Saturday, 6 December 2008

LIGI KUU: Wakubwa washinda!!

Timu zinazoaminika ndio 'Wakubwa', yaani Liverpool, Chelsea na Arsenal, zote zimepata ushindi kwenye mechi zao za LIGI KUU za leo na Mabingwa wenyewe, Manchester United, watashuka uwanjani kwake Old Trafford muda si mrefu kuanzia sasa kuwakaribisha Sunderland ambao hawana Meneja baada ya Nahodha wa zamani wa Man U, Roy Keane, kubwaga manyanga.

MATOKEO YA MECHI ZA LEO NI:

Arsenal 1-0 Wigan

Blackburn 1-3 Liverpool

Bolton 0-2 Chelsea

Fulham 1-1 Man City

Hull 2-1 Middlesbrough

Newcastle 2-2 Stoke
CARLING CUP: NUSU FAINALI= Burnley v Tottenham na Derby v Man United

Dro ya Nusu Fainali ya Kombe la Carling imefanyika na Timu ya Daraja la chini ya LIGI KUU ambayo mpaka sasa imeshawatoa kwenye muchuano hiyo Timu za vigogo za LIGI KUU za Fulham, Chelsea na Arsenal wamepangiwa kigogo mwingine wa LIGI KUU Tottenham ambao pia ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo.
Nao Derby County, timu nyingine ya Daraja la chini ya LIGI KUU, itapambana na Mabingwa wa LIGI KUU Manchester United.
Nusu Fainali ya Kombe hili zitachezwa kwa mikondo miwili, nyumbani na ugenini, na mechi ya kwanza itachezwa wiki inayoanzia Januari 5, 2009 na marudiano wiki inayoanza Januari 19, 2009.
Fainali itachezwa tarehe 1 Machi 2009.
EVRA AFUNGIWA MECHI 4 NA FAINI PAUNI 15,000!!!

Beki wa pembeni kushoto wa Mabingwa Manchester United Patrice Evra amefungiwa mechi 4 na kupigwa faini ya Pauni ya 15,000 baada ya FA kumwona ana hatia ya kupigana na Mkata Majani wa Chelsea, Sam Bethell, kosa lililotendeka Stamford Bridge mara tu baada ya mechi ya Man U na Chelsea mnamo tarehe 26 Aprili 2008.
Kufuatia adhabu hii ambayo ataanza kuitumikia Desemba 22 na ambayo Klabu yake Man U wametamka bado wanaitafakari na watajua hivi karibuni nini wafanye, Evra atazikosa mechi za LIGI KUU dhidi ya Stoke, ikifuatiwa na ya Middlesbrough kisha ya Southampton kugombea Kombe la FA na ya mwisho ni mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la CARLING.

Baada ya kifungo hicho, Evra anaweza kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Chelsea kwenye LIGI KUU hapo Januari 11, 2009.
Klabu ya Chelsea nayo imepigwa faini ya Pauni 25,000 kwa kushindwa kumdhibiti mfanyakazi wao Sam Bethell.


SAKATA LA MIDO KUBAGULIWA: Wawili wabambwa na Polisi kutua kortini Jumanne!

Watu wawili wenye umri ya miaka 49 na 23 wanashikiliwa na Polisi kwa kutuhuma za kutoa matusi ya kibaguzi dhidi ya Mchezaji kutoka Misri Mido anaechezea Middlesbrough kwenye mechi dhidi ya Newcastle hapo tarehe 29 Novemba 2008 na watafikishwa Mahakamani Jumanne ijayo.
Mido alilalamika vikali kushambuliwa na Washabiki wa Newcastle kwa misimu miwili mfululizo kibaguzi bila FA kuchukua hatua yeyote.

Friday, 5 December 2008

UEFA CUP: Portsmouth yatolewa nje!, Aston Villa yafungwa lakini yasonga mbele!!

Portsmouth imetwangwa mabao 3-2 na Wolfsburg ya Ujerumani na hivyo kutolewa nje ya Kombe la UEFA.
Aston Villa nao walifungwa mabao 2-1 na MSK Milina lakini wamemudu kusonga mbele kutoka kwenye Kundi lake baada ya Hamburg kuwafunga Slovakia Prague 2-0.
Aston Villa sasa wanaungana na Manchester City kuingia Raundi nyingine.

