Saturday, 13 September 2008

CHELSEA WAIFUNGA MAN CITY 3-1!

-Nahodha wao John Terry azawadiwa KADI NYEKUNDU!

-Robinho afunga goli la kwanza kwa timu yake mpya Man City!

Katika mechi ya mwisho ya leo ya LIGI KUU UINGEREZA Man City wakicheza nyumbani walifungwa 3-1 na Chelsea.
Robinho akiichezea Man City mechi yake ya kwanza alifunga bao la kwanza la mechi hii na la pekee kwa timu hiyo huku Shaun Wright-Phillips akiwa dhahiri mchezaji bora kwa Man City.
Nahodha wa Chelsea John Terry ambae pia ni Nahodha wa Timu ya Uingereza alipewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Jo na hivyo ataikosa mechi ya wiki ijayo na Manchester United.

ADEBAYOR APIGA GOLI 3!!

Blackburn 0 Arsenal 4

Emmanuel Adebayor aliweka bao 3 mguuni na kuwawezesha Arsenal kushinda mabao 4-0 zidi ya Blackburn katika mechi waliyocheza nyumbani kwa Blackburn kwenye Uwanja wa Ewood Park.
Bao jingine moja la Arsenal alifunga Van Persie.
Katika mechi hii tineja Theo Walcott alikuwa nyota tena kama alivyong'ara Jumatano alipochezea Timu ya Taifa ya Uingereza.
Lakini mechi hii ilipata kivutio pekee pale Bosi wa Arsenal Arsene Wenger alipomuingiza mtoto wa miaka 16 Aaron Ramsey ambae mara baada ya kuingia alimtengenezea pasi supa Adebayor aliefunga bao la nne.

MATOKEO MECHI NYINGINE NI:

FULHAM 2 BOLTON 1,

NEWCASTLE 1 HULL 2,

PORTSMOUTH 2 MIDDLESBROUGH 1,

WEST BROM 3 WEST HAM 2,

WIGAN 1 SUNDERLAND 1,

MAN CITY v CHELSEA kuanza muda si mrefu!!!
Muda si mrefu mechi inayongojewa kwa hamu ambayo ni ya kwanza kwa staa wa Brazil Robinho akichezea timu yake mpya ya Manchester City kwenye Uwanja wa kwao City of Manchester wakipambana na timu inayoongozwa na Mbrazi Luis Felipe Scolari timu ngumu ya Chelsea itaanza.
Matokeo tutawaletea baadae.

FERGUSON ASIKITISHWA NA MCHEZO HAFIFU WA MAN U!
-ASEMA: 'Tulishindwa kuhimili mikikimikiki, nguvu na rafu zao!!'
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesikitishwa na kiwango cha timu yake kwenye mechi waliyofungwa na Liverpool kwa mabao 2-1 nyumbani kwa Liverpool Uwanja wa Anfield.
Ferguson alisema mbali ya pengine Rio Ferdinand hakuna hata mchezaji mmoja aliecheza kwa kiwango na hilo lilimsikitisha sana.
Vilevile alisikitishwa na jinsi timu yake ilivyokuwa inajihami na kulaumu kuwa makosa ya ulinzi mbovu ndio yalisababisha magoli yote mawili.
Ferguson alitamka: 'Hutegemei hayo yote kwa timu kama Manchester United! Ilikuwa siku mbaya lakini hata tukiwa na siku mbaya huwa hatutoki mikono mitupu! Kiini cha kufungwa ni sisi kushindwa kukabiliana na mikiki, nguvu na rafu zao! Lazima uwape hongera kwa hilo lakini tulitakiwa tuhimili na kudhibiti hayo!
Bosi huyo wa Mabingwa Man U pia hakufurahishwa na Vidic kupewa kadi mbili za njano ambazo zilimaanisha kadi nyekundu kwa kudai Refa alishindwa kumpa hata kadi moja Carragher wa Liverpool aliekuwa akifanya faulo kama hizo mechi nzima.
LIVERPOOL 2 MAN U 1 !




Leo Liverpool wameonja ushindi ambao hawajahi kuupata kwa Man U toka Novemba, 2001 wakati mchezaji wao Danny Murphy alipofunga bao moja la penalti!
Mabingwa wa LIGI KUU Man U wakicheza ugenini Uwanja wa Anfield nyumbani kwa Liverpool ndio waliopata bao la kwanza lilofungwa na Carlos Tevez baada ya kazi murua ya Mchezaji mpya Dimitar Berbatov kwenye dakika ya 3.
Liverpool walisawazisha kwa goli la kujifunga mwenyewe la Wes Brown baada ya makosa makubwa ya Kipa Edwin van der Sar wa Man U.
Kipindi cha pili makosa ya Ryan Giggs kutegea mpira utoke yaliwapa mwanya Liverpool kumiliki mpira na Babel akaweka bao la pili.
Beki wa kutegemewa Nemanja Vidic alipewa kadi ya pili ya njano ingawa wengi wanaamini haikustahili na hivyo kulazimika kutoka kwa kadi nyekundu.

