin katika mechi ya pili ya Kundi C itakayoanza saa 3 na nusu usiku saa za bongo.
Kocha wa Msumbiji kutoka Uholanza, Mart Nooij, amesema Kikosi chake kipo imara na wanajiamini.
Nao Benin watamtegemea sana Straika wao Razak Omotoyossi anaechezea FC Metz ya huko Ufaransa.
Man City yaikwaa nafasi ya 4 Ligi Kuu!!
• Man City 4 Blackburn 1
Magoli matatu yaliyofungwa na Mchezaji anaeng’ara sana kwa sasa hivi, Carlos Tevez, na moja la Beki Micah Richards, yamewapa ushindi mnono Manchester City Uwanjani kwao City of Manchester baada ya kuwatwanga Blackburn Rovers mabao 4-1 kwenye mechi ya Ligi Kuu hapo jana usiku na hivyo kuifanya Man City iikwae nafasi ya 4 kwenye Ligi.
Carlos Tevez alifunga mabao yake matatu dakika za 7, 49 na 90. Richards alipachika la kwake dakika ya 39.
Goli pekee la Blackburn lilifungwa na Pedersen dakika ya 71.
Van der Sar arudi mazoezini Man U!!
Kipa Nambari Wani wa Manchester United Edwin Van der Sar hapo sasa ameanza mazoezi na Timu yake tangu aenda kumuuguza Mkewe mwezi uliopita baada ya kupewa likizo ya dharura na Man U kufuatia kuugua ghafla kwa Mkewe huko kwao Uholanzi.
Kabla ya kupata dharura hiyo, Van der Sar alikuwa hajaidakia Man U tangu Novemba 21 walipoifunga Everton 3-0 na akaumia goti kwenye mechi hiyo.
Van der Sar yupo kwenye Kikosi cha Manchester United kilichotua Doha, Qatar hapo juzi kwa mazoezi ya siku 4.
Kipa wa Akiba Tomasz Kuszczak ndie alikuwa akiidakia Man U kwa kipindi chote Van der Sar alichokosekana.

Monday 11 January 2010

NGOMA NGUMU: Ivory Coast 0 Burkina Faso 0
Mjini Cabinda, Mji uliokumbwa na msiba mkubwa kufuatia vifo vilivyotokea baada ya Basi la Timu ya Togo kupigwa risasi na Waasi, leo mechi ya kwanza ya Kundi B kati ya Ivory Coast na Burkina Faso ilichezwa na hakuna mbabe aliepatikana baada ya kutoka sare ya 0-0.
Mechi nyingine ya Kundi hili iliyotakiwa kuchezwa kati ya Ghana na Togo haifanyiki kwa vile Togo wamejitoa na kurudi kwao kwa mazishi ya Kocha wao Msaidizi na Afisa Habari wa Timu.
Ivory Coast walistahili kushinda mechi hii kwa vile waliitawala na kuwabana Burkina Faso nusu uwanja lakini Kikosi chao kilichojaa Mastaa kina Drogba, Kone, Yaya Toure, Kolo Toure, Eboue, Kalou na Dindane kilishindwa kupata hata kigoli cha babu.
Sasa Ivory Coast wana kimbembe kikubwa hapo Januari 15 watakapovaana na Timu ngumu Ghana.
MECHI ZA KESHO Januari 12: [saa za bongo]
[KUNDI C Mjini Benguela]
Egypt v Nigeria [saa 1 usiku]
Mozambique v Benin [saa 3 na nusu usiku]
Malawi 3 Algeria 0
Malawi leo huko Luanda, Angola iliistua Afrika na Dunia nzima pale ilipoifumua Timu ya kutegemewa Algeria mabao 3-0 katika mechi ya Kundi A ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Malawi walipata bao lao la kwanza dakika ya 17 kupitia Russel Mwafulirwa na Elvis Kafoteka akaongeza la pili na kuifanya Malawi iwe mbele 2-0 hadi mapumziko.
David Banda akapachika bao la 3 kipindi cha pili dakika ya 50 ya mchezo.
