Thursday 30 April 2009

LEO NI NUSU FAINALI UEFA CUP-Klabu za Ujerumani zinamenyana zenyewe na za Ukraine wanapambana wenyewe!!!
Leo usiku mechi za Nusu Fainali za Kombe la UEFA zitachezwa na ni vita kati ya Timu za Nchi ya Ukraine zinazopambana zenyewe kwenye Nusu Fainali ya kwanza na Nusu Fainali nyingine ni Timu za Nchi za Ujerumani.
Dynamo Kiev inacheza na Shakhtar Donetsk zote zikiwa zinatoka Ukraine na mechi nyingine ni Timu za Ujerumani Werder Bremen inayokwaana na Hamburg.
Marudiano ya mechi hizi ni wiki ijayo.
Washindi watakutana Fainali Mei 20.
RATIBA LIGI KUU ENGLAND: [saa ni za bongo]
Jumamosi, 2 Mei 2009
[saa 8 dak 45 mchana]
Middlesbrough v Man U
[saa 11 jioni]
Chelsea v Fulham
Man City v Blackburn
Portsmouth v Arsenal
Stoke v West Ham
Tottenham v West Brom
Wigan v Bolton
Jumapili, 3 Mei 2009
[saa 9 na nusu mchana]
Liverpool v Newcastle
[saa 12 jioni]
Sunderland v Everton
Jumatatu, 4 Mei 2009
[saa 4 usiku]
Aston Villa v Hull

Ferguson aionya Arsenal: 'Ni ngumu Arsenal kutuzuia kufunga goli Emirates!!!

Baada ya ushindi kiduchu wa bao 1-0 uwanjani kwake Old Trafford kwa bao lililopachikwa na Beki John O'Shea na huku wakikosa lundo la magoli, Mabingwa Watetezi Manchester United watatua Emirates Stadium Jumanne ijayo kurudiana na Arsenal na Meneja wa Mabingwa hao, Sir Alex Ferguson, ametamka itakuwa ngumu sana kwa Arsenal kuisimamisha kupata hata bao moja. Ili kuingia Fainali Arsenal inabidi aifunge Man U bao 2-0 na endapo Man U atapata bao moja basi inabidi Arsenal afunge bao 3.
Ferguson amesema: 'Najua tuna uwezo wa kwenda kwao Emirates na kufunga na hilo ndio tatizo kubwa kwa Arsenal!'
Nae Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amejitetea kwa kusema: 'Nna uhakika kwenye marudiano utaiona Arsenal nyingine! Pengine Man U watajuta kwa nini hawakufunga bao la pili!! Lakini pongezi kubwa ziende kwa Kipa Almunia alieokoa magoli mengi!!'

No comments:

Powered By Blogger