Tuesday 2 December 2008

RONALDO ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA ULAYA 2008: 'Ballon d'Or'!!!!

Mchezaji nyota wa Mabingwa wa Uingereza na Ulaya, Cristiano Ronaldo, leo alfajiri ametangazwa ndie mshindi wa Tuzo inayosifika ya 'Ballon d'Or', yaani 'Mpira wa Dhahabu, ambayo hutolewa na gazeti maarufu la soka liitwalo France Football Magazine na ambayo huzawadiwa kwa MCHEZAJI BORA WA ULAYA kila mwaka.
Ronaldo aliefunga mabao 42 msimu uliopita alizoa pointi 446 na kuwabwaga Lionel Messi (Barcelona) aliepata pointi 281 na Fernando Torres (Liverpool) aliepata 179 kufuatia kura zilizopigwa na Wandishi wa Habari 96 waliobobea toka kona zote za dunia.
Ronaldo, ambae pia ameshapata tuzo za Mchezaji na Mfungaji Bora wa Uingereza na Ulaya na pia Mchezaji Bora Duniani kwa Wachezaji wa kulipwa [FifPro World Player of the Year], anakuwa Mchezaji wa tatu wa Manchester United kunyakua tuzo hii.
Wengine ni: 1968 – George Best, 1965 – Bobby Charlton, 1964 – Denis Law.

Washindi wa Tuzo hii kwa miaka mitano iliyopita ni:

2007 – Kaka

2006 – Fabio Cannavaro

2005 – Ronaldinho

2004 – Andriy Shevchenko

2003 – Pavel Nedved
***********************************************************************************
Sir Alex Ferguson afurahia tuzo ya Balloon d'Or aliyopata Ronaldo!!!!
Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson amesema watu wote wa Manchseter United wanasikia fahari kubwa kwa Ronaldo kuzawadiwa Tuzo ya Mpira wa Dhahabu ikiashiria yeye ndie MCHEZAJI BORA WA ULAYA.
Ferguson akitabasamu alisema: 'Ni fahari kubwa! Manchester United imesubiri miaka 40 kwa tuzo hii! Mara ya mwisho alishinda Mchezaji wetu George Best mwaka 1968! Ronaldo ana miaka 23 tu na miaka yake bora bado iko mbele yake!'


LIGI KUU UINGEREZA: Liverpool 0 West Ham 0

Jana usiku wakiwa kwao Anfield, Liverpool walifanikiwa kuongoza LIGI KUU ingawa walicheza kandanda bovu na kutoka suluhu ya bila kufungana na West Ham.
Liverpool sasa ana pointi 34 kwa mechi 15, Chelsea 33 kwa mechi 15, Man U 28 kwa mechi 14 na Arsenal 26 kwa mechi 15.

No comments:

Powered By Blogger