Thursday 4 December 2008

MATOKEO MECHI ZA JUMATANO 3 DESEMBA 2008:

UEFA CUP: Man City 0 PSG 0

CARLING CUP: Man U 5 Blackburn 3 & Watford 1 Tottenham 2

Man U na Tottenham wajumuika na Burnley na Derby NUSU FAINALI!!!

Man Utd 5-3 Blackburn

Carlos Tevez ameibuka nyota wa mechi ya ya Robo Fainali ya Kombe la CARLING kwa kufunga mabao manne na kuwawezesha Man U waliochezesha chipukizi kuingia Nusu Fainali baada ya kuishindilia Blackburn iliyokuwa fulu mziki mabao 5-3.
Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson alishuhudia mechi hii akiwa ameketi kwenye jukwaa la Watazamaji kwani anatumikia kifungo cha mechi mbili za kutokukaa kwenye benchi la akiba la timu yake baada ya kufarakana na Refa Mike Dean kwenye mechi waliyocheza na Hull City.
Ferguson haruhusiwi pia kukaa benchi kwenye mechi ya LIGI KUU Jumamosi watakayocheza na Sunderland Old Trafford.
Mbali ya chipukizi Rafael da Silva, hakuna hata Mchezaji mmoja alieanza kwenye mechi ya Jumapili dhidi ya wapinzani wa jadi Man City ambayo Man U walishinda 1-0 alieanza mechi hii.
Tevez alifunga bao la kwanza kwa kichwa kwenye dakika ya 36 na kisha akamtengenezea Nani aliechomeka bao la pili dakika ya 41.
Kipindi cha pili, mtu wa bondeni Afrika Kusini, Benny McCarthy aliipatia bao la kwanza Blackburn baada ya kumshinda nguvu Gary Neville aliekuwa akicheza sentahafu pamoja na chipukizi Johnny Evans.
Lakini dakika 4 baadae, Tevez alichezewa vibaya na Ryan Nelsen na Refa Alan Wiley akaamua ipigwe penalti ambayo Tevez mwenyewe alifunga kifundi sana.
Dakika 3 baadae, gonga safi sana kati ya Giggs, Anderson na Tevez ilimaliziwa na Tevez aliefunga bao lake la 3.
Huku wakiongoza mabao 4-1, Man U waliamua kumuingiza Paul Scholes ambae hajacheza tangu Septemba alipoumizwa goti kwenye mechi iliyochezwa Denmark dhidi ya Aalborg kwenye mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Benny McCarthy na Derbyshire wakapata bao moja kila mmoja na kuifanya mechi iwe 4-3 huku zimesalia dakika 2 za nyongeza lakini ni Tevez tena aliewakata maini baada ya kufunga bao lake la 4 la mechi hiyo na la 5 kwa Man U kwa shuti kali sana.
Man Utd: Foster, Rafael Da Silva, Neville, Evans, O'Shea (Evra 66), Nani, Gibson, Possebon (Scholes 66), Anderson, Giggs (Manucho 71), Tevez.
Akiba hawakucheza: Kuszczak, Park, Vidic, Welbeck.
Magoli: Tevez 36, Nani 40, Tevez 51 pen, 54, 90.
Blackburn: Robinson, Olsson, Nelsen, Ooijer, Warnock, Treacy, Kerimoglu (Pedersen 70), Mokoena, Emerton (McCarthy 46), Derbyshire, Roque Santa Cruz (Fowler 76).
Akiba hawakucheza: Brown, Villanueva, Judge, Roberts.
Kadi: Nelsen.
Magoli: McCarthy 48, Derbyshire 84, McCarthy 90.
Watazamaji: 53,997.
Refa: Alan Wiley

Watford 1 Tottenham 2

Mabingwa Watetezi wa Kombe la Carling wamefanikiwa kuingia Nusu Fainali baada ya kutoka nyuma wakicheza ugenini na kuwafunga Watford mabao 2-1.
Watford, wanaocheza ligi daraja la chini ya LIGI KUU, walitangulia kufunga goli dakika ya 13 na Tottenham wakasawazisha kwa penalti dakika ya 45 baada ya Ross Jenkins kumchezea
faulo Jermaine Jenas na Mrusi Roman Pavlyuchenko akafunga penalti hiyo.
Katika dakika ya 76 Mshambuliaji wa Tottenham Darren Bent akafunga bao la pili na kuwawezesha Watetezi hao wa Kombe hili kuingia Nusu Fainali.

No comments:

Powered By Blogger