RATIBA YA LIGI KUU WIKIENDI HII:

Jumamosi, 6 Decemba 2008

[saa 9 dak 45 mchana]

Fulham v Man City

[saa 12 jioni]

Arsenal v Wigan

Blackburn v Liverpool

Bolton v Chelsea

Hull v Middlesbrough

Newcastle v Stoke

[saa 2 na nusu usiku]

Man U v Sunderland

Jumapili, 7 Decemba 2008

[saa 12 jioni]

West Brom v Portsmouth

[saa 1 usiku]

Everton v Aston Villa

Jumatatu, 8 Decemba 2008

[saa 5 usiku]

West Ham v Tottenham

Thursday, 4 December 2008

ROY KEANE ANG'OKA SUNDERLAND!

Kukiwa kumebaki siku mbili tu kabla Meneja Roy Keane [37] hajaipeleka timu yake Sunderland Old Trafford kukutana na Bosi wake wa zamani Sir Alex Ferguson wa Manchester United ambako Keane alikuwa Mchezaji na Nahodha mwenye sifa za kipekee, Roy Keane ameamua kuachana na Sunderland.
Roy Keane alianza kazi ya Umeneja Sunderland Agosti 2006 na akaifanya Sunderland iwe Bingwa wa COCA COLA LIGI na kuipandisha LIGI KUU msimu uliofuatia.
Keane aliwanunua Djibril Cisse, Pascal Chimbonda, Anton Ferdinand, El-Hadji Diouf na George McCartney kwa jumla ya Pauni Milioni 30 lakini mbali ya kucheza mechi 15 za LIGI KUU timu hiyo imeshinda mechi 4 tu na wako nafasi ya 18, yaani watatu toka chini!
MIDO AILAUMU FA: 'Walifanya msimu uliopita, wamefanya msimu huu hakuna kitakachotokea!!'

Mido, Mchezaji kutoka Misri anaecheza Middlesbrough, amelalamika vikali kushambuliwa na Washabiki wa Newcastle kwa misimu miwili mfululizo kibaguzi bila FA kuchukua hatua.
Mido amesema: 'Waliendelea kuimba ubaguzi, maneno ya kukashifu dini ya Kiislam na bahati mbaya ni Mashabiki haohao wamerudia mara ya pili!'
Akisikitika sana Mido alinung'unika: 'Hii imetokea tena kwa sababu FA haikuchukua hatua mara ya kwanza! Mie sijali nitukanwe binafsi lakini usitukane Uislamu!! Nina hakika hata safari hii hamna lolote litafanyika! Ni ujinga tu!'


KAULI YA MIDO INAFUATIA TAARIFA ZETU TULOTOA MAPEMA [SOMA CHINI]

FA KUCHUNGUZA TUHUMA WASHABIKI WALIMBAGUA MIDO

FA, Chama cha Soka Uingereza, kinachunguza tuhuma kuwa Washabiki wa Newcastle walimkejeli Mido, Mchezaji wa Middlesbrough anaetoka Misri, kibaguzi wakati alipokuwa akipasha moto mwili katika mechi ya ligi kati ya Middlesbrough na Newcastle juzi mechi ambayo iliisha suluhu ya 0-0.Washabiki hao walisikika wakiimba nyimbo za ubaguzi wa rangi wakimlenga Mido.
DRO YA NUSU FAINALI YA CARLING CUP KUFANYIKA JUMAMOSI Desemba 6, 2008.

Baada ya Timu za Daraja la chini Burnley na Derby kufuzu kuingia Nusu Fainali hapo juzi baada ya Burnley kuiadhiri Arsenal bao 2-0 na Derby kuwatoa Stoke kwa bao 1-0, jana miamba wa LIGI KUU, Man U ambao ni Mabingwa wa England na Ulaya na Tottenham ambao ni Mabingwa Watetezi wa Kombe hili la CARLING wamefanikiwa nao kuingia Nusu Fainali huku Man U wakiwachakaza Blackburn 5-3 na Tottenham kuwapiga Watford 2-1.