Kipigo hicho cha Algeria, Timu ambayo ndiyo iliwabwaga Misri, Mabingwa wa Afrika, nje ya Kombe la Dunia na kuwaingiza wao Fainali za Kombe la Dunia, ni maajabu kwa wengi.
Katika mechi zijazo za Kundi hili Angola watacheza na Malawi na Algeria watapambana na Mali mechi ambazo zitachezwa Januari 14.
Mkurugenzi Liverpool ajiuzulu baada ya kumtusi Shabiki!!!
• Ni Mtoto wa Mmiliki wa Liverpool Tom Hicks!!
Chama cha Washabiki wa Liverpool kiitwacho ‘Spirit of Shankly’ kimetoa shinikizo kubwa na kusababisha Mtoto wa mmoja wa Wamiliki wa Klabu hiyo Tom Hicks ambae pia jina lake ni Tom Hicks, Junior, miaka 39, na ambae ni Mkurugenzi wa Bodi ya Liverpool, kujiuzulu baada ya kumtumia Shabiki mmoja wa Liverpool barua pepe yenye matusi ikiwa ni majibu kwa Shabiki huyo aliehoji Madeni na hatima ya Timu yao kufuatia kutofanya vizuri uwanjani.
Barua pepe hiyo ilimwita Shabiki huyo ‘mpumbavu’ na kuandamana na matusi na kumalizia na kauli ‘nenda jehanamu, unanitia kichefuchefu!’
Ndipo Chama cha Mashabiki wa Liverpool walipomtaka Mkurugenzi huyo Tom Hicks, Junior, kuchukua ‘njia ya kiungwana na kujiuzulu’.
Liverpool inamilikiwa na Baba yake Tom Hicks Junior, aitwae Tom Hicks ambae ni Mmarekani, pamoja na Mmmarekani mwenzake aitwae David Gillett na Wamarekani wote hao wawili wanapingwa vikali na Kundi hilo la Mashabiki ‘Spirit of Shankly’ lenye dhamira ya kuwang’oa.
Jina la Kundi hilo la Mashabiki linatokana na Bill Shankly aliekuwa Meneja shupavu wa Liverpool miaka ya 80 alieleta mafanikio makubwa kwa Klabu hiyo kwa kuiwezesha kutwaa Mataji mengi ya Ubingwa wa England na Ulaya.
Man U yatangaza faida!!!
Manchester United wametangaza faida kwa Mwaka wa Fedha ulioisha Juni 20, 2009 ya Pauni Milioni 48 na pia wametaja mipango yao ya kuzalisha Pauni Milioni 500 kwa kuuza Hati za Dhamana za Klabu hiyo yenye mvuto mkubwa Duniani kote.
Faida hiyo imepigwa jeki hasa kwa mauzo ya Mchezaji Cristiano Ronaldo kwa Real Madrid ya Spain waliemnunua kwa zaidi ya Pauni Milioni 80 mwaka jana.
Wakati huo huo, Manchester United imethibitisha kuwa Msimu ujao Kampuni kubwa ya Kifedha huko Marekani, Aon, ndio watakuwa Wadhamini wa Jezi badala ya AIG na jina la AON ndilo litakuwa kifuani mwa Jezi za Man U.
LIGI KUU England leo: Manchester City v Blackburn Rovers
Manchester City leo watawakaribisha Blackburn Rovers Uwanjani kwao City of Manchester kwenye mechi pekee ya Ligi Kuu ambayo Mastafu wa Man City hapo uwanjani imebidi wafanye kazi ya ziada kuondoa barafu na kusafisha ili kuinusuru mechi hiyo isiahirishwe kama ilivyofanyika kwa mechi nyingi wikiendi hii iliyopita.
Ushindi kwa Man City leo utawafanya wawapiku Tottenham na kushika nafasi ya 4 kwenye msimamo wa Ligi na pia kuendeleza wimbi lao la ushindi la mechi 4 sasa huku Mchezaji wao Carlos Tevez akifunga kila mechi hivi karibuni na kumfanya apewe Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu kwa mwezi Desemba.
