Saturday, 2 May 2009

LEO NI 'EL CLASICO': Real Madrid v Barcelona!!!

Kwa wapenzi wa La Liga, yaani Ligi ya Spain, leo kivumbi kitatimka ndani ya Uwanja wa Santiago Bernabue, nyumbani kwa Real Madrid watakapo wakaribisha watani zao Barcelona.
Kukiwa kumebaki mechi 5 ligi kumalizika, Barcelona wanaongoza kwa pointi 4 huku Real Madrid wakiwanyemelea.
Barcelona wamekuwa wakiongoza ligi hiyo karibu msimu mzima na katika mechi 33 wamefunga mabao 94 lakini Real Madrid tangu wafungwe na Barcelona 2-0 Desemba huko Nou Camp uwanjani kwa Barcelona hawajapoteza mechi yeyote.
Mechi hii itaanza saa 3 usiku saa za bongo.

Wenger aunga mkono Almunia kudakia England

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameunga mkono hatua ya ya Kipa wa Arsenal Manuel Almunia kuchezea England endapo atachukua uraia. Almunia ni raia wa Spain lakini hajawahi kudakia nchi hiyo na kwa sababu ameshakaa England tangu 2004 akiomba uraia wa England atapewa.
Mwenyewe Almunia, mwenye umri wa miaka 31, anasema: 'Spain hawajaniita. Sasa ikiwa England wanaona nafaa itabidi nifikirie.'
Kwa sasa Kipa nambari wani wa England ni David James, mwnye miaka 38, na anakaribia kustaafu na wanaogombea nafasi hiyo ni Paul Robinson, Chris Kirkland, Robert Green na Ben Foster.
Ferguson akerwa mechi kuchezwa mapema!!
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amekerwa na mechi yao ya leo ya LIGI KUU England na Middlesbrough kuchezwa saa 8 dakika 45 mchana, saa za bongo, wakati huko England ni saa 6 dakika 45 mchana wakati Jumatano walicheza mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huko Old Trafford na Arsenal.
Ferguson amesema: 'Ni sababu ya TV lakini ni mechi muhimu kwetu ingawa nitapumzisha baadhi ya Wachezaji.'
Kwa sasa wako pointi 3 mbele ya Liverpool ingawa wana mechi moja mkononi. Liverpool anacheza kesho na Newcastle.

Friday, 1 May 2009

NUSU FAINALI UEFA CUP:

Werder Bremen 0 Hamburg 1

Kwenye mechi ya Klabu za Kijerumani, Hamburg wameweza kuibuka na ushindi mzuri wa ugenini baada ya kuwapiga wenzao Werder Bremen 1-0 kwa bao alilofunga Piotr Trochowski.
Timu hizi zitarudiana Alhamisi ijayo.

Dynamo Kiev 1 Shakhtar Donetsky 1

Mechi hii imehusisha Timu za Ukraine na ngoma ni dro ingawa Shakhtar Donestsky watakuwa wanachekelea kwani wamepata kigoli cha ugenini kwenye suluhu ya 1-1 na timu hizi zinarudiana Alhamisi ijayo.
LIGI ITALIA KUVUNJIKA: Inaanzishwa 'LEGA CALCIO SERIE A'
Baada ya kuona mafanikio makubwa ya England wakati ilipoanziashwa LIGI KUU England, Italia wanataka kuiga nini kilichotokea huko kwa kuanzisha LIGI PEKEE ambayo itakuwa tofauti na Ligi nyingine ya Klabu zilizo Madaraja ya chini. Ligi hiyo itaitwa LEGA CALCIO SERIE A.
Klabu 19 za SERIE A zimesaini mkataba wa makubaliano kuanzisha Ligi hiyo mpya na Klabu pekee iliyogoma kusaini ni Lecce ambayo inachungulia kaburi la kushushwa Daraja.
Huko England, LIGI KUU ilizaliwa mwaka 1992 baada ya Klabu zilizokuwa kile kilichokuwa kinaitwa Daraja la Kwanza kujitenga na kuamua kuchukua madaraka yote ya kusimamia haki za kibiashara kwenye mechi zao wao wenyewe.
Waliamua, haki za Matangazo ya TV, Biashara na kila kitu kitaendeshwa na wao kama LIGI KUU England [yaani English Premier League] na kuwaachia mamlaka ya uendeshaji wa Sheria chini ya FIFA yaendelee kwenye mamlaka ya FA, Chama cha Soka England, na Football League wasimamie Madaraja ya Chini.
Tangu wakati huo Dunia imeshuhudia mafanikio makubwa kwa Timu za England na zimekuwa zikitawala Ulaya na sasa Duniani huku Manchester United wakitamba kuwa ndio Mabingwa wa Dunia.
Katika miaka miwili iliyopita England imeingiza Timu 3 kwenye Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na pia kwa miaka minne mfululizo Timu moja toka England imeingia Fainali.
Sasa Italia wanataka kuiga mafanikio hayo, ambayo Rais wa Klabu ya Palermo anaelezea: 'Tumeanzisha Ligi mpya ya Serie A. Hatuna furaha lakini huu ndio ukweli na hili litatendeka.'

