Saturday 2 May 2009

Wenger aunga mkono Almunia kudakia England

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameunga mkono hatua ya ya Kipa wa Arsenal Manuel Almunia kuchezea England endapo atachukua uraia. Almunia ni raia wa Spain lakini hajawahi kudakia nchi hiyo na kwa sababu ameshakaa England tangu 2004 akiomba uraia wa England atapewa.
Mwenyewe Almunia, mwenye umri wa miaka 31, anasema: 'Spain hawajaniita. Sasa ikiwa England wanaona nafaa itabidi nifikirie.'
Kwa sasa Kipa nambari wani wa England ni David James, mwnye miaka 38, na anakaribia kustaafu na wanaogombea nafasi hiyo ni Paul Robinson, Chris Kirkland, Robert Green na Ben Foster.
Ferguson akerwa mechi kuchezwa mapema!!
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amekerwa na mechi yao ya leo ya LIGI KUU England na Middlesbrough kuchezwa saa 8 dakika 45 mchana, saa za bongo, wakati huko England ni saa 6 dakika 45 mchana wakati Jumatano walicheza mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huko Old Trafford na Arsenal.
Ferguson amesema: 'Ni sababu ya TV lakini ni mechi muhimu kwetu ingawa nitapumzisha baadhi ya Wachezaji.'
Kwa sasa wako pointi 3 mbele ya Liverpool ingawa wana mechi moja mkononi. Liverpool anacheza kesho na Newcastle.

No comments:

Powered By Blogger