Wednesday 2 December 2009

KOMBE LA DUNIA FIFA kutangaza mgawanyo wa Timu kwa ajili ya DROO ya Ijumaa leo!!
Leo, mjini Cape Town South Africa, FIFA itatangaza mgawanyo wa Timu katika Makapu manne ili zipangiwe Makundi na Ratiba siku ya Ijumaa Desemba 4, droo ambayo pia itafanyika laivu Cape Town mbele ya Watu mashuhuri mbalimbali duniani na kushuhudiwa na moja kwa moja na Watu Milioni 200 kutoka Nchi 200 Duniani kote .
Droo hiyo ya Siku ya Ijumaa itaanza saa 1 usiku saa za bongo.
Makundi katika Fainali hizo za Kombe la Dunia zitakazochezwa kuanzia Juni 11 hadi Julai 11 mwakani yatakuwa manane ya Timu 4 kila moja zitakazocheza kwa mtindo wa Ligi na Timu mbili za juu zitaingia Raundi ya Pili.
Katika Kila Kundi haziruhusiwi kuwa na Timu 2 toka Bara moja lakini kwa vile Ulaya ndiyo ina Timu nyingi kwenye Fainali hizo ikiwa na Timu 13 ndilo Bara pekee linaloweza kuwa na Timu 2 Kundi moja.
Mgawanyo wa Makapu manne kwa Timu hizo 32 utafuata vigezo vya Ubora wa Timu na nafasi yake kwenye Listi ya Ubora ya FIFA, rekodi ya kulitwaa Kombe la Dunia na wapi Nchi inatoka, yaani Bara lipi.
Ingawa Afrika Kusini ni ya 82 kwa Ubora Duniani itawekwa Kapu la Kwanza kwa vile tu ni Wenyeji wa Mashindano. Kapu hili la kwanza litakuwa pia na Italia ambao ndio Mabingwa wa Watetezi wa Dunia na Timu nyingine kama vile Brazil, Spain, England na kadhalika.
Timu za Afrika zinategemewa kuwekwa Kapu lao peke yao.
Nchi zilizowahi kutwaa Kombe la Dunia ni Brazil, mara 5, Italy mara 4, Germany mara 3, Argentina na Uruguay mara 2 kila mmoja, England na Ufaransa mara 1 kila mmoja.
TIMU zilizofuzu kuingia Fainali ni:
WENYEJI: South Africa
AFRICA: Algeria, Cameroun, Ghana, Ivory Coast, Nigeria
ASIA: Australia, Japan, North Korea, South Korea
EUROPE: Denmark, England, France, Germany, Greece, Italy,Netherlands, Portugal, Serbia, Slovakia, Slovenia, Spain, Switzerland.
SOUTH AMERICA: Argentina, Brazil, Chile, Paraguay, Uruguay.
NORTH, CENTRAL AMERICA AND CARIBBEAN: United States, Mexico, Honduras
ASIA/OCEANIA: New Zealand.

No comments:

Powered By Blogger