Thursday, 30 April 2009

LEO NI NUSU FAINALI UEFA CUP-Klabu za Ujerumani zinamenyana zenyewe na za Ukraine wanapambana wenyewe!!!
Leo usiku mechi za Nusu Fainali za Kombe la UEFA zitachezwa na ni vita kati ya Timu za Nchi ya Ukraine zinazopambana zenyewe kwenye Nusu Fainali ya kwanza na Nusu Fainali nyingine ni Timu za Nchi za Ujerumani.
Dynamo Kiev inacheza na Shakhtar Donetsk zote zikiwa zinatoka Ukraine na mechi nyingine ni Timu za Ujerumani Werder Bremen inayokwaana na Hamburg.
Marudiano ya mechi hizi ni wiki ijayo.
Washindi watakutana Fainali Mei 20.
RATIBA LIGI KUU ENGLAND: [saa ni za bongo]
Jumamosi, 2 Mei 2009
[saa 8 dak 45 mchana]
Middlesbrough v Man U
[saa 11 jioni]
Chelsea v Fulham
Man City v Blackburn
Portsmouth v Arsenal
Stoke v West Ham
Tottenham v West Brom
Wigan v Bolton
Jumapili, 3 Mei 2009
[saa 9 na nusu mchana]
Liverpool v Newcastle
[saa 12 jioni]
Sunderland v Everton
Jumatatu, 4 Mei 2009
[saa 4 usiku]
Aston Villa v Hull

Ferguson aionya Arsenal: 'Ni ngumu Arsenal kutuzuia kufunga goli Emirates!!!

Baada ya ushindi kiduchu wa bao 1-0 uwanjani kwake Old Trafford kwa bao lililopachikwa na Beki John O'Shea na huku wakikosa lundo la magoli, Mabingwa Watetezi Manchester United watatua Emirates Stadium Jumanne ijayo kurudiana na Arsenal na Meneja wa Mabingwa hao, Sir Alex Ferguson, ametamka itakuwa ngumu sana kwa Arsenal kuisimamisha kupata hata bao moja. Ili kuingia Fainali Arsenal inabidi aifunge Man U bao 2-0 na endapo Man U atapata bao moja basi inabidi Arsenal afunge bao 3.
Ferguson amesema: 'Najua tuna uwezo wa kwenda kwao Emirates na kufunga na hilo ndio tatizo kubwa kwa Arsenal!'
Nae Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amejitetea kwa kusema: 'Nna uhakika kwenye marudiano utaiona Arsenal nyingine! Pengine Man U watajuta kwa nini hawakufunga bao la pili!! Lakini pongezi kubwa ziende kwa Kipa Almunia alieokoa magoli mengi!!'
Man U 1 Arsenal o

John O'Shea ameifungia Mabingwa Watetezi wa Ulaya, Manchester United, bao moja dhidi ya Arsenal uwanja wa nyumbani Old Trafford na kuwapa ushindi wa bao 1-0 katika mechi waliyoitawala kabisa na kukosa lundo la magoli huku Kipa wa Arsenal, Manuel Almunia, akiibuka shujaa kwa kuokoa mabao hayo.

Timu hizi zitarudiana Jumanne ijayo Emirates Stadium.

