Wednesday 2 December 2009

CARLING CUP: Man U na Villa zatinga Nusu Fainali!!!!
Klabu za Manchester United, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe la Carling, na Aston Villa zimeingia Nusu Fainali baada ya kushinda mechi zao za Jumanne usiku.
Man U wakicheza kwao Old Trafford na kuchezesha Kikosi dhaifu waliifunga Tottenham  iliyokuwa fulu nondo mabao 2-0.
Mabao ya Man U yalifungwa na Darron Gibson.
Katika mechi hiyo, Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man U, alikaa jukwaani kwa Watizamaji kwani alikuwa akikamilisha kifungo chake cha mechi mbili alichopewa na FA kwa kumkashifu Refa Alan Wiley.
Juzi Jumamosi pia alikaa kwa Watizamaji katika mechi na Portsmouth ya LIGI KUU.
Nao Aston Villa wakicheza ugenini Uwanja wa Fratton Park waliifunga Portsmouth mabao 4-2.
Mabao ya Aston Villa yalifungwa na Stewart Downing, Emile Heskey, James Milner na Ashley Young.
Mabao ya Portsmouth yalipatikana kupitia Stiliyan Petrov wa Villa, aliejifunga mwenyewe, na Kanu.
Leo Jumatano Desemba 2, Mechi mbili za ROBO FAINALI zitachezwa kati ya Manchester City na Arsenal na nyingine ni Blackburn Rovers na Chelsea.
Droo ya mechi za NUSU FAINALI ya Kombe la Carling itafanywa mara baada ya mechi za Jumatano.

No comments:

Powered By Blogger