Patrick Vieira, Mchezaji mpya wa Man City waliemchukua kutoka Inter Milan kwa mkopo wa miezi 6, leo atashindwa kucheza mechi yake ya kwanza kwa vile ana maumivu ya musuli.
Vilevile, Man City itawakosa kina Shaun Wright-Phillips, Joleon Lescott, Nedum Onuoha na Stephen Ireland kwa kuwa wote ni majeruhi.
Pia, Kolo Toure na Emmanuel Adebayor hawatakuwemo kwa vile wako kwenye Timu zao za Taifa kwa ajili ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika huko Angola ingawa Adebayor sasa amerudi kwao Togo baada ya Timu hiyo kupata msiba mkubwa huko Angola.
Blackburn itawakosa Vince Grella ambae ni majeruhi na El-Hadji Diouf ambae amefungiwa baada ya kutwangwa Kadi Nyekundu katika mechi ilyopita ya Kombe la FA Blackburn waliyofungwa na Aston Villa.
VIKOSI VINATEMEGEWA KUWA:
Man City: Given, Zabaleta, Boyata, Kompany, Sylvinho, Wright-Phillips, De Jong, Barry, Petrov, Bellamy, Tevez.
Blackburn: Robinson, Chimbonda, Nelsen, Samba, Givet, Emerton, Andrews, N'Zonzi, Pedersen, McCarthy, Roberts.
KOMBE LA AFRIKA: Togo warudi kwao kwa mazishi, maombolezo siku 3!!
  • Wataka kurudi tena Angola wakimaliza msiba, CAF yagoma!!!
Wakati mechi ya ufunguzi kati ya Wenyeji Angola na Mali ikianza huko Luanda Mji mkuu wa Angola hapo jana usiku, Timu ya Togo ilikuwa njiani kwenda Uwanja wa Ndege wa Cabinda, Angola ili kupanda Ndege waliyoletewa na Rais wa Nchi yao, Faure Gnassingbe, ili kurudi kwao huku wakiibeba miili ya wenzao wawili waliouwa kwenye shambulizi la la risasi wakiwa kwenye Basi hapo majuzi mara tu baada ya kuingia Angola wakitokea Congo.
Kikosi hicho cha Togo kiliamriwa kurudi Togo kwa mazishi na maombolezo ya siku 3 yaliyotangazwa na Nchi yao.
Hata hivyo, Waziri wa Michezo wa Togo, Christophe Tchao, alisema wameiomba CAF kurekebisha Ratiba ili waweze kurudi Angola baada ya mazishi na maombolezo lakini CAF inaelekea haitakubali ombi hilo.
Togo walikuwa leo wacheze na Ghana kwenye mechi ya Kundi B.
MECHI ZA LEO: Jumatatu Januari 11 [saa za bongo]
KUNDI A [Luanda]
Malawi v Algeria [saa 10 dk 45 jioni]
KUNDI B [Cabinda]
Ivory Coast v Burkina Faso [saa 1 usiku]
Ghana v Togo [Hamna mechi, Togo imejitoa]
Manchester United ndani ya Doha, Qatar!!

Kikosi kamili cha Mabingwa wa England Manchester United jana jioni kilitua Doha, Qatar ili kufanya mazoezi ya siku 4 wakiwa wageni wa Kituo cha Mafunzo ya Michezo cha Aspire ambacho ni spesheli kwa kukuza vipaji vya Vijana toka kila pembe ya Dunia.
Pichani ni Wachezaji wa Man U wakishuka toka kwenye Ndege Uwanja wa Kimataifa wa Doha [Picha ni toka Gulf Times, Qatar].
Manchester United wamelazimika kuja Doha ili kuikwepa hali ya hewa ya baridi kali na barafu nyingi iliyoikumba Uingereza ambayo imesababisha Michezo mingi kutochezeka na mazoezi kutofanyika kwenye Viwanja vya nje na hivyo kulazimisha Timu kufanya mazoezi kwenye Jimu tu.