Friday, 12 September 2008

WAKATI WEST HAM WAMKARIBISHA MENEJA MPYA ZOLA, MDHAMINI WAO AWA MUFILISI!!

Wakati Klabu ya West Ham inatangaza rasmi kuwa Mtaliana Gianfranco Zola ndie Meneja mpya kuchukua nafasi ya Alan Curbishley alietimka kufuatia mfarakano na uongozi wa juu kuhusu uuzaji Wachezaji, Mfadhili mkuu wa Klabu hiyo XL Holidays ambayo kiukubwa ni ya tatu katika nyanja ya usafirishaji Watalii huko Uingereza imetangazwa kufilisika.
Jezi za West Ham zilikuwa na maandishi XL kifuani na Jumamosi kwenye mechi yao na West Bromwich watacheza wakivaa jezi zisizokuwa na maandishi hayo kifuani.


West Ham walikuwa na mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya XL Holidays wenye thamani ya Pauni Milioni 7 na nusu.
Klabu hiyo ililipwa Pauni Milioni 2 na nusu Februari, 2007 na baada ya hapo haikulipwa chochote na kuna madai mmiliki wa West Ham vilevile ni muhusika wa Kampuni hiyo mufilisi ya XL Holidays.
WENGER AWASHTUMU WAMILIKI WAPYA WA MAN CITY: 'Lazima waheshimu taratibu! Soka sio supamaketi!!'
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameibuka na kuwaponda Wamiliki wapya wa Manchester City, Kampuni ya Abu Dhabi, Falme za Nchi za Kiarabu, iitwayo ABU DHABI UNITED GROUP, ambayo inasemekana ni mali ya Familia ya Kifalme huko Abu Dhabi, kwa majigambo yao kwamba ifikapo Januari watawanunua Cristiano Ronaldo, Cesc Fabregas, Fernando Torres nk, na kuifanya klabu hiyo kuwa kubwa kupita zote duniani.
Wenger alifoka: 'Kuna sheria! Lazima ziheshimike!'
'Huwezi kuibuka na kudai ntamlipa Ronaldo Pauni 250,000 kwa wiki na ntamnunua kwa Pauni Milioni 135 wakati ana mkataba na Man U!'
Wenger aliongeza kubwata:'Soka sio supamaketi!'
Wakati huohuo kuna taarifa kwamba aliekaririwa akitoa kauli hizo za kununua Wachezaji nyota mara baada ya kutangazwa kuinunua Man City ambae ni kiongozi mwandamizi wa Kampuni hiyo ya Abu Dhabi, Dr Sulaiman Al Fahim, amewekwa pembeni na tajiri na mmiliki hasa wa kampuni hiyo, SHEIKH Mansour bin Zahed Al Nahyan ambae ni mtoto wa muasisi wa nchi ya Falme za Nchi za Kiarabu na anaesifika sana kama mpenzi wa kweli wa soka na mtu asiependa makuu na sifa za kipuuzi.
LIGI KUU UINGEREZA YARUDI DIMBANI KESHO JUMAMOSI!!!!
Baada ya Mechi za kimataifa za kugombea nafasi za kuingia Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010 zilizochezwa wikiendi iliyopita na katikati ya wiki sasa LIGI KUU inarudi tena kesho kwa pambano la watani wa jadi la kukata na shoka kati ya Liverpool na Mabingwa wa LIGI KUU Manchester United mechi itakayochezwa saa 8 dakika 45 mchana saa za bongo Uwanja wa Anfield nyumbani kwa Liverpool.
Wabongo wataiona mechi hii laivu kupitia GTV kwenye chaneli ya GS1.
Mechi hii itakuwa kivutio kikubwa kwani washabiki wengi wana shauku kumuona mchezaji mpya wa Man U Dimitar Berbatov akishirikiana na kina Wayne Rooney na Carlos Tevez kuongoza mashambulizi.
Mechi nyingine inayongojewa kwa hamu ni kumuona mchezaji mpya Robinho wa Manchester City akiikaribisha Chelsea timu aliyoiponda dakika za mwisho na kujiunga Man City badala yake. Pia atakuwemo Shaun Wright-Phillips aliekuwa Chelsea na sasa yuko Man City timu aliyokuwa akicheza kabla ya kwenda huko Chelsea.
Mechi hii iko laivu GTV chaneli ya GS1 kuanzia saa 1 na nusu usiku bongo time.
Wale wapambe wa Arsenal bila shaka watataka kumuona chipukizi wao Theo Walcott akionyesha maajabu yaliyowaua Croatia Jumatano wakati alipochezea Uingereza katika mechi Croatia waliyopigwa 4-1 nyumbani kwao huku bwana mdogo huyu akipachika mabao 3 mguuni kwake.


