Friday 4 December 2009

DROO YA KOMBE LA DUNIA LEO!!
Baada ya Makapu kugawiwa na kupata mgawanyo wa Makapu manne ambayo yana Timu 8 kila moja, leo kuanzia saa 1 usiku saa za Bongo, droo ya kugawa Makundi na kupanga Ratiba ya Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Juni 11 hadi Julai 11 mwakani huko Afrika Kusini, itafanyika.
Makapu ni:
KAPU LA 1:
-Afrika Kusini
-Argentina
-Brazil
-England
-Germany
-Italy
-Netherlands
-Spain
KAPU LA 2:
-Australia
-Japan
-North Korea
-South Korea
-Honduras
-Mexico
-USA
-New Zealand
KAPU LA 3:
-Algeria
-Cameroun
-Ghana
-Ivory Coast
-Nigeria
-Chile
-Paraguay
-Uruguay
KAPU LA 4:
-Denmark
-France
-Greece
-Portugal
-Serbia
-Slovakia
-Slovenia
-Switzerland
Tayari Mwenyeji Afrika Kusini ashapangwa Kundi A na leo atapata Timu nyingine 3 lakini zitatoka nje ya Bara la Afrika kwani taratibu za Kombe la Dunia haziruhusu Timu 2 za Bara moja kuwa Kundi moja isipokuwa kwa Bara la ULaya tu kwani wao wana Timu 13 Fainali hizo na nazo ni nyingi.
CARLING CUP: Nusu Fainali yapangwa!!!
Hughes amshutumu Wenger!!!
Timu za Mji mmoja na ambazo ni Mahasimu wakuu, Manchester United na Manchester City, zimepangwa kukutana Nusu Fainali ya Kombe la Carling ambayo itachezwa kwa mechi 2, nyumbani na ugenini, hapo Januari 4 na 18 mwakani.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya Blackburn Rovers na Aston Villa.
Manchester United ambao ni Mabingwa Watetezi wa Kombe hili walitinga Nusu Fainali baada ya kuifunga Tottenham 2-0.
Manchester City waliitandika Arsenal 3-0.
Blackburn waliitoa Chelsea kwa penalti baada ya mechi kwisha 3-3. Nao Aston Villa waliibwaga Portsmouth 4-2.
Wakati huohuo Meneja wa Manchester City, Mark Hughes, amemshutumu Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, kwa tabia yake kwa kukataa kupeana mkono mara baada ya mechi ambayo Man City waliipiga Arsenal 3-0 na kuibwaga nje ya Carling Cup.
Hughes alifoka: “Pengine hajazoea kufungwa na ndio maana hajui kuwa na tabia nzuri akifungwa!”
Nae Wenger alijibu: “Nipo huru kupeana mkono na mtu yeyote!”

No comments:

Powered By Blogger