Wednesday 3 December 2008

Arsenal na Stoke watupwa nje Kombe la Carling!

Burnley 2 Arsenal o

Burnley, timu iliyo nafasi ya 4 kwenye LIGI YA COCA COLA ambayo kidaraja iko chini tu ya LIGI KUU na ambayo Raundi iliyokwisha ya Kombe hili iliibwaga Chelsea nyumbani kwake Stamford Bridge kwa penalti 5-4 baada ya mechi kuisha 1-1, jana imeitwanga Arsenal iliyo LIGI KUU kwa mabao 2-0 na kuwatoa nje ya KOMBE LA CARLING na wao kuingia Nusu Fainali ya Kombe hilo.
Magoli mawili yaliyofungwa na Kiungo wa Burnley, Kevin McDonald, la kwanza likiwa dakika ya 6 ya mchezo na la pili dakika ya 57 ndio yalikitoa kikosi chenye chipukizi wengi cha Arsenal.
Kikosi hicho cha Arsenal kilikuwa na vijana kama Paul Rodgers [19], Jack Wilshere [16] na Aaron Ramsey [17] huku veterani Silvestre akiwa ndie sentahafu na safu ya ushambuliaji ikioongozwa na straika wao wa kutumainiwa Nicklas Bendtner aliyekosa lukuki ya mabao.
Burnley: Jensen, Duff, Carlisle, Caldwell, Jordan, Alexander, Blake (Elliott 77), McDonald (Gudjonsson 61), McCann, Eagles, Paterson (Akinbiyi 74).
Akiba hawakucheza: Penny, Mahon, Rodriguez, MacDonald.
Arsenal: Fabianski, Hoyte, Silvestre, Ramsey, Gibbs, Rodgers (Lansbury 46), Randall (Bischoff 72), Merida, Wilshere (Simpson 63), Bendtner, Vela.
Akiba hawakucheza: Mannone, Coquelin, Steer, Frimpong.
Kadi: Randall, Merida.
Watazamaji: 19,045
Refa: Andre Marriner

Stoke 0 Derby 1

Derby, timu iliyo daraja la chini ya LIGI KUU, jana iliifunga timu ya LIGI KUU Stoke bao 1-0 na kuwatoa nje ya Kombe la Carling na hivyo kuingia Nusu Fainali.
Bao la ushindi la Derby iliyocheza ugenini lilipatikana dakika ya 94 ya mchezo kwa penalti iliyofungwa na Nathan Ellington.
Penalti hiyo zikiwa zimebaki sekunde tu pambano liiinge muda wa nyongeza wa nusu saa ili kupata mshindi ilitolewa na Refa Rob Styles baada ya Beki wa Stoke Andy Griffin kuushika mpira kwenye boksi.

RATIBA YA LEO CARLING CUP:

Man U v Blackburn [saa 5 usiku]

Watford v Tottenham [saa 4 dak 45 usiku]

No comments:

Powered By Blogger