Tuesday 9 September 2008

PIGO KWA CHELSEA: MICHAEL ESSIEN NJE YA UWANJA MUDA MREFU!!
Mchezaji mahiri wa Chelsea raia wa Ghana Michael Essien aliumizwa vibaya siku ya Ijumaa wakati akichezea nchi yake ya Ghana ilipocheza na Libya huko Tripoli kugombea nafasi za kuingia Fainali ya Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010.
Klabu yake ya Chelsea imethibitisha Essien atafanyiwa operesheni wiki ijayo baada ya uvimbe kupungua kwenye goti lake aliloumia na baada ya hapo atakuwa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa.
Kukosekana kwa Michael Essien ni pigo kubwa kwa timu ya Luiz Felipe Scolari Meneja wa Chelsea hasa kipindi hiki kwani Jumamosi inacheza na Manchester City kwenye LIGI KUU na katikati ya wiki ijayo inapambana na Bordeaux ya Ufaransa kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE ikifuatiwa na mechi ya kukata na shoka ya pambano zidi ya MABINGWA wa LIGI KUU Manchester United tarehe 21 Septemba 2008.

No comments:

Powered By Blogger