Saturday, 26 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

ZIGO LA AFRIKA KICHWANI GHANA: Sisi wote ni NYOTA NYEUSI!!!
Walikuwepo Wenyeji Afrika Kusini, maarufu Bafana Bafana, walikuwepo, Ivory Coast na kina Drogba, Cameroun na Eto’o, Nigeria na Algeria, lakini sasa imebaki ‘Nyota Nyeusi’ tu, Ghana, iliyobeba matumaini yote ya Afrika katika Fainali za Kombe la Dunia za kihistoria kwa vile kwa mara ya kwanza zinachezwa Afrika.
Leo, Jumamosi Juni 26, huko Uwanja wa Royal Bafokeng, Rustenburg Ghana inaivaa USA kwenye mechi ya Raundi ya Pili.
Ikiwa Ghana watashinda watakuwa wameifikia rekodi ya Cameroun ya Mwaka 1990 na Senegal 2002 ya Nchi ya Afrika kuweza kutinga Robo Fainali za Kombe la Dunia.
Ghana, bila Supastaa Michael Essien wa Chelsea, imewasuuza wengi akiwemo Jomo Sono wa Afrika Kusini ambae alikuwa maarufu kama Mchezaji na Mdau mkubwa wa Soka huko Bondeni na ambae ameisifia kwa kusema: “Ghana hawana majina makubwa, hawana wale Wachezaji nnaowaita wa Luninga! Wao wanacheza kitimu na kusaidiana. Hawana ubinafsi kama wengine!”
MUNGU IBARIKI GHANA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!
AMINA.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Uruguay Timu ya kwanza ndani ya Robo Fainali
Bao mbili za Mchezaji kutoka Klabu ya Ajax, Luis Suarez, zimewaingiza Uruguay Robo Fainali wakiwa ndio Timu ya kwanza kufuzu baada ya kuifunga Korea Kusini 2-1.
Suarez alifunga bao lake la kwanza dakika ya 8 kufuatia uzembe wa Difensi ya Korea na kumkuta mpira pembeni na kufunga kilaini.
Kipindi cha Pili dakika ya 68, Korea walirudisha baada ya frikiki kuunganishwa na Lee Chung-young.
Kona iliyopigwa dakika ya 80 ilimkuta Luis Suarez akiwa kushoto mwa goli na akapiga shuti la kupinda likagonga posti na kuipa ushindi Uruguay.
Robo Fainali, Uruguay itacheza na Mshindi kati ya USA v Ghana.
Maradona: “Veron ni Kocha wangu Uwanjani!’
Kocha wa Argentina Diego Maradona amesema Mchezaji Mkongwe Juan Sebastian Veron ndie Kocha wake akicheza Uwanjani.
Maradona na Veron walikutana Boca Juniors Mwaka 1996 wakati Maradona akikaribia kustaafu na Veron ndio kwanza anaanza kuchipukia.
Veron, Miaka 35, aliandika kwenye kitabu chake: “Ukweli kwamba nilicheza na Maradona ni heshima kubwa!”
Veron kwa sasa anachezea Klabu ya kwao huko Argentina, Estudiantes, baada ya kushindwa kuwika akiwa na Manchester United na baadae Chelsea lakini tangu arudi Estudiantes, Klabu aliyocheza nayo akianza Soka lake, Veron amewika na kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora Marekani ya Kusini mara mbili na pia kushinda Kombe la Klabu Bingwa Marekani ya Kusini, Libertadores na vilevile kurudishwa Kikosi cha Argentina ambacho hakuchukuliwa Fainali za Kombe la Dunia za huko Ujerumani Mwaka 2006 baada ya kutupiwa lawama ya kusababisha Argentina itolewe Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2002 Raundi ya Kwanza.
Ingawa Nahodha wa Argentina ni Javier Mascherano wa Liverpool, Maradona ameonyesha imani kubwa kwa Veron alipotamka: “Yeye ni Mchezaji wa Argentina anaejua Soka sana na ndio maana akicheza yeye ni Kocha wangu Uwanjani!”
Maradona aliongeza kwa kusema kuwa anamuhitaji sana Veron kwa vile anawahamasisha na kuwapigia kelele wenzake wakicheza Uwanjani.
Pia Maradona alinena: “Namuhitaji Veron kwa sababu ni Mtu pekee anaeweza kumkontroli Messi. Messi anamsikiliza sana Veron! Hilo ni jambo kubwa sana!”
CHEKI: www.sokainbongo.com