Sasa nani anacheza na nani kwenye Nusu Fainali ya CARLING CUP itajulikana Jumamosi tarehe 6 Desemba 2008 wakati dro maalum itakapofanyika.

Mechi za Nusu Fainali zitatakiwa zichezwe kwa mtindo wa nyumbani na ugenini huku mechi ya kwanza inabidi ichezwe wiki ya kuanzia Januari 5, 2009 na marudiano ni wiki ya kuanzia Januari 19, 2009.

FAINALI itachezwa tarehe 1 Machi 2009.
MATOKEO MECHI ZA JUMATANO 3 DESEMBA 2008:

UEFA CUP: Man City 0 PSG 0

CARLING CUP: Man U 5 Blackburn 3 & Watford 1 Tottenham 2

Man U na Tottenham wajumuika na Burnley na Derby NUSU FAINALI!!!

Man Utd 5-3 Blackburn

Carlos Tevez ameibuka nyota wa mechi ya ya Robo Fainali ya Kombe la CARLING kwa kufunga mabao manne na kuwawezesha Man U waliochezesha chipukizi kuingia Nusu Fainali baada ya kuishindilia Blackburn iliyokuwa fulu mziki mabao 5-3.
Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson alishuhudia mechi hii akiwa ameketi kwenye jukwaa la Watazamaji kwani anatumikia kifungo cha mechi mbili za kutokukaa kwenye benchi la akiba la timu yake baada ya kufarakana na Refa Mike Dean kwenye mechi waliyocheza na Hull City.
Ferguson haruhusiwi pia kukaa benchi kwenye mechi ya LIGI KUU Jumamosi watakayocheza na Sunderland Old Trafford.
Mbali ya chipukizi Rafael da Silva, hakuna hata Mchezaji mmoja alieanza kwenye mechi ya Jumapili dhidi ya wapinzani wa jadi Man City ambayo Man U walishinda 1-0 alieanza mechi hii.
Tevez alifunga bao la kwanza kwa kichwa kwenye dakika ya 36 na kisha akamtengenezea Nani aliechomeka bao la pili dakika ya 41.
Kipindi cha pili, mtu wa bondeni Afrika Kusini, Benny McCarthy aliipatia bao la kwanza Blackburn baada ya kumshinda nguvu Gary Neville aliekuwa akicheza sentahafu pamoja na chipukizi Johnny Evans.
Lakini dakika 4 baadae, Tevez alichezewa vibaya na Ryan Nelsen na Refa Alan Wiley akaamua ipigwe penalti ambayo Tevez mwenyewe alifunga kifundi sana.
Dakika 3 baadae, gonga safi sana kati ya Giggs, Anderson na Tevez ilimaliziwa na Tevez aliefunga bao lake la 3.
Huku wakiongoza mabao 4-1, Man U waliamua kumuingiza Paul Scholes ambae hajacheza tangu Septemba alipoumizwa goti kwenye mechi iliyochezwa Denmark dhidi ya Aalborg kwenye mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Benny McCarthy na Derbyshire wakapata bao moja kila mmoja na kuifanya mechi iwe 4-3 huku zimesalia dakika 2 za nyongeza lakini ni Tevez tena aliewakata maini baada ya kufunga bao lake la 4 la mechi hiyo na la 5 kwa Man U kwa shuti kali sana.
Man Utd: Foster, Rafael Da Silva, Neville, Evans, O'Shea (Evra 66), Nani, Gibson, Possebon (Scholes 66), Anderson, Giggs (Manucho 71), Tevez.
Akiba hawakucheza: Kuszczak, Park, Vidic, Welbeck.
Magoli: Tevez 36, Nani 40, Tevez 51 pen, 54, 90.
Blackburn: Robinson, Olsson, Nelsen, Ooijer, Warnock, Treacy, Kerimoglu (Pedersen 70), Mokoena, Emerton (McCarthy 46), Derbyshire, Roque Santa Cruz (Fowler 76).
Akiba hawakucheza: Brown, Villanueva, Judge, Roberts.
Kadi: Nelsen.
Magoli: McCarthy 48, Derbyshire 84, McCarthy 90.
Watazamaji: 53,997.
Refa: Alan Wiley

