Saturday 5 December 2009

KOMBE LA DUNIA: Wanasemaje Mameneja?
MAKUNDI:
Group A: South Africa, Mexico, Uruguay, France
Group B: Argentina, South Korea, Nigeria, Greece
Group C: England, USA, Algeria, Slovenia
Group D: Germany, Australia, Ghana, Serbia
Group E: Netherlands, Japan, Cameroon, Denmark
Group F: Italy, New Zealand, Paraguay, Slovakia
Group G: Brazil, North Korea, Ivory Cost, Portugal
Group H: Spain, Honduras, Chile, Switzerland
-Meneja wa Ufaransa, Raymond Domenech: "Tupo Kundi gumu! Inabidi tushinde mechi 2 ili kufuzu!"
-Meneja wa Italia, Marcello Lippi: "Inabidi tujitayarishe! Watu wanasema ni Kundi rahisi lakini lazima ufanye matayarisho!"
-Vicente Del Bosque, Meneja wa Spain: "Hatuna malalamiko! Hatuwezi kuficha ukweli kuwa sisi tunaonekana Timu bora!"  
-Meneja wa Ivory Coast, Vahid Halilhodzic: "Tupo Kundi gumu sana na Timu ngumu Brazil na Ureno! Inabidi tufanye maandalizi makali ili tuzipindue Timu hizo kali!"
-Meneja wa Ujerumani, Joachim Loew: "Ghana Timu ngumu, Australia tulicheza nao Kombe la Mabara na tunaiheshimu Serbia!"
-Meneja wa England, Fabio Capello: "Sio mbaya sana! Tushawahi kucheza na USA na Slovenia na kupata ushindi mzuri! Algeria pia wazuri kwani wamewafunga Egypt!! Lakini ikifika Juni mwakani Timu zote zitabadilika!"
-Meneja wa Afrika Kusini, Carlos Alberto Parreira: "Ni Kundi lenye usawa! Inabidi tufanye maandalizi ya hali ya juu na pia Watu wote waishangilie Bafana Bafana!! Hilo ni muhimu!!"
KOMBE LA DUNIA 2010: Makundi yapangwa, England yaridhika, Afrika ipo Makundi Magumu!!!
Jana, mjini Cape Town, Afrika Kusini, mbele ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Sepp Blatter wa FIFA na Watu maarufu kadhaa, Makundi Manane yenye Timu 4 kila moja yatakayocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani kuanzia Juni 11 hadi Julai 11, yalipangwa.
Yafuatayo ndiyo Makundi yenyewe:
Group A: South Africa, Mexico, Uruguay, France
Group B: Argentina, South Korea, Nigeria, Greece
Group C: England, USA, Algeria, Slovenia
Group D: Germany, Australia, Ghana, Serbia
Group E: Netherlands, Japan, Cameroon, Denmark
Group F: Italy, New Zealand, Paraguay, Slovakia
Group G: Brazil, North Korea, Ivory Cost, Portugal
Group H: Spain, Honduras, Chile, Switzerland
Mechi ya ufunguzi itachezwa 11 Juni 2010, Mjini Johannesburg kati ya Wenyeji Afrika Kusini na Mexico.