Man Utd: Van der Sar, O'Shea, Ferdinand (Evans 87), Vidic, Evra, Fletcher, Carrick, Anderson (Giggs 66), Ronaldo, Tevez (Berbatov 66), Rooney.Akiba hawakucheza: Foster, Park, Scholes, Rafael Da Silva.
Kadi: Tevez.
Arsenal: Almunia, Sagna, Toure, Silvestre, Gibbs, Song, Diaby, Walcott (Bendtner 70), Fabregas, Nasri, Adebayor (Eduardo 82).Akiba hawakucheza: Fabianski, Denilson, Ramsey, Djourou, Eboue.
Watazamaji: 74,733
Refa: Claus Bo Larsen (Denmark).

Wednesday, 29 April 2009

NDANI YA NOU CAMP: Barcelona 0 Chelsea 0
Barcelona wakiwa kwao Nou Camp huku kila mtu akitegemea Messi, Eto’o au Henry atafunga wameambua patupu baada ya Chelsea kufunga milango yote.
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Marquez (Puyol 52), Pique, Abidal, Xavi, Toure Yaya, Iniesta, Messi, Eto'o (Bojan 82), Henry (Hleb 87).Akiba hawakucheza: Jorquera, Gudjohnsen, Keita, Sylvinho.
Kadi: Toure Yaya, Puyol.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Alex, Terry, Bosingwa, Mikel, Ballack (Anelka 90), Essien, Lampard (Belletti 71), Malouda, Drogba.Akuba hawakucheza: Hilario, Di Santo, Kalou, Mancienne, Stoch.
Kadi: Alex, Ballack.
Watazamaji: 95,000.
Refa: Wolfgang Stark (Germany).
REFA WEBB akiri kosa!!
Refa Howard Webb aliechezesha mechi ya Manchester United na Tottenham uwanjani Old Trafford na Man U kuibuka washindi 5-2 wakati walikuwa nyuma 2-0 hadi hafutaimu amekubali alikosea kuipa Man U penalti kipindi cha pili na ambayo Ronaldo aliifungia timu yake bao la kwanza.
Webb amesema: ‘Nimeangalia tena na nadhani ni kosa lakini sisi huwa tunatoa uamuzi wa haki pale pale. Sisi tuko uwanjani na nilimwona Mchezaji wa Manchester akiucheza mpira na kuangushwa lakini sikuona Kipa akiugusa mpira ule. Inasikitisha lakini nionyeshe mtu asiefanya makosa na mimi ntakuonyesha mtu asiefanya chochote!’
Penalti hiyo imezua mzozo mkubwa hadi Kiungo wa Tottenham Jermaine Jenas ametakiwa na FA ajieleze ndani ya siku 7 kwa kauli yake ya kumkashifu Refa.
Lakini wadau wengi wanajiuliza hata kama Refa alikosea na 'KUIBEBA' Man U kupata bao la kwanza walikuwa wapi mabao mengine 'HALALI' 'MANNE; kuingia?
Hakika mfa maji haishi kutapatapa!!!!!

Tuesday, 28 April 2009

NUSU FAINALI UBINGWA WA ULAYA: ULAYA MOTO KUWAKA!!! Barcelona v Chelsea leo, kesho Man U v Arsenal!!