Mabingwa hao kwa sasa wako nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu wakiwa pointi moja nyuma ya Chelsea na pia wapo Nusu Fainali ya Carling Cup na watacheza na Mahasimu wao wakubwa Manchester City wiki ijayo.
Vilevile, mwezi ujao watamenyena na AC Milan katika Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Mechi ambazo zinawakabili Man U hivi karibuni ni:
-Jumamosi, Januari 16: LIGI KUU: Man U v Burnley
-Jumanne, Januari 19: CARLING CUP: Man City v Man U
-Jumamosi, Januari 23: LIGI KUU: Man U v Hull
-Jumatano, Januari 27: CARLING CUP: Man U v Man City
-Jumamosi, Januari 31: LIGI KUU: Arsenal v Man U
Angola 4 Mali 4
Katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Mataifa ya Afrika huko Luanda, Angola, Wenyeji Angola na Mali walitoka sare 4-4
Angola itabidi wajilaumu wenyewe kwani walikuwa mbele kwa bao 4-0 lakini Mali wakarudisha bao zote.
Mpaka mapumziko Angola walikuwa mbele kwa bao 2-0 zilizofungwa na Flavio anaechezea Al Ahli ya Misri kwenye dakika ya 37 na 42.
Kipindi cha pili Angola wakaongeza bao nyingine mbili zote zikiwa za penalti Wafungaji wakiwa Gilberto, anaechezea Al Ahli kama Flavio, na Manucho, Mchezaji wa zamani wa Manchester United ambae sasa yuko Spain.
Mali walipata bao lao la kwanza dakika ya 78 ambalo alifunga Seydou Keita na Freddy Kanoute akafunga la pili dakika ya 87.
Bao la tatu la Mali lilifungwa tena na Seydou Keita dakika ya 89 na Mali wakasawazisha dakika ya 93 kupitia Mustapha Yatabare.
Mechi inayofuata kwa Kundi hili A ni kesho kati ya Algeria na Malawi na kisha Januari 14 Angola v Malawi na Mali v Algeria.
VIKOSI:
Angola: Fernandes, Mabina, Kali, Rui Marques, Stelvio, Xara, Dede, Zuela, Gilberto, Flavio, Manucho.
Mali: Sidibe, Diamountene, Berthe, Tamboura, Soumare, Diarra, Traore, Traore, Bagayoko, Maiga, Kanoute
MECHI ZA KESHO Januari 11:
[KUNDI A]
Malawi v Algeria
[KUNDI B]
Ivory Coast v Burkina Faso
Ghana v Togo [Togo imejitoa]

Sunday 10 January 2010

SAKATA LA TOGO KOMBE LA AFRIKA:
  • Adebayor: “Tunarudi nyumbani!”
Nahodha wa Timu ya Togo, Emmaneuel Adebayor, amethibitisha Togo inarudi kwao baada ya kuamrishwa na Serikali yao kufuatia amri ya Waziri Mkuu Gilbrert Houngbo licha ya Wachezaji kukubaliana kwa kauli moja kuendelea kucheza Kombe la Afrika ili kuwaenzi wenzao waliouawa.
Basi lililokuwa likiwasafirisha Wachezaji wa Togo kutoka Congo lilishambuliwa kwa risasi mara ya baada ya kuingia jimboni Cabinda Nchini Angola na Dereva wake akauawa pamoja na Kocha Msaidizi na Afisa Habari wa Togo.
Shambulio hilo linasemekana imefanywa na Waasi wa Cabinda wanaopigania uhuru wa Jimbo hilo tajiri kwa mafuta.
Wachezaji wengine wawili walijeruhiwa vibaya na ilibidi wafanyiwe operesheni.
Adebayor pia amethibitisha kuwa Rais wa Togo Faure Gnassingbe ametuma Ndege yake ili kukisafirisha Kikosi cha Togo toka Cabinda hadi kwao Togo.
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yataanza rasmi leo usiku saa 4, saa za bongo, kwa pambano kati ya Wenyeji Angola na Mali litakalofanyika Mji Mkuu wa Angola, Luanda.