Friday 4 December 2009

RATIBA LIGI KUU WIKIENDI HII:
JUMAMOSI, DESEMBA 5:
[SAA 9 DAK 45]
Portsmouth v Burnley
[SAA 12 JIONI]
Arsenal v Stoke
Aston Villa v Hull
Blackburn v Liverpool
West Ham v Man U
Wigan v Birmingham
Wolves v Bolton
[SAA 2 NA NUSU USIKU]
Man City v Chelsea
JUMAPILI, DESEMBA 6
[SAA 12 JIONI]
Fulham v Sunderland
[SAA 1 USIKU]
Everton v Tottenham
Portsmouth yashindwa kulipa Wachezaji Mishahara!!!
Kwa mara ya pili sasa katika msimu huu, Klabu ya Ligi Kuu England, Portsmouth, imeshindwa kuwalipa Wachezaji wake Mishahara baada ya baadhi yao kukosa Mishahara ya Novemba.
Portsmouth yenyewe imethibitisha tukio hilo lakini imesema Wachezaji watalipwa leo. Mwezi Septemba Klabu hiyo ilishindwa kulipa Mishahara ingawa baadae walilipwa na Mnunuzi mpya wa Klabu hiyo Sulaiman Al Fahim alieinunua Klabu kutoka kwa Alexandre Gaydamak. Sulaiman kwa sasa ameuza asilimia 90 ya Klabu hiyo kwa Tajiri wa Saudi Arabia Ali Al Faraj lakini Al Faraj alikiri ameinunua Klabu kwa ajili ya faida tu na si Soka.
Kwa sasa Portsmouth imezuiwa na FA kutosajili Mchezaji yeyote hadi watakapozilipa Klabu nyingine Madeni yanayohusiana na ununuzi wa Wachezaji ambayo hawajayalipa.
DROO YA KOMBE LA DUNIA LEO!!
Baada ya Makapu kugawiwa na kupata mgawanyo wa Makapu manne ambayo yana Timu 8 kila moja, leo kuanzia saa 1 usiku saa za Bongo, droo ya kugawa Makundi na kupanga Ratiba ya Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Juni 11 hadi Julai 11 mwakani huko Afrika Kusini, itafanyika.
Makapu ni:
KAPU LA 1:
-Afrika Kusini
-Argentina
-Brazil
-England
-Germany
-Italy
-Netherlands
-Spain
KAPU LA 2:
-Australia
-Japan
-North Korea
-South Korea
-Honduras
-Mexico
-USA
-New Zealand
KAPU LA 3:
-Algeria
-Cameroun
-Ghana
-Ivory Coast
-Nigeria
-Chile
-Paraguay
-Uruguay
KAPU LA 4:
-Denmark
-France
-Greece
-Portugal
-Serbia
-Slovakia
-Slovenia
-Switzerland
Tayari Mwenyeji Afrika Kusini ashapangwa Kundi A na leo atapata Timu nyingine 3 lakini zitatoka nje ya Bara la Afrika kwani taratibu za Kombe la Dunia haziruhusu Timu 2 za Bara moja kuwa Kundi moja isipokuwa kwa Bara la ULaya tu kwani wao wana Timu 13 Fainali hizo na nazo ni nyingi.
CARLING CUP: Nusu Fainali yapangwa!!!
Hughes amshutumu Wenger!!!
Timu za Mji mmoja na ambazo ni Mahasimu wakuu, Manchester United na Manchester City, zimepangwa kukutana Nusu Fainali ya Kombe la Carling ambayo itachezwa kwa mechi 2, nyumbani na ugenini, hapo Januari 4 na 18 mwakani.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya Blackburn Rovers na Aston Villa.
Manchester United ambao ni Mabingwa Watetezi wa Kombe hili walitinga Nusu Fainali baada ya kuifunga Tottenham 2-0.
Manchester City waliitandika Arsenal 3-0.
Blackburn waliitoa Chelsea kwa penalti baada ya mechi kwisha 3-3. Nao Aston Villa waliibwaga Portsmouth 4-2.
Wakati huohuo Meneja wa Manchester City, Mark Hughes, amemshutumu Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, kwa tabia yake kwa kukataa kupeana mkono mara baada ya mechi ambayo Man City waliipiga Arsenal 3-0 na kuibwaga nje ya Carling Cup.
Hughes alifoka: “Pengine hajazoea kufungwa na ndio maana hajui kuwa na tabia nzuri akifungwa!”
Nae Wenger alijibu: “Nipo huru kupeana mkono na mtu yeyote!”