RATIBA YA MECHI:
JUMAMOSI 13 Septemba 2008
[SAA 8 DAK 45 BONGO TIME]
LIVERPOOL v MAN U
[SAA 11 JIONI BONGO TIME]
BLACKBURN v ARSENAL
FULHAM v BOLTON
NEWCASTLE v HULL
PORTSMOUTH v MIDDLESBROUGH
WEST BROM v WEST HAM
WIGAN v SUNDERLAND
[SAA 1 NA NUSU USIKU BONGO TIME]
MAN CITY v CHELSEA
JUMAPILI 14 Septemba 2008
STOKE CITY v EVERTON
JUMATATU 15 Septemba 2008
TOTTENHAM v ASTON VILLA
MATOKEO MECHI ZA MCHUJO KUINGIA FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010:

-Uingereza yakata ngebe ya Croatia ya kutofungwa nyumbani, yaikung'uta 4-1!!

Huko Zagreb, Croatia, Uingereza ilifanya kile ambacho hakuna timu imewahi kufanya baada ya kuikung'uta Croatia 4-1 mbele ya mashabiki wake. Mabao 3 yalipachikwa na chipukizi wa Arsenal Theo Walcott na moja lilifungwa na Wayne Rooney.

MATOKEO MENGINE KWA NCHI ZA ULAYA NI:

Marcedonia 1 Holland 2, Finland 3 Germany 3, France 2 Serbia 1, Iceland 1 Scotland 2, Italy 2 Georgia 0, Latvia 0 Greece 2, Lithuania 2 Austria 0, Portugal 2 Denmark 3, Russia 2 Wales 1, Spain 4 Armenia 0, Sweden 2 Hungary 1, Turkey 1 Belgium 1.

HUKO MAREKANI YA KUSINI:

Brazil na Argentina zavutwa mashati!!

Brazil ikicheza nyumbani ililazimishwa sare ya 0-0 na Bolivia huku Argentina ikiwa ugenini ilikwenda sare ya 1-1 na Peru.

Wednesday, 10 September 2008

ZIDANE ATAMKA: 'RONALDO NI MCHEZAJI BORA DUNIANI!!!'
Aliewahi kuwa MCHEZAJI BORA DUNIANI MARA 3 Zinedine Zidane wa Ufaransa ametamka Cristiano Ronaldo ambae ni staa wa MABINGWA wa UINGEREZA na ULAYA Manchester United ndie pekee anaestahili kuwa MCHEZAJI BORA DUNIANI kwa mwaka 2007/8.
Kwa sasa kuna mjadala mkubwa kuhusu uteuzi wa Mchezaji Bora na unawalenga sana Wachezaji watatu ambao ni Messi, Kaka na Ronaldo.
Msimu uliopita Kaka ndie alieopoa tuzo hiyo.
Ronaldo ambae alifunga jumla ya magoli 42 msimu uliopita kwa sasa yuko nje ya uwanja baada ya kufanyiwa operesheni ya enka na anatarajiwa kurudi dimbani mwishoni mwa mwezi huu.
Ronaldo ndie aliepata tuzo ya MCHEZAJI BORA wa ULAYA pamoja na MFUNGAJI BORA wa ULAYA.
Vilevile amepata tuzo hizo hizo kwenye LIGI KUU UINGEREZA.

Zola -huenda leo akapewa Umeneja WEST HAM!