Watford 1 Tottenham 2

Mabingwa Watetezi wa Kombe la Carling wamefanikiwa kuingia Nusu Fainali baada ya kutoka nyuma wakicheza ugenini na kuwafunga Watford mabao 2-1.
Watford, wanaocheza ligi daraja la chini ya LIGI KUU, walitangulia kufunga goli dakika ya 13 na Tottenham wakasawazisha kwa penalti dakika ya 45 baada ya Ross Jenkins kumchezea
faulo Jermaine Jenas na Mrusi Roman Pavlyuchenko akafunga penalti hiyo.
Katika dakika ya 76 Mshambuliaji wa Tottenham Darren Bent akafunga bao la pili na kuwawezesha Watetezi hao wa Kombe hili kuingia Nusu Fainali.

Wednesday, 3 December 2008

Arsenal na Stoke watupwa nje Kombe la Carling!

Burnley 2 Arsenal o

Burnley, timu iliyo nafasi ya 4 kwenye LIGI YA COCA COLA ambayo kidaraja iko chini tu ya LIGI KUU na ambayo Raundi iliyokwisha ya Kombe hili iliibwaga Chelsea nyumbani kwake Stamford Bridge kwa penalti 5-4 baada ya mechi kuisha 1-1, jana imeitwanga Arsenal iliyo LIGI KUU kwa mabao 2-0 na kuwatoa nje ya KOMBE LA CARLING na wao kuingia Nusu Fainali ya Kombe hilo.
Magoli mawili yaliyofungwa na Kiungo wa Burnley, Kevin McDonald, la kwanza likiwa dakika ya 6 ya mchezo na la pili dakika ya 57 ndio yalikitoa kikosi chenye chipukizi wengi cha Arsenal.
Kikosi hicho cha Arsenal kilikuwa na vijana kama Paul Rodgers [19], Jack Wilshere [16] na Aaron Ramsey [17] huku veterani Silvestre akiwa ndie sentahafu na safu ya ushambuliaji ikioongozwa na straika wao wa kutumainiwa Nicklas Bendtner aliyekosa lukuki ya mabao.
Burnley: Jensen, Duff, Carlisle, Caldwell, Jordan, Alexander, Blake (Elliott 77), McDonald (Gudjonsson 61), McCann, Eagles, Paterson (Akinbiyi 74).
Akiba hawakucheza: Penny, Mahon, Rodriguez, MacDonald.
Arsenal: Fabianski, Hoyte, Silvestre, Ramsey, Gibbs, Rodgers (Lansbury 46), Randall (Bischoff 72), Merida, Wilshere (Simpson 63), Bendtner, Vela.
Akiba hawakucheza: Mannone, Coquelin, Steer, Frimpong.
Kadi: Randall, Merida.
Watazamaji: 19,045
Refa: Andre Marriner

Stoke 0 Derby 1

Derby, timu iliyo daraja la chini ya LIGI KUU, jana iliifunga timu ya LIGI KUU Stoke bao 1-0 na kuwatoa nje ya Kombe la Carling na hivyo kuingia Nusu Fainali.
Bao la ushindi la Derby iliyocheza ugenini lilipatikana dakika ya 94 ya mchezo kwa penalti iliyofungwa na Nathan Ellington.
Penalti hiyo zikiwa zimebaki sekunde tu pambano liiinge muda wa nyongeza wa nusu saa ili kupata mshindi ilitolewa na Refa Rob Styles baada ya Beki wa Stoke Andy Griffin kuushika mpira kwenye boksi.

RATIBA YA LEO CARLING CUP:

Man U v Blackburn [saa 5 usiku]

Watford v Tottenham [saa 4 dak 45 usiku]

Tuesday, 2 December 2008

NDANI YA KABATI LA CRISTIANO RONALDO ZIPO TUZO ZIFUATAZO:

Cristiano Ronaldo, ambae leo alfajiri ameikwaa Tuzo ya Mpira wa Dhahabu[Ballon d'Or] ikimaanisha yeye ndie MCHEZAJI BORA WA ULAYA 2008, tangu atue Manchester United mwaka 2003 ameshatwaa Tuzo kibao.

