Sunday 30 November 2008

MAN CITY 0 MAN U 1
Rooney afunga goli la 100 na la ushindi kwa Man U! Ronaldo alambwa Kadi Njano 2 na kuona Nyekundu!

Mabingwa wa LIGI KUU, Manchester United, leo wamewatoa nishai jirani zao na watani wao wa jadi Manchester City tena wakiwa kwao City of Manchester Stadium baada ya kuwatungua kwa bao 1-0 bao lililofungwa na Wayne Rooney likiwa bao lake la 100 kwa mechi za klabu.
Kitu cha kushangaza kwenye mechi hii ni Refa kumpa Ronaldo Kadi ya Njano ya kwanza wakati alicheza mpira.
Ronaldo tena, akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga bao kwa kichwa, aliushika kwa mkono akidhani filimbi imepigwa!
Refa huyo Howard Webb akamtwanga Ronaldo Kadi ya pili ya Njano ikimaanisha Nyekundu na Ronaldo akatolewa nje!
Hivyo, Man U ilibidi wacheze dakika 22 zilizobaki wakiwa watu pungufu.
Lakini wakiwa watu 10, Mabingwa hao walisimama imara na kupata ushindi.

FERGUSON: Tulitawala mechi hii!!!

Sir Alex Ferguson anaamini kabisa timu yake ilistahili kushinda kwani ilitawala mechi yote dhidi ya Watani wao wa jadi.
Ferguson akihojiwa baada ya mechi alinena: 'Nadhani kipindi cha kwanza tulikuwa ni murua, bora sana! Hatugusiki! Wao kipindi cha pili, dakika 10 za kwanza, waliibuka lakini hawakuwa tishio hata chembe! Na ikabidi tucheze zaidi ya dakika 20 za mwisho tukiwa 10 tu! Si rahisi lakini hatukuwa hatarini!'
Refa Howard Webb alimuwasha Cristiano Ronaldo Kadi Nyekundu baada ya kumpa Kadi Njano 2 ya pili ikiwa baada ya Kona ya Rooney na yeye Ronaldo akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga kwa kichwa aliushika mpira kwa mikono miwili!
Ronaldo amedai alisikia filimbi ya Refa!
Ferguson amesema: 'Ronaldo kasema alisikia filimbi. Pengine vilevile alisukumwa nyuma! Siwezi kuzungumza hayo, tutakesha hadi asubuhi! Kitu muhimu tumeshinda na pointi 3 tunazo!

No comments:

Powered By Blogger