Friday, 12 September 2008

WENGER AWASHTUMU WAMILIKI WAPYA WA MAN CITY: 'Lazima waheshimu taratibu! Soka sio supamaketi!!'
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameibuka na kuwaponda Wamiliki wapya wa Manchester City, Kampuni ya Abu Dhabi, Falme za Nchi za Kiarabu, iitwayo ABU DHABI UNITED GROUP, ambayo inasemekana ni mali ya Familia ya Kifalme huko Abu Dhabi, kwa majigambo yao kwamba ifikapo Januari watawanunua Cristiano Ronaldo, Cesc Fabregas, Fernando Torres nk, na kuifanya klabu hiyo kuwa kubwa kupita zote duniani.
Wenger alifoka: 'Kuna sheria! Lazima ziheshimike!'
'Huwezi kuibuka na kudai ntamlipa Ronaldo Pauni 250,000 kwa wiki na ntamnunua kwa Pauni Milioni 135 wakati ana mkataba na Man U!'
Wenger aliongeza kubwata:'Soka sio supamaketi!'
Wakati huohuo kuna taarifa kwamba aliekaririwa akitoa kauli hizo za kununua Wachezaji nyota mara baada ya kutangazwa kuinunua Man City ambae ni kiongozi mwandamizi wa Kampuni hiyo ya Abu Dhabi, Dr Sulaiman Al Fahim, amewekwa pembeni na tajiri na mmiliki hasa wa kampuni hiyo, SHEIKH Mansour bin Zahed Al Nahyan ambae ni mtoto wa muasisi wa nchi ya Falme za Nchi za Kiarabu na anaesifika sana kama mpenzi wa kweli wa soka na mtu asiependa makuu na sifa za kipuuzi.

No comments:

Powered By Blogger