Mlolongo wa Tuzo hizo, Mwaka aliozichukua na jina lake rasmi kwa Kiingereza ni kama ifuatavyo:

-Mchezaji Bora Chipukizi kwa Wachezaji wa Kulipwa 2004/5 & 2005/6 [FIFPro Special Young Player of the Year]
-Mchezaji Bora Chipukizi kwa Wachezaji wa Kulipwa wa Uingereza 2006/7 [PFA Young Player of the Year]

-Mchezaji Bora Alieteuliwa na Wachezaji wenzake wa Kulipwa Uingereza 2006/7 & 2007/8 [PFA Player's Player of the Year]

-Mchezaji Bora alieteuliwa na Mashabiki 2006/7 & 2007/8 [PFA Fans' Player of the Year]

-Mchezaji Bora alieteuliwa na Waandishi wa Habari wa Soka 2006/7 & 2007/8 [Football Writers' Footballer of the year]

-Mchezaji Bora wa Barclays [Wadhamini wa LIGI KUU] 2006/7 & 2007/8 [Barclays Player of the Season]

-Barclays Buti ya Dhahabu 2007/8 [Barclays Golden Boot]=Mfungaji Bora LIGI KUU

-Buti ya Dhahabu ya Ulaya 2007/8 [European Golden Shoe]=Mfungaji Bora wa Klabu Ulaya

-Fowadi Bora wa UEFA 2007/8 [UEFA Club Forward of the Year]

-Mchezaji Bora wa Klabu za Ulaya 2007/8 [UEFA Club Footballer of the Year]

-Mchezaji Bora wa Wachezaji wa Kulipwa Duniani 2007/8 [FIFPro World Player of the Year]

-Mchezaji Bora wa MEN 2008 [MEN Player of the Year]=MEN ni Gazeti la Manchester Evening News

-Mchezaji Bora wa Manchester United anaevikwa Tuzo ya Sir Matt Busby 2004, 2007 & 2008 [Sir Matt Busby Manchester United Player of the Year]

-Mchezaji Bora wa Manchester United 2007, 2008 [Manchester United Players' Player of the Year]
RATIBA YA SOKA WIKI HII:

Jumanne, 2 Desemba 2008

Carling Cup

[ssa 4 dak 45 usiku]

Burnley v Arsenal

Stoke v Derby

Jumatano, 3 Decemba 2008

UEFA CUP

[saa 4 dak 45 usiku]

Man City v PSG,

Carling Cup

Man U v Blackburn [saa 5 usiku]

Watford v Tottenham [saa 4 dak 45 usiku]

Alhamisi, 4 Decemba 2008

UEFA Cup

[saa 4 dak 45 usiku]

Aston Villa v MSK Zilina

Wolfsbyrg v Portsmouth

LIGI KUU UINGEREZA

Jumamosi, 6 Decemba 2008

[saa 9 dak 45 mchana]

Fulham v Man City

[saa 12 jioni]

Arsenal v Wigan

Blackburn v Liverpool

Bolton v Chelsea

Hull v Middlesbrough

Newcastle v Stoke

[saa 2 na nusu usiku]

Man U v Sunderland

Jumapili, 7 Decemba 2008

[saa 12 jioni]

West Brom v Portsmouth

[saa 1 usiku]

Everton v Aston Villa

Jumatatu, 8 Decemba 2008

[saa 5 usiku]

West Ham v Tottenham
RONALDO ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA ULAYA 2008: 'Ballon d'Or'!!!!

Mchezaji nyota wa Mabingwa wa Uingereza na Ulaya, Cristiano Ronaldo, leo alfajiri ametangazwa ndie mshindi wa Tuzo inayosifika ya 'Ballon d'Or', yaani 'Mpira wa Dhahabu, ambayo hutolewa na gazeti maarufu la soka liitwalo France Football Magazine na ambayo huzawadiwa kwa MCHEZAJI BORA WA ULAYA kila mwaka.
Ronaldo aliefunga mabao 42 msimu uliopita alizoa pointi 446 na kuwabwaga Lionel Messi (Barcelona) aliepata pointi 281 na Fernando Torres (Liverpool) aliepata 179 kufuatia kura zilizopigwa na Wandishi wa Habari 96 waliobobea toka kona zote za dunia.
Ronaldo, ambae pia ameshapata tuzo za Mchezaji na Mfungaji Bora wa Uingereza na Ulaya na pia Mchezaji Bora Duniani kwa Wachezaji wa kulipwa [FifPro World Player of the Year], anakuwa Mchezaji wa tatu wa Manchester United kunyakua tuzo hii.
Wengine ni: 1968 – George Best, 1965 – Bobby Charlton, 1964 – Denis Law.