LIGI KUU England: Arsenal na Man U chupuchupu jana!!!!!
• Nini Wenger na Fergie wamesema baada ya sare zao?
Katika mechi mbili pekee za Ligi Kuu zilizochezwa jana, huku nyingine 7 kuahirishwa, Timu za Manchester United na Arsenal, ambazo ziko nafasi ya pili na ya tatu, zote ziliponea chupuchupu kufungwa na zote kulazimisha sare na hivyo kushindwa kuwakaribia vinara Chelsea ambao mechi yao na Hull haikuchezwa kwa ajili ya barafu.
Mpaka sasa Chelsea yuko juu akiwa amecheza mechi 20 na pointi 45 mkononi, Man U ni wa pili mechi 21 na pointi 44 na Arsenal ni watatu kwa mechi 20 na pointi 42.
Arsene Wenger wa Arsenal, ambayo Timu yake ilitoka nyuma mara mbili na kuambua suluhu ya 2-2 na Everton, alikiri Everton iliwazidi kila kitu na walibahatika kupata pointi moja.
Wenger alisema: “Walituzuia tusitandaze soka letu la kawaida! Walipokuwa mbele 2-1 nusura wapate la 3 lakini ni bahati na sisi hatukukata tamaa na tukarudisha ikawa 2-2!”
David Moyes wa Everton alisikitishwa na Timu yake kupoteza pointi 3 walipowaruhusu Arsenal kusawazisha dakika za majeruhi na hasa alikiri hawakuwa na bahati kwani goli mbili zote za Arsenal zilitokana na mikwaju iliyowababatiza Mabeki wake na kumhadaa Kipa wake Tim Howard.
Nae Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, licha ya kumsifia Meneja wa Birmigham Alex McLeish, ambae aliwahi kuwa Mchezaji wake wakati yeye ni Kocha wa Aberdeen ya Scotland, kwa kuisuka vyema Birmingham na kuifanya haijafungwa katika mechi 12 mfululizo za Ligi Kuu, pia alimlaumu Mwamuzi Mark Clattenburg.
Ingawa Manchester United walitawala kipindi chote cha kwanza, ni Birmingham ndio walifunga bao dakika ya 39 kupitia Cameron Jerome na Man U wakasawazisha dakika ya 63 kwa goli la kujifunga wenyewe baada ya krosi ya Evra kuingizwa wavuni na Beki wa Birmingham Scott Dann.
Lakini Mshika Kibendera alilikataa bao hilo kwa kuashiria Rooney yupo ofsaidi na ndipo yakaanza majadiliano kati ya Refa Clattenburg na Mshika Kibendera huyo kisha Refa Clattenburg akampiku Msaidizi wake na kuamua ni goli.
Katika mechi hiyo, Refa Clattenburg alimtwanga Darren Fletcher wa Man U Kadi mbili za Njano na hivyo kumtoa nje kwa Kadi Nyekundu na kuwaacha wengi wakiishangaa ile Kadi ya pili ya Njano ambayo haikustahili.
Ferguson alizungumzia maamuzi ya Waamuzi wa mechi hiyo: “Sijawahi kuona Mchezaji anatolewa nje kwa rafu ya aina ile! Ni upuuzi mkubwa! Nimekuwa nikimtazama Refa Clattenburg msimu huu na alichezesha mechi ya Arsenal v Tottenham ambayo pengine ilihitajika mtu amtwange mwenzake na shoka ndipo Clattenburg atoe Kadi lakini mechi yetu anamtoa mtu kwa kitu kidogo na cha ajabu!”
Ferguson akaongeza: “Kulikuwa na maamuzi ya ajabu mle! Mshika Kibendera anatoa ofsaidi kwa goli la kujifunga wenyewe! Uliona wapi goli la kujifunga mwenyewe lina ofsaidi?”
Hata hivyo Ferguson amesema wanashkuru kuambulia pointi moja kwani Birmingham chini ya Mchezaji wake wa zamani Alex McLeish ni kiboko.