UEFA CHAMPIONS LEAGUE leo inaingia hatua ya Nusu Fainali huku England ikitawala Ulaya kwa kuwa na Timu 3 kati ya 4 zilizo Nusu Fainali na leo Barcelona, ndani ya nyumba yao Nou Camp, wanawakaribisha Chelsea. Kesho, ndani ya Old Trafford nyumbani kwa Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo, Manchester United, Arsenal atakuwa mgeni wa Bingwa huyo.
Marudiano ya Nusu Fainali hizi ni wiki ijayo wakati Jumanne ijayo Arsenal atakuwa mwenyeji wa Man U na Chelsea atamkaribisha Barcelona ndani ya Stamford Bridge.
Washindi wa Nusu Fainali hizi watapambana kwenye Fainali mjini Rome, Italia mnamo tarehe 27 Mei 2009.
Ndani ya Nou Camp, ngome thabiti ya Barcelona inayoongozwa na Meneja wao Pep Guardiola aliekuwa Mchezaji wa zamani wa Barcelona, Chelsea watakuwa na kazi ngumu sana ya kusimamisha Washambuliaji hatari wa Barcelona kina Lionel Messi, Samuel Eto'o na Thierry Henry wanaolishwa na viungo Andres Iniesta na Xavi.
Kazi ya Chelsea itakuwa ngumu kweli hasa kwani itawakosa Mabeki wao wawilli wa kutumainiwa ambao ni Ricardo Carvalho, alie majeruhi, na Ashley Cole, mwenye Kadi. Nafasi zao zinategemewa kuchukuliwa na Alex na Jose Bosingwa ambae itabidi achezeshwe kama Beki wa kushoto kuziba pengo la Ashley Cole.
Pep Guardiola, Meneja wa Barcelona, anakiri Chelsea wana mibavu kupita wao kwa kusema: 'Niliwaona wakiwatoa Liverpool Robo Fainali. Ni wazuri na wana nguvu sana kupita sisi hivyo ni muhimu sana kwetu kumiliki na kudhibiti mpira na kushinda Nou Camp.'
Guus Hiddink, Meneja wa Chelsea, anasema: 'Messi ni hatari. Lakini ukitaka kumkaba Messi peke yake ni kosa kwani wapo Eto'o na Henry ambao ni hatari kubwa pia!'
NEWCASTLE NA BALAA LA KUSHUKA DARAJA!! SHEARER: 'MUDA UNAYOYOMA!!!'
Newcastle 0 Portsmouth 0
Shujaa wa zamani wa Newcastle kama Mchezaji, Alan Shearer, alieletwa tena Newcastle kama Meneja ili kuinusuru timu toka balaa la kushuka Daraja, jana baada ya suluhu ya 0-0 na Portsmouth nyumbani St James Park, amekiri muda unayoyoma kwa Newcastle kujikwamua na sasa wamebakiwa na mechi 4 tu huku wakiwa wamekwama kwenye eneo la timu 3 zitakazoshushwa daraja.
Timu za Newcastle [nafasi ya 18 pointi 31], Middlesbrough [nafasi ya 19 pointi 31] na West Bromwich [nafasi ya 20 (na ya mwisho) pointi 28] ndizo zipo kwenye nafasi ya Timu 3 zinazoshushwa.
Juu yao, zipo Hull City, nafasi ya 17 pointi 34, Sunderland, nafasi ya 16 pointi 35 na Blackburn, nafasi ya 15, pointi 37.
Mechi inayofuata kwa Newcastle ni safari ya kwenda Anfield nyumbani kwa Liverpool wikiendi hii.
Jermaine Jenas atakiwa atoe maelezo na FA kuhusu madai Refa kawabeba Man U!!!
Baada ya kipigo cha mabao 5-2 na Manchester United, Kiungo wa Tottenham Hotspurs, Jermaine Jenas, ametakiwa atoe maelezo na FA, Chama cha Soka England, ndani ya siku 7 juu ya kauli yake kwamba Refa wa mechi hiyo, Howard Webb, alizidiwa na presha ya kuchezesha mechi Old Trafford nyumbani kwa Man U.
Jenas alikaririwa akisema: 'Refa hata hakufikiria na hata hakusita kutoa penalti!!! Ilikuwa kama vile kisha amua kikianza kipindi cha pili basi atatoa kitu!!'
Katika mechi hiyo, Tottenham walikuwa mbele kwa mabao 2-0 hadi mapumziko lakini kipindi cha pili Man U wakaibuka na kuwanyuka mabao matano na hivyo kushinda 5-2.
Jenas alikuwa akizungumzia bao la kwanza ambalo Refa Howard Webb alitoa penalti baada ya Michael Carrick wa Man U kuangushwa na Kipa Gomes wa Tottenham.

Monday, 27 April 2009

KWA UFUPI:::::::::::::::::

LEO FAINALI YA ALAN SHEARER!!