Washindi wa Tuzo hii kwa miaka mitano iliyopita ni:

2007 – Kaka

2006 – Fabio Cannavaro

2005 – Ronaldinho

2004 – Andriy Shevchenko

2003 – Pavel Nedved
***********************************************************************************
Sir Alex Ferguson afurahia tuzo ya Balloon d'Or aliyopata Ronaldo!!!!
Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson amesema watu wote wa Manchseter United wanasikia fahari kubwa kwa Ronaldo kuzawadiwa Tuzo ya Mpira wa Dhahabu ikiashiria yeye ndie MCHEZAJI BORA WA ULAYA.
Ferguson akitabasamu alisema: 'Ni fahari kubwa! Manchester United imesubiri miaka 40 kwa tuzo hii! Mara ya mwisho alishinda Mchezaji wetu George Best mwaka 1968! Ronaldo ana miaka 23 tu na miaka yake bora bado iko mbele yake!'


LIGI KUU UINGEREZA: Liverpool 0 West Ham 0

Jana usiku wakiwa kwao Anfield, Liverpool walifanikiwa kuongoza LIGI KUU ingawa walicheza kandanda bovu na kutoka suluhu ya bila kufungana na West Ham.
Liverpool sasa ana pointi 34 kwa mechi 15, Chelsea 33 kwa mechi 15, Man U 28 kwa mechi 14 na Arsenal 26 kwa mechi 15.

Monday, 1 December 2008

KWA NINI RONALDO ALISHIKA MPIRA HUU?
[TIZAMA PICHA HII!!!]

Kona ya Rooney ilimkuta Ronaldo alieruka juu vizuri akiwa tayari kupiga kichwa na kufunga bao la pili kwa Man U katika mechi ya jana dhidi ya Watani wao wa Jadi Man City, lakini, kwa mshangao wa wengi, Mchezaji huyo ambae ndie Mchezaji Bora wa Uingereza na wa Dunia kwa Wachezaji wa Kulipwa na ambae pia inategemewa sana leo atatwaa taji lingine la Mchezaji Bora wa Ulaya kwa kunyakua tuzo ya Ballon d'Or [yaani MPIRA WA DHAHABU], aliinua mikono yake miwili na kuuzuia mpira huo!
Kabla ya hapo Ronaldo alikuwa keshapewa Kadi ya Njano.
Na kwa kosa hilo la kushika mpira akapewa Kadi ya pili ya Njano na ikabidi apewe Nyekundu na hivyo kutolewa nje ya uwanja kwenye dakika ya 68 akiiacha timu yake ilinde goli lake moja ikiwa na watu 10 tu uwanjani.
Mwenyewe Ronaldo amejitetea alisikia filimbi.
Meneja wa Man U, Sir Alex Ferguson, amezidi kumtetea leo kwa kusema: 'Nimeangalia tena video! Inaonyesha alisukumwa nyuma na mwenyewe amesema alisikia filimbi imepigwa!'
WENGI WANAJIULIZA: SI PIGA KICHWA KWANZA NA BAADAE UTAJUA REFA KAAMUA NINI?
SCOLARI ATAKA REFA AOMBE RADHI KWA KULIKUBALI BAO LA OFSAIDI!!
Mfungaji van Persie akiri aliotea!

