Saturday 13 September 2008

FERGUSON ASIKITISHWA NA MCHEZO HAFIFU WA MAN U!
-ASEMA: 'Tulishindwa kuhimili mikikimikiki, nguvu na rafu zao!!'
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesikitishwa na kiwango cha timu yake kwenye mechi waliyofungwa na Liverpool kwa mabao 2-1 nyumbani kwa Liverpool Uwanja wa Anfield.
Ferguson alisema mbali ya pengine Rio Ferdinand hakuna hata mchezaji mmoja aliecheza kwa kiwango na hilo lilimsikitisha sana.
Vilevile alisikitishwa na jinsi timu yake ilivyokuwa inajihami na kulaumu kuwa makosa ya ulinzi mbovu ndio yalisababisha magoli yote mawili.
Ferguson alitamka: 'Hutegemei hayo yote kwa timu kama Manchester United! Ilikuwa siku mbaya lakini hata tukiwa na siku mbaya huwa hatutoki mikono mitupu! Kiini cha kufungwa ni sisi kushindwa kukabiliana na mikiki, nguvu na rafu zao! Lazima uwape hongera kwa hilo lakini tulitakiwa tuhimili na kudhibiti hayo!
Bosi huyo wa Mabingwa Man U pia hakufurahishwa na Vidic kupewa kadi mbili za njano ambazo zilimaanisha kadi nyekundu kwa kudai Refa alishindwa kumpa hata kadi moja Carragher wa Liverpool aliekuwa akifanya faulo kama hizo mechi nzima.

No comments:

Powered By Blogger