RATIBA: Jumapili, Juni 27
Saa 11 jioni: Uwanja Free State, Bloemfontein
England v Germany
Katika historia England na Germany zimeshakutana mara 31 na England wameshinda mechi 15, Germany mara 10, na sare 6.
England, chini ya Fabio Capello, imeshawahi kuifunga Germany bao 2-1 walipokutana Novemba 2008 Uwanja wa Olimpiki huko Berlin, Ujerumani.
Timu hizi mbili ni Mahasimu wakubwa na hii itakuwa mara ya 3 kukutana kwenye Mashindano makubwa katika Miaka 20 iliyopita.
Kwenye Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 1990 huko Italia na EURO 96, Germany iliibwaga England kwa penalti kwenye hatua ya Nusu Fainali.
Kwenye Fainali hizi huko Afrika Kusini, Germany walianza kwa kutisha walipoidunda Australia 4-0 lakini nao wakatwangwa 1-0 na Serbia kisha wakaifunga Ghana 1-0 kwa mbinde na kufuzu kuingia Raundi ya Pili.
England walianza kwa kusuasua kwenye Kundi lao kwa kupata sare za 1-1 na USA na 0-0 na Algeria na ikabidi waifunge Slovenia ili wafuzu na kweli walishinda 1-0.
Lakini, kwa ujumla, kiwango cha England kipo chini.
Wakati England hawana majeruhi kambini mwao, Germany inasemekana wana majeruhi wakiwemo Cacau, Bastian Schweinsteiger, Jerome Boateng, Mesut Ozil na Miroslav Klose ingawa baadhi wanategemewa kucheza.
Timu:
England: David James, Johnson, Ashley Cole, Terry, Upson, Barry, Lampard, Milner, Gerrard, Defoe, Rooney
Germany: Neuer, Friedrich, Mertesacker, Lahm, Badstuber, Scheinsteiger, Ozil, Khedira, Muller, Klose, Podolski.
Refa: J. Larrionda [Uruguay]
-------------------------------------------------------------------
Saa 3.30 usiku: Soccer City, Soweto, Johannesburg
Argentina v Mexico
Argentina na Mexico zimewahi kukutana mara 10 kwenye Fainali za Kombe la Dunia na Argentina wameshinda mara 7 kati ya hizo.
Mexico wataingia mechi hii wakitoka Kundi B ambako walitoka sare na Afrika Kusini 1-1, kuitandika Ufaransa 2-0 na kufungwa na Uruguay 1-0.
Argentina wao walishinda mechi zao zote kwa kuifunga Nigeria 1-0, Korea Kusini 4-1 na Ugiriki 2-0.
Wakati Mexico hawana uhakika kama Straika wa Arsenal Carlos Vela atakuwa fiti kucheza, Argentina hawana Mchezaji yeyote majeruhi.
Timu:
Argentina: Romero, Samuel, Demichelis, Gutierrez, Mascherano, Heinze, Veron, Di Maria, Tevez, Messi, Higuain.
Mexico: Perez, Moreno, Rodriguez, Osorio, Marquez, Salcido, Torrado, Guardado, Giovani, Franco, Hernandez.
Refa: Roberto Rosetti [Italy]
CHEKI: www.sokainbongo.com

FIFA yaionya Ufaransa
**Waziri ataka kuangusha kisago kwa walioleta aibu!!
FIFA imewasiliana na Serikali ya Ufaransa na kuwakumbusha kuwa wasiingilie masuala ya FFF, Chama cha Soka cha Ufaransa, kufuatia kutupwa nje ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini na Timu yao kukumbwa na mzozo mkubwa uliosababisha Mchezaji Nicolas Anelka atimuliwe toka kwenye Timu baada ya ugomvi na Kocha Raymond Domenech.
Kufuatia kuaibishwa kwa kumaliza Kundi lao wakiwa mkiani, Wizara ya Michezo ikiongozwa na Waziri, Bibi Roselyne Bachelot, imetaka serikali iingilie kati uozo uliokuwepo FFF.
Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, amesema wameijulisha Ufaransa kuhusu msimamo wa FIFA kuhusiana na masuala ya Soka kutoingiliwa na Serikali.
FIFA imewahi kuwasimamisha Uanachama baadhi ya Vyama vya Soka vya Nchi kwa kuingiliwa na Serikali katika uendeshaji wake na Valcke ametamka: “Tumeongea na Waziri na tumemjulisha wajibu wao. Wana uhuru wa kukutana nao, kujadiliana, kutaka Watu waombe radhi lakini wasiingilie uendeshaji na kutaka Watu wajiuzulu. FIFA itachukua hatua kama zilivyochukuliwa Nchi nyingine.”
CHEKI: www.sokainbongo.com

Kaiser aomba radhi
Mkongwe wa Ujerumani Franz Beckenbauer ameomba radhi kwa kauli zake za kuikandya England huku Timu hizi zikitegemewa kucheza Jumapili Juni 27 kwenye mechi ya Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.
Beckenbauer, aliewahi kushinda Kombe la Dunia kama Mchezaji na baadae kama Kocha akiwa na Ujerumani, alidaiwa kuisema England ni wapumbavu na wachovu.
Sasa amefuta kauli hizo na kudai zilimtoka tu baada ya kufadhaishwa na uchezaji wa hali ya chini wa England.

