Friday 12 September 2008

WAKATI WEST HAM WAMKARIBISHA MENEJA MPYA ZOLA, MDHAMINI WAO AWA MUFILISI!!

Wakati Klabu ya West Ham inatangaza rasmi kuwa Mtaliana Gianfranco Zola ndie Meneja mpya kuchukua nafasi ya Alan Curbishley alietimka kufuatia mfarakano na uongozi wa juu kuhusu uuzaji Wachezaji, Mfadhili mkuu wa Klabu hiyo XL Holidays ambayo kiukubwa ni ya tatu katika nyanja ya usafirishaji Watalii huko Uingereza imetangazwa kufilisika.
Jezi za West Ham zilikuwa na maandishi XL kifuani na Jumamosi kwenye mechi yao na West Bromwich watacheza wakivaa jezi zisizokuwa na maandishi hayo kifuani.


West Ham walikuwa na mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya XL Holidays wenye thamani ya Pauni Milioni 7 na nusu.
Klabu hiyo ililipwa Pauni Milioni 2 na nusu Februari, 2007 na baada ya hapo haikulipwa chochote na kuna madai mmiliki wa West Ham vilevile ni muhusika wa Kampuni hiyo mufilisi ya XL Holidays.

No comments:

Powered By Blogger