Sunday, 26 April 2009

Man U waibomoa Tottenham 5-2!!! Tottenham waliongoza 2-0 hadi mapumziko!!!

Wengi wanakumbuka mechi ya LIGI KUU England iliyochezwa White Hart Lane Septemba 2001 na Tottenham wakawa wanaongoza kwa bao 3-0 hadi mapumziko lakini Manchester United wakarudi kipindi cha pili na kushinda 5-3!!!

Jana mambo yalikuwa hivyo hivyo kwani hadi mapumziko, Man U 0 Tottenham 2!!

Bila shaka matokeo hayo yangebaki hivyo, Liverpool wangeshangilia kwani katika mechi waliyocheza jana lakini mapema kidogo, Liverpool waliifunga Hull City mabao 3-1 na kufikisha pointi 74 sawa na Man U lakini wakawa wanaongoza ligi kwa ubora wao wa magoli.

Hata hivyo, Mabingwa Man U waliibuka kipindi cha pili na kuibadili stori yote.

Carrick aliangushwa na Kipa Gomes kwenye boksi na Ronaldo akafunga penalti kuandika bao la kwanza dakika ya 57.

Dakika kumi baadae Rooney akasawazisha na dakika moja baadae Ronaldo akafunga bao tamu kwa kichwa na kuwafanya Man U waongoze kwa bao 3-2. Dakika tatu baadae Rooney akafunga la nne na Berbatov akachomeka la tano.

Mabingwa Man U sasa wako tena kileleni wakiwa na pointi 77 kwa mechi 33, Liverpool anafuata pointi 74 mechi 34 kisha Chelsea pointi 71 mechi 34 na Arsenal ni wa nne pointi 62 mechi 33.

Baada ya mechi Sir Alex Ferguson akizungumzia penalti:
"Ni bahati. Soka ni mchezo wa ajabu. Wiki iliyokwisha tulinyimwa penalti ya dhahiri na ikatung'oa kwenye Nusu Fainali ya FA CUP!! Lakini, kipindi cha pili cha mechi hii tulicheza vizuri sana!!!!"

Meneja waTottenham Harry Redknapp:
"Mechi iligeuka baada ya penalti! Kabla nilidhani hatufungwi. Ile penalti ni zawadi!! Ni kosa kubwa!! Howard Webb wanasema ndie Refa bora hapa sasa sijui huyo Refa mbovu yuko vipi!!"
Man Utd: Van der Sar, Rafael Da Silva (O'Shea 70), Ferdinand, Vidic, Evra, Ronaldo, Carrick, Fletcher (Scholes 61), Nani (Tevez 46), Berbatov, Rooney.
Akiba hawakucheza: Foster, Anderson, Evans, Macheda.
Kadi: Tevez, Scholes, Ronaldo.
Magoli: Ronaldo 57 pen, Rooney 67, Ronaldo 68, Rooney 71, Berbatov 79.
Tottenham: Gomes, Corluka, Woodgate, King, Assou-Ekotto, Lennon, Palacios, Jenas, Modric (Bale 86), Keane (Huddlestone 87), Bent.
Akiba hawakucheza: Cudicini, Hutton, Zokora, Bentley, Chimbonda.
Kadi: Woodgate, Jenas, Gomes.
Magoli: Bent 29, Modric 32.
Watazamaji: 75,458
Refa: Howard Webb
Hull City 1 Liverpool 3
Liverpool wakicheza ugenini waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Hull City mabao yao yakifungwa na Alonso dakika ya 45 na mawili na Kuyt dakika ya 63 na 89. Bao la Hull lilifungwa na Giovanni dakika ya 72.
Kwenye dakika ya 59, Folan wa Hull City alilambwa Kadi Nyekundu na Refa Martin Atkinson kwa kumpiga teke Martin Skrtel.
West Ham 0 Chelsea 1
Bao la Salomon Kalou kwenye dakika ya 55 liliwapa ushindi mwembamba Chelsea waliocheza ugenini nyumbani kwa West Ham lakini Kalou huyo huyo angegeuka mbaya baada ya kutoa penalti alipomchezea vibaya Hireta Ilunga lakini penalti hiyo iliyopigwa na Mark Noble iliokolewa na Kipa Pete Cech.


MATOKEO MECHI NYINGINE:


Bolton 1 Aston Villa 1


Everton 1 Man City 2


Fulham 1 Stoke 0


West Brom 3 Sunderland 0


MECHI ZA LEO:

JUMAPILI, 26 April 2009
[Saa 9 na nusu]
Arsenal v Middlesbrough
[Saa 12 jioni]
Blackburn v Wigan


No comments:

Powered By Blogger