Monday 1 December 2008

KWA NINI RONALDO ALISHIKA MPIRA HUU?
[TIZAMA PICHA HII!!!]

Kona ya Rooney ilimkuta Ronaldo alieruka juu vizuri akiwa tayari kupiga kichwa na kufunga bao la pili kwa Man U katika mechi ya jana dhidi ya Watani wao wa Jadi Man City, lakini, kwa mshangao wa wengi, Mchezaji huyo ambae ndie Mchezaji Bora wa Uingereza na wa Dunia kwa Wachezaji wa Kulipwa na ambae pia inategemewa sana leo atatwaa taji lingine la Mchezaji Bora wa Ulaya kwa kunyakua tuzo ya Ballon d'Or [yaani MPIRA WA DHAHABU], aliinua mikono yake miwili na kuuzuia mpira huo!
Kabla ya hapo Ronaldo alikuwa keshapewa Kadi ya Njano.
Na kwa kosa hilo la kushika mpira akapewa Kadi ya pili ya Njano na ikabidi apewe Nyekundu na hivyo kutolewa nje ya uwanja kwenye dakika ya 68 akiiacha timu yake ilinde goli lake moja ikiwa na watu 10 tu uwanjani.
Mwenyewe Ronaldo amejitetea alisikia filimbi.
Meneja wa Man U, Sir Alex Ferguson, amezidi kumtetea leo kwa kusema: 'Nimeangalia tena video! Inaonyesha alisukumwa nyuma na mwenyewe amesema alisikia filimbi imepigwa!'
WENGI WANAJIULIZA: SI PIGA KICHWA KWANZA NA BAADAE UTAJUA REFA KAAMUA NINI?

No comments:

Powered By Blogger