Newcastle United, ikiwa chini ya Nyota wa zamani Alan Shearer kama Meneja wao, leo usiku wanajitupa uwanjani kwao St James Park kupambana na Portsmouth katika vita yao ya kujinusuru wasishuke Daraja. Newcastle wako nafasi ya 19 kwenye msimamo wa LIGI KUU England ikiwa ni nafasi moja tu toka mkiani na wana pointi 30. Juu yao, kwenye nafasi ya 18, wako Middlesbrough wenye pointi 31 na nafasi ya 17 wako Hull City wenye pointi 34. Nafasi ya 20 na ya mwisho inashikiliwa na West Bromwich wenye pointi 28.
Timu tatu za mwisho, yaani zitazomaliza ligi zikiwa nafasi ya 18, 19 na 20 kwenye ligi , hushushwa Daraja.
Portsmouth wako nafasi ya 14 wakiwa na pointi 37 na ingawa wako afueni kidogo lakini bado hawajasalimika kwani kuna mechi 4 au 5 kwa baadhi ya Timu kumaliza ligi.
Rafael aongeza mkataba Old Trafford hadi 2013!!!!

Chipukizi kutoka Brazil, Rafael da Silva, ameongeza mkataba wake na Manchester United hadi Juni 2013.
Rafael yuko Man U pamoja na pacha mwenzake Fabio, wote wakiwa na miaka 18 tu lakini Rafael ndie alieichukua Manchester United kwa kishindo kwani tangu aanze kuchezea Timu ya kwanza Agosti mwaka jana katika mechi na Newcastle amekuwa na mafanikio makubwa na mpaka sasa ameshacheza mechi 24.
Rafael, anaecheza kama beki wa pembeni kulia, ana nafasi kubwa ya kujenga zaidi jina lake hasa kutokana na kuumia kwa Mabeki wanaomudu nafasi hiyo Nahodha Gary Neville na Wes Brown.
Mtoto wa Sir Alex Ferguson aipandisha timu yake Daraja!!!
Darren Ferguson, mtoto wa Sir Alex Ferguson wa Manchester United, ambae ni Meneja wa Timu ya Peterborough iliyokuwa ikicheza Ligi iitwayo LEAGUE 1 ambalo ni Daraja chini ya COCA COLA CHAMPIONSHIP, Daraja ambalo liko chini ya LIGI KUU England, ameweza kuipandisha Timu hiyo na sasa inaungana na Bingwa wa Ligi hiyo Leicester City kuingia COCA COLA CHAMPIONSHIP msimu ujao.
Peterborough imeshika nafasi ya pili kwenye LEAGUE 1 baada ya kuifunga Colchester bao 1-0.
Klinsman atimuliwa Umeneja Bayern Munich
Staa wa zamani wa Ujerumani, Jurgen Klinsman ambae alikuwa Meneja wa Klabu kongwe ya Bundesliga huko Ujerumani, Bayern Munich, amefukuzwa kazi miezi minane tu tangu ateuliwa baada ya matokeo mabaya ya Timu hiyo.
Juzi, kwenye mechi ya Bundesliga, Bayern Munich ilichapwa bao 1-0 na Schalke matokeo yaliyoifanya Bayern iwe nafasi ya 3 kwenye Ligi na hivyo kuwa hatarini kukosa UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao.
Majuzi tu, kwenye Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Bayern ilibamizwa mabao 5-1 na Barcelona na kutupwa nje ya mashindano hayo.

Giggs anyakua Tuzo ya Mchezaji Bora wa PFA!!!!!