Luis Felipe Scolari, Timu Meneja wa Chelsea, amemtaka Refa Mike Dean [pichani ] aliechezesha pambano lao na Arsenal aombe radhi kwa makosa aliyofanya kwa kulikubali bao la kwanza la Arsenal lililofungwa na Robin van Persie akiwa dhahiri ofsaidi.
Scolari amenung'unika: 'Nataka refa aangalie TV na kukiri amekosea! Tunataka refa akija Stamford Bridge achezeshe timu zote 2 na sio moja!'
Mfungaji wa bao hilo, Robin va Persie wa Arsenal amekiri kuwa alikuwa ameotea kwa kusema: 'Nilikuwa kidogo ofsaidi lakini ni goli kwani limekubaliwa! '


FA KUCHUNGUZA TUHUMA WASHABIKI WALIMBAGUA MIDO

FA, Chama cha Soka Uingereza, kinachunguza tuhuma kuwa Washabiki wa Newcastle walimkejeli Mido, Mchezaji wa Middlesbrough anaetoka Misri, kibaguzi wakati alipokuwa akipasha moto mwili katika mechi ya ligi kati ya Middlesbrough na Newcastle juzi mechi ambayo iliisha suluhu ya 0-0.
Washabiki hao walisikika wakiimba nyimbo za ubaguzi wa rangi wakimlenga Mido.

MSHAMBULIAJI WA EVERTON YAKUBU NJE MSIMU MZIMA!

Mshambuliaji wa Everton, Yakubu anaetoka Nigeria, atalazimika kuwa nje ya uwanja kwa msimu wote uliobakia baada ya kuumia.
Yakubu aliumia katika mechi ya timu yake ilipoifunga Tottenham bao 1-0 jana kwenye dakika ya 10 ya mchezo na akatolewa na kuingizwa Luis Saha ambae pia hakumaliza mechi hiyo kwani nae alijeruhiwa.


LEO LIVERPOOL v WEST HAM

Leo saa 5 usiku saa za kibongo, Liverpool wataingia uwanja wao wa Anfield kuwapokea West Ham na endapo watashinda basi watachukua uongozi wa LIGI KUU.
Mpaka sasa Chelsea, ambae jana alikung'utwa 2-1 na Arsenal kwake Stamford Bridge anaongoza akiwa na pointi 33 kwa mechi 15.

Liverpool ana pointi 33 kwa mechi 14 na Mabingwa Man U wanafuata wakiwa na pointi 28 kwa mechi 14 huku Arsenal wako nyuma yao wakiwa pointi 26 kwa mechi 15.
West Ham wako nafasi ya 15 wakiwa na pointi
17 kwa mechi 14.

Sunday, 30 November 2008

KWA MARA NYINGINE TENA DARAJA LA STAMFORD LAVUNJWA!

Chelsea 1 Arsenal 2

Arsenal, timu iliyofutwa kwenye kinyang'anyiro cha LIGI KUU baada ya vipigo mfululizo, leo imezinduka na kuitandika Chelsea wakiwa kwao Stamford Bridge kwa mabao ya Mdachi Robin van Persie.
Johan Djorou wa Arsenal alijifunga mwenyewe baada ya krosi ya Beki wa Chelsea Jose Bosingwa katika dakika ya 31 kumkuta na akashindwa kuifuta.
Lakini katika dakika ya 59, akionekana kuwa ofsaidi, Robin van Persie, alisawazisha na dakika mbili baadae akachomeka bao la ushindi kufuatia kushushiwa na Adebayor kwa kichwa.

MATOKEO MECHI NYINGINE ZA LIGI KUU LEO:

Tottenham 0 Everton 1

Portsmouth 3 Blackburn 2
KOMBE LA FA: DROO YA RAUNDI YA 3 IMETOKA!

TIMU ZA LIGI KUU KUANZA MAPIGANO!

MECHI KUCHEZWA WIKIENDI YA JANUARI 3 AU 4 2009!

Portsmouth v Bristol City

Sheffield Wed v Fulham

Preston v Liverpool

Birmingham v Wolves

West Ham v Barnsley

Middlesbrough v Barrow

Hull City v Newcastle

Hartlepool v Stoke

Chelsea v Southend

Manchester City v Nottingham Forest

Cardiff v Reading

Ipswich v Chesterfield or Droylsden

Charlton v Norwich

West Brom v Peterborough or Tranmere

Torquay v Blackpool

Leyton Orient v Sheffield United

Southampton v Manchester United

Millwall v Carlisle or Crewe

Histon v Swansea

Forest Green Rovers v Derby

QPR v BurnleyLeicester v Crystal Palace

Tottenham v Wigan

Morecambe or Cheltenham v Doncaster

Arsenal v Plymouth

Notts County or Kettering v Eastwood Town

Bournemouth or Blyth

Spartans v Blackburn

Macclesfield v Everton

Watford v Scunthorpe

Sunderland v Bolton

Coventry v Kidderminster

Gillingham or Stockport v Aston Villa
MAN CITY 0 MAN U 1
Rooney afunga goli la 100 na la ushindi kwa Man U! Ronaldo alambwa Kadi Njano 2 na kuona Nyekundu!

