Monday 1 December 2008

SCOLARI ATAKA REFA AOMBE RADHI KWA KULIKUBALI BAO LA OFSAIDI!!
Mfungaji van Persie akiri aliotea!

Luis Felipe Scolari, Timu Meneja wa Chelsea, amemtaka Refa Mike Dean [pichani ] aliechezesha pambano lao na Arsenal aombe radhi kwa makosa aliyofanya kwa kulikubali bao la kwanza la Arsenal lililofungwa na Robin van Persie akiwa dhahiri ofsaidi.
Scolari amenung'unika: 'Nataka refa aangalie TV na kukiri amekosea! Tunataka refa akija Stamford Bridge achezeshe timu zote 2 na sio moja!'
Mfungaji wa bao hilo, Robin va Persie wa Arsenal amekiri kuwa alikuwa ameotea kwa kusema: 'Nilikuwa kidogo ofsaidi lakini ni goli kwani limekubaliwa! '


FA KUCHUNGUZA TUHUMA WASHABIKI WALIMBAGUA MIDO

FA, Chama cha Soka Uingereza, kinachunguza tuhuma kuwa Washabiki wa Newcastle walimkejeli Mido, Mchezaji wa Middlesbrough anaetoka Misri, kibaguzi wakati alipokuwa akipasha moto mwili katika mechi ya ligi kati ya Middlesbrough na Newcastle juzi mechi ambayo iliisha suluhu ya 0-0.
Washabiki hao walisikika wakiimba nyimbo za ubaguzi wa rangi wakimlenga Mido.

MSHAMBULIAJI WA EVERTON YAKUBU NJE MSIMU MZIMA!

Mshambuliaji wa Everton, Yakubu anaetoka Nigeria, atalazimika kuwa nje ya uwanja kwa msimu wote uliobakia baada ya kuumia.
Yakubu aliumia katika mechi ya timu yake ilipoifunga Tottenham bao 1-0 jana kwenye dakika ya 10 ya mchezo na akatolewa na kuingizwa Luis Saha ambae pia hakumaliza mechi hiyo kwani nae alijeruhiwa.


LEO LIVERPOOL v WEST HAM

Leo saa 5 usiku saa za kibongo, Liverpool wataingia uwanja wao wa Anfield kuwapokea West Ham na endapo watashinda basi watachukua uongozi wa LIGI KUU.
Mpaka sasa Chelsea, ambae jana alikung'utwa 2-1 na Arsenal kwake Stamford Bridge anaongoza akiwa na pointi 33 kwa mechi 15.

Liverpool ana pointi 33 kwa mechi 14 na Mabingwa Man U wanafuata wakiwa na pointi 28 kwa mechi 14 huku Arsenal wako nyuma yao wakiwa pointi 26 kwa mechi 15.
West Ham wako nafasi ya 15 wakiwa na pointi
17 kwa mechi 14.

No comments:

Powered By Blogger