Kiungo Ryan Giggs wa Manchester United ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa PFA [-Professional Footballers Association-Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa-] na hii ikiwa ni mara yake ya kwanza kuitwaa Tuzo hiyo ingawa ashawahi kushinda Tuzo hiyo wanayopewa Wachezaji Vijana mara mbili. Giggs, mwenye umri wa miaka 35, aliwabwaga wenzake wa Man U Nemanja Vidic, Rio Ferdinand, Cristiano Ronaldo, Edwin van der Sar na Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard kwa kushinda Tuzo hiyo.
Giggs, akiwa na Manchester United tangu aanze kuichezea mwaka 1991 akiwa na miaka 17, ameshashinda LIGI KUU mara 10, FA CUP mara 4, League Cup [siku hizi huitwa Carling Cup] mara 3 na UEFA CHAMPIONS LEAGUE mara 2.
Mchezaji Chipukizi wa Aston Villa, Asley Young, ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Vijana. Young amewabwaga kina Jonny Evans na Rafael Da Silva wa Man U, Aaron Lennon wa Spurs na Kiungo wa Manchester City Stephen Ireland.
Giggs, akitoa shukrani, alitamka: 'Ni tuzo kubwa sana!! Ni heshima kuipata kwani wanaochagua ni Wachezaji wenzangu!! Namshukuru sana Meneja wangu Sir Alex Ferguson!!! Yeye ni mtu muhimu sana maishani mwangu!! Nilikutana nae mara ya kwanza nikiwa na miaka 13 tu na kwa zaidi ya miaka 20 sasa, amenilea vizuri!!!'
Mbali ya kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora, Giggs pia ametajwa mmoja wa Kikosi cha Timu Bora ya Msimu ambayo ina jumla ya Wachezaji 6 kutoka Mabingwa Manchester United.
Tuzo hii pamoja na Kikosi cha Timu Bora huchaguliwa na kupigiwa kura na Wachezaji wote wa
Kulipwa wanaochezea LIGI KUU England.
Kikosi kamili cha Timu Bora ni:
Edwin Van der Sar (Manchester United), Glen Johnson (Portsmouth), Rio Ferdinand (Manchester United), Nemanja Vidic (Manchester United), Patrice Evra (Manchester United), Ashley Young (Aston Villa), Steven Gerrard (Liverpool), Ryan Giggs (Manchester United), Cristiano Ronaldo (Manchester United), Nicolas Anelka (Chelsea), Fernando Torres (Liverpool)

Sunday, 26 April 2009

Arsenal 2 Middlesbrough 0

Wakati Arsenal, kwa ushindi wa leo, wanazidi kujichimbia kwenye nafasi ya 4 ya msimamo wa ligi na hivyo kupata nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao, Middlesbrough wamezidi kuganda nafasi ya tatu toka chini na hivyo wako kwenye hatari kubwa kuporomoka daraja huku wakiwa wamesaliwa na mechi 4 tu.
Nahodha Fabregas ndie alifunga bao zote mbili za Arsenal na kuwafanya wafikishe pointi 65 wakiwa nafasi ya nne huku Chelsea wakiwa mbele yao wakiwa na pointi 71.
Middlesbrough wako nafasi ya 18, ikiwa ni ya tatu toka chini, na wana pointi 31 huku juu yao wapo Hull City pointi 34. Chini ya Middlesbrough wako Newcastle United pointi 30 na wa mwisho ni West Bromwich pointi 28.
Timu tatu za mwisho ndio huporomoshwa daraja
Arsenal: Almunia, Eboue, Toure, Silvestre, Gibbs, Walcott, Denilson, Fabregas, Nasri, Arshavin, Bendtner.
Akiba: Fabianski, Diaby, Sagna, Vela, Song Billong, Djourou, Adebayor. Middlesbrough: Jones, McMahon, Wheater, Huth, Taylor, O'Neil, Bates, Sanli, Downing, Aliadiere, King.
Akiba: Turnbull, Hoyte, Digard, Emnes, Alves, Adam Johnson, Grounds.
Refa: Chris Foy

Blackburn 2 Wigan 0

Jana, Benni McCarthy na Nahodha Nielsen waliifungia mabao Blackburn na kuifanya ijiwekee kizingiti cha pointi 6 na zile timu zilizo kwenye balaa la kushuka daraja.
Blackburn: Robinson, Ooijer, Nelsen, Givet, Warnock, Diouf, Grella, Kerimoglu, Pedersen, Samba, McCarthy.
Akiba: Bunn, Dunn, Khizanishvili, Andrews, Villanueva, Olsson, Doran.
Wigan: Kirkland, Boyce, Scharner, Bramble, Figueroa, Valencia, Watson, Cattermole, N'Zogbia, Mido, Rodallega.
Akiba: Pollitt, Edman, Koumas, De Ridder, Kapo, Zaki, Brown.
Refa: Peter Walton

Man U waibomoa Tottenham 5-2!!! Tottenham waliongoza 2-0 hadi mapumziko!!!

Wengi wanakumbuka mechi ya LIGI KUU England iliyochezwa White Hart Lane Septemba 2001 na Tottenham wakawa wanaongoza kwa bao 3-0 hadi mapumziko lakini Manchester United wakarudi kipindi cha pili na kushinda 5-3!!!