Mabingwa wa LIGI KUU, Manchester United, leo wamewatoa nishai jirani zao na watani wao wa jadi Manchester City tena wakiwa kwao City of Manchester Stadium baada ya kuwatungua kwa bao 1-0 bao lililofungwa na Wayne Rooney likiwa bao lake la 100 kwa mechi za klabu.
Kitu cha kushangaza kwenye mechi hii ni Refa kumpa Ronaldo Kadi ya Njano ya kwanza wakati alicheza mpira.
Ronaldo tena, akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga bao kwa kichwa, aliushika kwa mkono akidhani filimbi imepigwa!
Refa huyo Howard Webb akamtwanga Ronaldo Kadi ya pili ya Njano ikimaanisha Nyekundu na Ronaldo akatolewa nje!
Hivyo, Man U ilibidi wacheze dakika 22 zilizobaki wakiwa watu pungufu.
Lakini wakiwa watu 10, Mabingwa hao walisimama imara na kupata ushindi.

FERGUSON: Tulitawala mechi hii!!!

Sir Alex Ferguson anaamini kabisa timu yake ilistahili kushinda kwani ilitawala mechi yote dhidi ya Watani wao wa jadi.
Ferguson akihojiwa baada ya mechi alinena: 'Nadhani kipindi cha kwanza tulikuwa ni murua, bora sana! Hatugusiki! Wao kipindi cha pili, dakika 10 za kwanza, waliibuka lakini hawakuwa tishio hata chembe! Na ikabidi tucheze zaidi ya dakika 20 za mwisho tukiwa 10 tu! Si rahisi lakini hatukuwa hatarini!'
Refa Howard Webb alimuwasha Cristiano Ronaldo Kadi Nyekundu baada ya kumpa Kadi Njano 2 ya pili ikiwa baada ya Kona ya Rooney na yeye Ronaldo akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga kwa kichwa aliushika mpira kwa mikono miwili!
Ronaldo amedai alisikia filimbi ya Refa!
Ferguson amesema: 'Ronaldo kasema alisikia filimbi. Pengine vilevile alisukumwa nyuma! Siwezi kuzungumza hayo, tutakesha hadi asubuhi! Kitu muhimu tumeshinda na pointi 3 tunazo!
MECHI ZA LIGI KUU JANA:

Aston Villa 0 Fulham 0,

Stoke 1 Hull 1,

Sunderland 1 Bolton 4,

Wigan 2 West Brom 1,

Middlesbrough 0 Newcastle 0

Bolton wamezidi kuwakandamiza Sunderland kwa kuwapa kipigo cha mabao 4-1 nyumbani kwao na kuwafanya wateremke nafasi na kuingia lile kundi la timu 3 za mwisho zilizo nafasi ya kushuka daraja.
Fulham wakicheza nyumbani kwa Aston Villa waligangamara na kulazimisha suluhu ya 0-0.
Wigan, wakiwa nyumbani, walitoka nyuma baada ya kupachikwa bao na timu iliyo mkiani West Brom na kulazimisha ushindi wa 2-1.
Timu zilizopanda daraja msimu huu, Stoke City na Hull City, zilimenyana zenyewe na kujikuta ngoma droo ya 1-1.
Na timu zilizo majirani za Middlesbrough na Newcastle ziliumana vikali lakini hakuna mbabe aliepatikani na mechi ikaisha 0-0.


RATIBA MECHI ZA LEO:

Man City v Man u [saa 10 jioni bongo taimu]

[saa 12 jioni]

Portsmouth v Blackburn

Tottenham v Everton

[saa 1 usiku]

Chelsea v Arsenal
Powered By Blogger