Katika mechi hiyo ya jana, Sir Alex Ferguson aliweka rekodi mpya kwa kubadilisha Timu katika kila mechi katika mechi 100 mfululizo walizocheza mpaka jana na kufanya katika kila mechi hizo 100 kinashuka Kikosi cha Wachezaji tofauti.
Pengine ubadilishaji huo unaonyesha Man U ina Wachezaji wengi lakini Wadau wengi wanalalamikia hilo linadidimiza uchezaji wa Timu kwani Wachezaji wanakuwa hawachezi kitimu kwani hawaelewani vizuri.
KOMBE LA AFRIKA: Laanza leo, majonzi na utata vyatawala!
• Hamna uhakika Togo imejitoa au la!!
Leo saa 4 usiku, saa za bongo, Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yataanza rasmi kwa Wenyeji Angola kucheza na Mali Mjini Luanda, Angola lakini furaha za uzinduzi wa Michuano hii mikubwa Barani Afrika imefunikwa na msiba mkubwa uliotokea baada ya Basi lilobeba Timu ya Togo kushambuliwa kwa risasi muda mfupi baada ya kuvuka mpaka wa Congo na Angola Jimboni Cabinda na kusababisha vifo vya Dereva wa Basi hilo, Kocha Msaidizi na Afisa Habari wa Togo na pia kuwajeruhi Wachezaji wawili.
Awali, Timu ya Togo, ikiongozwa na Nahodha Emmanuel Adebayor, walitangaza kujitoa Mashindanoni lakini leo asubuhi Wachezaji wa Timu hiyo wakatangaza ili kuwaenzi wenzao waliouawa na kujeruhiwa watacheza kishujaa michuano hiyo.
Mara baada ya kuibuka taarifa za Togo kuendelea na Mashindano, Serikali ya Togo ikatoa amri kupitia Waziri Mkuu Gilbert Houngbo kuwa hawaruhusiwi kucheza na lazima warudi nyumbani.
Inasemekana Serikali ya Togo imetuma ndege kuwarudisha Wachezaji wao nyumbani.
Wakati sakata la Togo likiendelea, Serikali ya Angola imeimarisha ulinzi kila kona na ufunguzi rasmi wa Mashindano haya utafanyika baadae leo na kufuatiwa na Mechi ya Kundi A, ambalo limepangiwa Mji wa Luanda, kati ya Angola na Mali.
Katika Kundi A pia wamo Algeria na Malawi.
Mbali ya Mji Mkuu wa Angola, Luanda, michezo mingine ya Makundi mengine imepangiwa kwenye Miji mingine mitatu.
Kundi B la Togo, Ivory Coast, Ghana na Burkina Faso lipo Mjini Cabinda.
Kundi C la Misri, Benin, Mozambique na Nigeria lipo Benguela.
Kundi D la Cameroun, Gabon, Tunisia na Zambia lipo Lubango.
RATIBA KAMILI:
Januari 10:
[KUNDI A]
Angola v Mali
Januari 11:
[KUNDI A]
Malawi v Algeria
[KUNDI B]
Ivory Coast v Burkina Faso
Ghana v Togo
Januari 12:
[KUNDI C]
Egypt v Nigeria
Mozambique v Benini [
Januari 13:
[KUNDI D]
Cameroun v Gabon
Zambia v Tunisia
Januari 14:
[KUNDI A]
Mali v Algeria
Angola v Malawi
Januari 15:
[KUNDI B]
Burkina Faso v Togo
Ivory Coast v Ghana
Januari 16:
[KUNDI C]
Nigeria v Benin
Egypt v Mozambique
Januari 17:
[KUNDI D]
Gabon v Tunisia
Cameroun v Zambia
Januari 18:
[KUNDI A]
Angola v Algeria
Mali v Malawi
Januari 19:
[KUNDI B]
Burkina Faso v Ghana
Ivory Coast v Togo
Januari 20:
[KUNDI C]
Egypt v Benin
Nigeria v Mozambique
Januari 21:
[KUNDI D]
Gabon v Zambia
Cameroun v Tunisia
Powered By Blogger