Kiungo Ryan Giggs wa Manchester United ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa PFA [-Professional Footballers Association-Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa-] na hii ikiwa ni mara yake ya kwanza kuitwaa Tuzo hiyo ingawa ashawahi kushinda Tuzo hiyo wanayopewa Wachezaji Vijana mara mbili. Giggs, mwenye umri wa miaka 35, aliwabwaga wenzake wa Man U Nemanja Vidic, Rio Ferdinand, Cristiano Ronaldo, Edwin van der Sar na Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard kwa kushinda Tuzo hiyo.
Giggs, akiwa na Manchester United tangu aanze kuichezea mwaka 1991 akiwa na miaka 17, ameshashinda LIGI KUU mara 10, FA CUP mara 4, League Cup [siku hizi huitwa Carling Cup] mara 3 na UEFA CHAMPIONS LEAGUE mara 2.
Mchezaji Chipukizi wa Aston Villa, Asley Young, ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Vijana. Young amewabwaga kina Jonny Evans na Rafael Da Silva wa Man U, Aaron Lennon wa Spurs na Kiungo wa Manchester City Stephen Ireland.
Giggs, akitoa shukrani, alitamka: 'Ni tuzo kubwa sana!! Ni heshima kuipata kwani wanaochagua ni Wachezaji wenzangu!! Namshukuru sana Meneja wangu Sir Alex Ferguson!!! Yeye ni mtu muhimu sana maishani mwangu!! Nilikutana nae mara ya kwanza nikiwa na miaka 13 tu na kwa zaidi ya miaka 20 sasa, amenilea vizuri!!!'
Mbali ya kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora, Giggs pia ametajwa mmoja wa Kikosi cha Timu Bora ya Msimu ambayo ina jumla ya Wachezaji 6 kutoka Mabingwa Manchester United.
Tuzo hii pamoja na Kikosi cha Timu Bora huchaguliwa na kupigiwa kura na Wachezaji wote wa Kulipwa wanaochezea LIGI KUU England.
Kikosi kamili cha Timu Bora ni: Edwin Van der Sar (Manchester United), Glen Johnson (Portsmouth), Rio Ferdinand (Manchester United), Nemanja Vidic (Manchester United), Patrice Evra (Manchester United), Ashley Young (Aston Villa), Steven Gerrard (Liverpool), Ryan Giggs (Manchester United), Cristiano Ronaldo (Manchester United), Nicolas Anelka (Chelsea), Fernando Torres (Liverpool)
Monday, 27 April 2009
Giggs anyakua Tuzo ya Mchezaji Bora wa PFA!!!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment