Friday, 1 May 2009

NUSU FAINALI UEFA CUP:

Werder Bremen 0 Hamburg 1

Kwenye mechi ya Klabu za Kijerumani, Hamburg wameweza kuibuka na ushindi mzuri wa ugenini baada ya kuwapiga wenzao Werder Bremen 1-0 kwa bao alilofunga Piotr Trochowski.
Timu hizi zitarudiana Alhamisi ijayo.

Dynamo Kiev 1 Shakhtar Donetsky 1

Mechi hii imehusisha Timu za Ukraine na ngoma ni dro ingawa Shakhtar Donestsky watakuwa wanachekelea kwani wamepata kigoli cha ugenini kwenye suluhu ya 1-1 na timu hizi zinarudiana Alhamisi ijayo.
LIGI ITALIA KUVUNJIKA: Inaanzishwa 'LEGA CALCIO SERIE A'
Baada ya kuona mafanikio makubwa ya England wakati ilipoanziashwa LIGI KUU England, Italia wanataka kuiga nini kilichotokea huko kwa kuanzisha LIGI PEKEE ambayo itakuwa tofauti na Ligi nyingine ya Klabu zilizo Madaraja ya chini. Ligi hiyo itaitwa LEGA CALCIO SERIE A.
Klabu 19 za SERIE A zimesaini mkataba wa makubaliano kuanzisha Ligi hiyo mpya na Klabu pekee iliyogoma kusaini ni Lecce ambayo inachungulia kaburi la kushushwa Daraja.
Huko England, LIGI KUU ilizaliwa mwaka 1992 baada ya Klabu zilizokuwa kile kilichokuwa kinaitwa Daraja la Kwanza kujitenga na kuamua kuchukua madaraka yote ya kusimamia haki za kibiashara kwenye mechi zao wao wenyewe.
Waliamua, haki za Matangazo ya TV, Biashara na kila kitu kitaendeshwa na wao kama LIGI KUU England [yaani English Premier League] na kuwaachia mamlaka ya uendeshaji wa Sheria chini ya FIFA yaendelee kwenye mamlaka ya FA, Chama cha Soka England, na Football League wasimamie Madaraja ya Chini.
Tangu wakati huo Dunia imeshuhudia mafanikio makubwa kwa Timu za England na zimekuwa zikitawala Ulaya na sasa Duniani huku Manchester United wakitamba kuwa ndio Mabingwa wa Dunia.
Katika miaka miwili iliyopita England imeingiza Timu 3 kwenye Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na pia kwa miaka minne mfululizo Timu moja toka England imeingia Fainali.
Sasa Italia wanataka kuiga mafanikio hayo, ambayo Rais wa Klabu ya Palermo anaelezea: 'Tumeanzisha Ligi mpya ya Serie A. Hatuna furaha lakini huu ndio ukweli na hili litatendeka.'

No comments:

Powered By Blogger