Monday 8 September 2008

MAN U WAPUUZA KAULI YA MFANYABIASHARA WA ABU DHABI YA KUMNUNUA RONALDO.
-Mmiliki mpya wa MAN CITY adai atamnunua Ronaldo kwa kitita cha Pauni Milioni 135 ifikapo Januari!!!

-Wengine kwenye listi yake ni Torres na Fabregas!!!
Mkurugenzi Mtendaji wa Manchester United David Gill amepuuza kauli ya Sulaiman Al-Fahim ambae hivi majuzi ameinunua Klabu ya Manchester City ambao ni watani wa jadi wa Man U kwamba watatoa ofa ya Pauni Milioni 135 kumchukua Cristiano Ronaldo kwenda Man City.
Mfanyabiashara huyo wa Abu Dhabi, Falme za Nchi za Kiarabu ambae ni mmoja wa ukoo wa Kifalme huko Abu Dhabi alitoa kauli hiyo mara tu baada ya kuinunua Man City kutoka kwa aliekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Thaksin Shinawatra ambae ameikimbia nchi yake baada ya yeye na mkewe kukabiliwa na mashitaka mazito ya rushwa.
Mbali ya kutoa ofa hiyo kwa Ronaldo, Sheikh huyo wa Abu Dhabi amekaririwa akisema pia atawanunua Fernando Torres wa Liverpool na Cesc Fabregas hiyo Januari wakati kipindi cha usajili wachezaji kitakapofunguliwa tena.
‘Ni kitu cha kushangaza kwani hivi karibuni Tottenham wametushitaki sisi kwa Uongozi wa LIGI KUU kwa sababu Ferguson alikaririwa akisema tunataka kumnunua Berbatov….,’David Gill alitamka.'…sasa huyu bwana ametamka listi ya wachezaji atakaowanunua..........!!!’

No comments:

Powered By Blogger