Baada ya kuondoka Meneja Alan Curbishley, West Ham leo inategemewa kumtangaza Mtaliana Gianfranco Zola kuwa Meneja mpya wa klabu hiyo.
Zola ambae alikuwa Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Italy na Chelsea kwa sasa ni Meneja wa Timu ya Taifa ya Italy ya Vijana wa chini ya miaka 21.
Zola ameahidi kuwa endapo atapata fursa hii basi atahakikisa West Ham inacheza aina moja tu ya soka!
Alisema: 'Mie najua kucheza mtindo mmoja tu! Kutuliza mpira chini kwenye kapeti na kushambulia!'
MCHUJO KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010
PARAGUAY YAZIDI KUPAA KUNDI LA MAREKANI KUSINI!
Paraguay 2 Venezuela 0!
Leo alfajiri Paraguay iliifunga Venezuela bao 2-0 na kuzidi kuongoza Kundi la nchi za Marekani Kusini zinazowania kuingia Fainali ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Timu ya pili kundi hilo ni Brazil inayocheza baadae leo na Bolivia.
MECHI NYINGINE ZINACHEZWA BAADAE LEO:
Uruguay v Ecuador

Chile v Colombia

Peru v Argentina

Brazil v Bolivia

Tuesday, 9 September 2008

PIGO KWA CHELSEA: MICHAEL ESSIEN NJE YA UWANJA MUDA MREFU!!
Mchezaji mahiri wa Chelsea raia wa Ghana Michael Essien aliumizwa vibaya siku ya Ijumaa wakati akichezea nchi yake ya Ghana ilipocheza na Libya huko Tripoli kugombea nafasi za kuingia Fainali ya Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010.
Klabu yake ya Chelsea imethibitisha Essien atafanyiwa operesheni wiki ijayo baada ya uvimbe kupungua kwenye goti lake aliloumia na baada ya hapo atakuwa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa.
Kukosekana kwa Michael Essien ni pigo kubwa kwa timu ya Luiz Felipe Scolari Meneja wa Chelsea hasa kipindi hiki kwani Jumamosi inacheza na Manchester City kwenye LIGI KUU na katikati ya wiki ijayo inapambana na Bordeaux ya Ufaransa kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE ikifuatiwa na mechi ya kukata na shoka ya pambano zidi ya MABINGWA wa LIGI KUU Manchester United tarehe 21 Septemba 2008.
FAINALI KOMBE LA DUNIA AFIKA KUSINI 2010

MECHI ZA MCHUJO NCHI ZA ULAYA
Jumatano 10 Septemba 2008
Uingereza kesho itashuka uwanjani mjini Zagreb, Croatia kupambana na timu ya Croatia iliyosababisha isicheze Fainali za EURO 2008 mwaka huu.
Uingereza na Croatia zilikuwa Kundi moja kwenye mashindano hayo na iliifunga Uingereza katika mechi zote mbili za Kundi hilo.
Mechi ya kwanza iliyochezwa nchini Croatia, Uingereza ililamba mabao 3-2 na katika mechi ya pili iliyochezwa Uwanja wa Wembley nyumbani kwa Uingereza, Croatia waliiadhiri vibaya Uingereza walipowashindilia mabao 2-0.
Mechi nyingine inayongojwa kwa hamu ni ya Ufarasa kwani Mabingwa hao wa Dunia wa zamani walitolewa nishai juzi katika mechi ya kwanza ya mchujo huu walipofungwa mabao 3-1 na Austria huko nchini Austria.
Ufaransa atakuwa nyumbani akicheza na Serbia.
MECHI:
Albania v Malta,
Andorra v Belarus,
Azerbaijan v Liechtenstein,
Bosnia-Herzegovina v Estonia,
Croatia v England,
Faroe Islands v Romania,
Finland v Germany,
France v Serbia,
FYR Macedonia v Holland,
Iceland v Scotland,
Italy v Georgia,
Kazakhstan v Ukraine,
Latvia v Greece,
Lithuania v Austria,
Moldova v Israel,
Montenegro v Rep of Ireland,
Northern Ireland v Czech Republic,
Portugal v Denmark,
Russia v Wales,
San Marino v Poland,
Slovenia v Slovakia,
Spain v Armenia,
Sweden v Hungary,
Switzerland v Luxembourg,
Turkey v Belgium,

Monday, 8 September 2008

Baada ya Kevin Keagan kutimka, Hughton apewa timu NEWCASTLE!!!
Chris Hughton ameteuliwa kuwa Meneja wa muda wa Newcastle kufuatia kutimka kwa Kevin Keagan aliegombana na Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu hiyo kuhusu kuuza Wachezaji bila kumhusisha.
Vilevile wasaidizi wengine wa Keagan, Terry McDermott na Adam Sadler wameamua kufuata nyayo za bosi wao Keagan na kuamua kuondoka klabuni..
Chris Hughton alikuwa Meneja Msaidizi wa Tottenham kabla ya kuhamia Newcastle msimu uliopita ambako pia alishika wadhifa huohuo.