Jana mambo yalikuwa hivyo hivyo kwani hadi mapumziko, Man U 0 Tottenham 2!!

Bila shaka matokeo hayo yangebaki hivyo, Liverpool wangeshangilia kwani katika mechi waliyocheza jana lakini mapema kidogo, Liverpool waliifunga Hull City mabao 3-1 na kufikisha pointi 74 sawa na Man U lakini wakawa wanaongoza ligi kwa ubora wao wa magoli.

Hata hivyo, Mabingwa Man U waliibuka kipindi cha pili na kuibadili stori yote.

Carrick aliangushwa na Kipa Gomes kwenye boksi na Ronaldo akafunga penalti kuandika bao la kwanza dakika ya 57.

Dakika kumi baadae Rooney akasawazisha na dakika moja baadae Ronaldo akafunga bao tamu kwa kichwa na kuwafanya Man U waongoze kwa bao 3-2. Dakika tatu baadae Rooney akafunga la nne na Berbatov akachomeka la tano.

Mabingwa Man U sasa wako tena kileleni wakiwa na pointi 77 kwa mechi 33, Liverpool anafuata pointi 74 mechi 34 kisha Chelsea pointi 71 mechi 34 na Arsenal ni wa nne pointi 62 mechi 33.

Baada ya mechi Sir Alex Ferguson akizungumzia penalti:
"Ni bahati. Soka ni mchezo wa ajabu. Wiki iliyokwisha tulinyimwa penalti ya dhahiri na ikatung'oa kwenye Nusu Fainali ya FA CUP!! Lakini, kipindi cha pili cha mechi hii tulicheza vizuri sana!!!!"

Meneja waTottenham Harry Redknapp:
"Mechi iligeuka baada ya penalti! Kabla nilidhani hatufungwi. Ile penalti ni zawadi!! Ni kosa kubwa!! Howard Webb wanasema ndie Refa bora hapa sasa sijui huyo Refa mbovu yuko vipi!!"
Man Utd: Van der Sar, Rafael Da Silva (O'Shea 70), Ferdinand, Vidic, Evra, Ronaldo, Carrick, Fletcher (Scholes 61), Nani (Tevez 46), Berbatov, Rooney.
Akiba hawakucheza: Foster, Anderson, Evans, Macheda.
Kadi: Tevez, Scholes, Ronaldo.
Magoli: Ronaldo 57 pen, Rooney 67, Ronaldo 68, Rooney 71, Berbatov 79.
Tottenham: Gomes, Corluka, Woodgate, King, Assou-Ekotto, Lennon, Palacios, Jenas, Modric (Bale 86), Keane (Huddlestone 87), Bent.
Akiba hawakucheza: Cudicini, Hutton, Zokora, Bentley, Chimbonda.
Kadi: Woodgate, Jenas, Gomes.
Magoli: Bent 29, Modric 32.
Watazamaji: 75,458
Refa: Howard Webb
Hull City 1 Liverpool 3
Liverpool wakicheza ugenini waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Hull City mabao yao yakifungwa na Alonso dakika ya 45 na mawili na Kuyt dakika ya 63 na 89. Bao la Hull lilifungwa na Giovanni dakika ya 72.
Kwenye dakika ya 59, Folan wa Hull City alilambwa Kadi Nyekundu na Refa Martin Atkinson kwa kumpiga teke Martin Skrtel.
West Ham 0 Chelsea 1
Bao la Salomon Kalou kwenye dakika ya 55 liliwapa ushindi mwembamba Chelsea waliocheza ugenini nyumbani kwa West Ham lakini Kalou huyo huyo angegeuka mbaya baada ya kutoa penalti alipomchezea vibaya Hireta Ilunga lakini penalti hiyo iliyopigwa na Mark Noble iliokolewa na Kipa Pete Cech.


MATOKEO MECHI NYINGINE:


Bolton 1 Aston Villa 1


Everton 1 Man City 2


Fulham 1 Stoke 0


West Brom 3 Sunderland 0


MECHI ZA LEO:

JUMAPILI, 26 April 2009
[Saa 9 na nusu]
Arsenal v Middlesbrough
[Saa 12 jioni]
Blackburn v Wigan


Powered By Blogger