Wednesday 2 December 2009

KOMBE LA DUNIA FIFA kutangaza mgawanyo wa Timu kwa ajili ya DROO ya Ijumaa leo!!
Leo, mjini Cape Town South Africa, FIFA itatangaza mgawanyo wa Timu katika Makapu manne ili zipangiwe Makundi na Ratiba siku ya Ijumaa Desemba 4, droo ambayo pia itafanyika laivu Cape Town mbele ya Watu mashuhuri mbalimbali duniani na kushuhudiwa na moja kwa moja na Watu Milioni 200 kutoka Nchi 200 Duniani kote .
Droo hiyo ya Siku ya Ijumaa itaanza saa 1 usiku saa za bongo.
Makundi katika Fainali hizo za Kombe la Dunia zitakazochezwa kuanzia Juni 11 hadi Julai 11 mwakani yatakuwa manane ya Timu 4 kila moja zitakazocheza kwa mtindo wa Ligi na Timu mbili za juu zitaingia Raundi ya Pili.
Katika Kila Kundi haziruhusiwi kuwa na Timu 2 toka Bara moja lakini kwa vile Ulaya ndiyo ina Timu nyingi kwenye Fainali hizo ikiwa na Timu 13 ndilo Bara pekee linaloweza kuwa na Timu 2 Kundi moja.
Mgawanyo wa Makapu manne kwa Timu hizo 32 utafuata vigezo vya Ubora wa Timu na nafasi yake kwenye Listi ya Ubora ya FIFA, rekodi ya kulitwaa Kombe la Dunia na wapi Nchi inatoka, yaani Bara lipi.
Ingawa Afrika Kusini ni ya 82 kwa Ubora Duniani itawekwa Kapu la Kwanza kwa vile tu ni Wenyeji wa Mashindano. Kapu hili la kwanza litakuwa pia na Italia ambao ndio Mabingwa wa Watetezi wa Dunia na Timu nyingine kama vile Brazil, Spain, England na kadhalika.
Timu za Afrika zinategemewa kuwekwa Kapu lao peke yao.
Nchi zilizowahi kutwaa Kombe la Dunia ni Brazil, mara 5, Italy mara 4, Germany mara 3, Argentina na Uruguay mara 2 kila mmoja, England na Ufaransa mara 1 kila mmoja.
TIMU zilizofuzu kuingia Fainali ni:
WENYEJI: South Africa
AFRICA: Algeria, Cameroun, Ghana, Ivory Coast, Nigeria
ASIA: Australia, Japan, North Korea, South Korea
EUROPE: Denmark, England, France, Germany, Greece, Italy,Netherlands, Portugal, Serbia, Slovakia, Slovenia, Spain, Switzerland.
SOUTH AMERICA: Argentina, Brazil, Chile, Paraguay, Uruguay.
NORTH, CENTRAL AMERICA AND CARIBBEAN: United States, Mexico, Honduras
ASIA/OCEANIA: New Zealand.

CARLING CUP: Man U na Villa zatinga Nusu Fainali!!!!
Klabu za Manchester United, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe la Carling, na Aston Villa zimeingia Nusu Fainali baada ya kushinda mechi zao za Jumanne usiku.
Man U wakicheza kwao Old Trafford na kuchezesha Kikosi dhaifu waliifunga Tottenham  iliyokuwa fulu nondo mabao 2-0.
Mabao ya Man U yalifungwa na Darron Gibson.
Katika mechi hiyo, Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man U, alikaa jukwaani kwa Watizamaji kwani alikuwa akikamilisha kifungo chake cha mechi mbili alichopewa na FA kwa kumkashifu Refa Alan Wiley.
Juzi Jumamosi pia alikaa kwa Watizamaji katika mechi na Portsmouth ya LIGI KUU.
Nao Aston Villa wakicheza ugenini Uwanja wa Fratton Park waliifunga Portsmouth mabao 4-2.
Mabao ya Aston Villa yalifungwa na Stewart Downing, Emile Heskey, James Milner na Ashley Young.
Mabao ya Portsmouth yalipatikana kupitia Stiliyan Petrov wa Villa, aliejifunga mwenyewe, na Kanu.
Leo Jumatano Desemba 2, Mechi mbili za ROBO FAINALI zitachezwa kati ya Manchester City na Arsenal na nyingine ni Blackburn Rovers na Chelsea.
Droo ya mechi za NUSU FAINALI ya Kombe la Carling itafanywa mara baada ya mechi za Jumatano.
Powered By Blogger