Hughton atasaidiwa na waliokuwa wasimamizi wa Timu za Vijana hapo klabuni Richard Money na Alan Thompson.
Mechi ya kwanza chini ya usimamizi wa mteule Hughton itakuwa ni wikiendi hii ambako Newcastle watacheza na Hull City.
MCHUJO WA NCHI ZA MAREKANI KUSINI:
BRAZIL WAPAA HADI NAFASI YA PILI!

Leo alfajiri Brazil imepata ushindi mnono wa ugenini baada ya kuwafunga wenyeji wao Chile mabao 3-0 na hivyo kumpa ahueni Kocha wao ambae ni Nahodha wa zamani wa Brazil Dunga kutoka kwenye hatihati ya kumwaga unga katika mechi za mchujo kutafuta timu zitakazoingia Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Ingawa Ronaldinho alikosa penalti mabao mawili ya Luis Fabiano na moja la Robinho yaliwainua Brazil na kuwafanya wachupe toka nafasi ya sita hadi ya pili nyuma ya Paraguay ambao wako pointi mbili mbele.
Nafasi ya tatu inashikwa na Argentina na ya nne ni Uruguay.
Katika kundi hili timu nne za juu zinafuzu kuingia Fainali moja kwa moja na ya tano itacheza na timu kutoka kundi dogo la Marekani ya Kati kupata mshindi.
Jana Argentina wakiwa nyumbani walibanwa na Paraguay kwa kutoka suluhu ya bao 1-1 katika mechi ambayo wachezaji wawili wa Manchester United walikuwa vivutio-ingawa mmoja wa zamani-Gabriel Heinz alijifunga mwenyewe na Carlos Tevez alipata kadi nyekundu.
Pia jana hiyo hiyo Uruguay alimfunga Colombia 1-0 nyumbani kwake.
Mechi za Kundi hili zitaendelea kesho kwa mechi kati ya Paraguay na Venezuela.
Kesho kutwa ni mechi hizi:
Uruguay v Ecuador
Chile v Colombia
Peru v Argentina
Brazil v Bolivia

MAN U WAPUUZA KAULI YA MFANYABIASHARA WA ABU DHABI YA KUMNUNUA RONALDO.
-Mmiliki mpya wa MAN CITY adai atamnunua Ronaldo kwa kitita cha Pauni Milioni 135 ifikapo Januari!!!

-Wengine kwenye listi yake ni Torres na Fabregas!!!
Mkurugenzi Mtendaji wa Manchester United David Gill amepuuza kauli ya Sulaiman Al-Fahim ambae hivi majuzi ameinunua Klabu ya Manchester City ambao ni watani wa jadi wa Man U kwamba watatoa ofa ya Pauni Milioni 135 kumchukua Cristiano Ronaldo kwenda Man City.
Mfanyabiashara huyo wa Abu Dhabi, Falme za Nchi za Kiarabu ambae ni mmoja wa ukoo wa Kifalme huko Abu Dhabi alitoa kauli hiyo mara tu baada ya kuinunua Man City kutoka kwa aliekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Thaksin Shinawatra ambae ameikimbia nchi yake baada ya yeye na mkewe kukabiliwa na mashitaka mazito ya rushwa.
Mbali ya kutoa ofa hiyo kwa Ronaldo, Sheikh huyo wa Abu Dhabi amekaririwa akisema pia atawanunua Fernando Torres wa Liverpool na Cesc Fabregas hiyo Januari wakati kipindi cha usajili wachezaji kitakapofunguliwa tena.
‘Ni kitu cha kushangaza kwani hivi karibuni Tottenham wametushitaki sisi kwa Uongozi wa LIGI KUU kwa sababu Ferguson alikaririwa akisema tunataka kumnunua Berbatov….,’David Gill alitamka.'…sasa huyu bwana ametamka listi ya wachezaji atakaowanunua..........!!!’

Sunday, 7 September 2008

MATOKEO YA BAADHI YA MECHI ZA JANA ZA KUWANIA KUINGIA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA HUKO AFRIKA KUSINI 2010:
Albania 0 Swden 0
Andorra 0 Uingereza 2
Armenia 0 Uturuki 2
Austria 3 France 1
Belgium 3 Estonia 2
Croatia 3 Kazakhstan 0
Cyprus 1 Italy 2
Hungary 0 Denmark 0
Liechtenstein 0 Germany 6
Luxemborg 0 Greece 3
Malta 0 Ureno 4
Spain 1 Bosnia-Herzegovina 0
Mauritius 1 Tanzania 4
Powered By Blogger