Friday, 25 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Spain, Chile zapita!!
Ni Brazil v Chile  & Spain v Ureno Raundi ya Pili!!
Spain imeifunga Chile bao 2-1 na kuingia Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia na pia ushindi huu umewafanya kuwakwepa Brazil Raundi ya Pili kwa kumaliza Kundi H wakiwa juu.
Spain watakutana na jirani zao Ureno na Brazil watacheza na wenzao toka Marekani ya Kusini Chile.
Mabao ya Spain yalifungwa na David Villa na Iniesta.
Rodrigo Millar ndie alieipa Chile bao.
Marco Estrada wa Chile alitolewa kwa Kadi Nyekundu na Refa Rodriguez toka Mexico kwa kosa la kutatanisha baada ya Fernando Torres kujidondosha wakati ilionekana wazi hakutegewa.
Uswisi 0 Honduras 0
Uswisi na Honduras zimetoka sare 0-0 katika mechi nyingine ya Kundi H na hivyo wote kutolewa nje ya Kombe la Dunia.
CHEKI: www.sokainbongo.com

RAUNDI YA PILI YA MTOANO TIMU 16 kuanza Kesho!!
Timu 16 zitakazocheza Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini zitakamilika baada ya Kundi la mwisho Kundi H, lenye Timu za Chile, Spain, Uswisi na Honduras, kumaliza mechi zao leo usiku Ijumaa Juni 25.
Mechi za Raundi hii ya Pili zinanaanza Jumamosi Juni 26.
Ratiba ya Jumamosi Juni 26
Saa 11 jioni:
URUGUAY v SOUTH KOREA
Nelson Mandela, Port Elizabeth
Saa 3.30 usiku:
USA v GHANA
Royal Bafokeng, Rustenburg
TATHMINI:
Uruguay v South Korea
Uruguay walifuzu kuingia Raundi hii baada ya kutwaa uongozi wa Kundi A waliposhinda mechi mbili na kutoka sare moja.
South Korea, wakiongozwa na Nahodha Park Ji-Sung toka Manchester United, wametoka Kundi B ambako walishinda mechi moja, sare moja na kufungwa moja.
Timu hizi zimewahi kukutana mara 4 hapo nyuma na Uruguay wameshinda mechi 3 na sare moja.
Huko Afrika Kusini, Uruguay walitoka sare na Ufaransa na kuzitungua Bafana Bafana na Mexico.
Korea walishinda mechi ya kwanza dhidi ya Ugiriki, wakafungwa na Argentina na kutoka sare na Nigeria.
Mshindi wa mechi hii atakutana na Mshindi wa mechi kati ya USA v Ghana kwenye Robo Fainali.
Wakati Korea hupenda kutumia fomesheni ya 4-4-2 huku Park Ji-Sung na Lee Chung-yong wakileta moto toka kwenye Winga, Uruguay hupenda kutumia 4-3-3 inayoongozwa na Washambuliaji Edinson Cavani wa Klabu ya Palermo, Italia na Luis Suarez na Diego Forlan.
USA v Ghana
Meneja wa USA, Bob Bradley, ambae mwanawe Michael Bradley ni mmoja wa Wachezaji shupavu wa USA, ana imani ya hali ya juu na Timu yake akiamini itafika Fainali hapo Julai 11.
USA walimaliza Kundi C wakiwa sawa na England kwa pointi 5 kila mmoja lakini waliukwaa uongozi kwa kufunga goli nyingi.
Ghana walimaliza Kundi D nyuma ya Germany na ndio Timu pekee toka Afrika iliyobaki kwenye Mashindano haya makubwa yanayofanyika Afrika kwa mara ya kwanza.
Bradley ameizungumza Ghana: “Timu hii Ghana chini ya Kocha Milovan Rajevac ni nzuri sana! Wametulia, wana vipaji na pia wana nguvu!”
Wakati USA watawategemea sana Altidore, Clint Dempsey na Landon Donovan, Ghana wapo kina Asamoah Gwyan, Ayew [Mtoto wa Abedi Pele], Mensah na Kipa Kingston ambae ni imara mno.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Cannavaro akiri Italia vijeba!!
Fabio Cannavaro amewataka Viongozi Italy wawekeze katika kuwaendeleza Vijana baada ya Timu yao iliyonyakua Kombe la Dunia Mwaka 2006 kutolewa Raundi ya Kwanza tu ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini kwa kumaliza Kundi lao kwa kupigwa 3-2 na Slovakia hivyo kubaki mkiani huku Timu ‘vibonde’ New Zealand ikiwa juu yao.
Cannavaro, Miaka 36, aliekuwa Nahodha wa Italy na anaejiuzulu kuchezea Timu ya Taifa, amekiri: “Lazima tuendeleze Vijana! Lazima tujifunze toka aibu hii la sivyo itachukua tena Miaka 27 kushinda tena Kombe la Dunia.”
Timu ya Italy iliyocheza huko Afrika Kusini ilikuwa na Wachezaji 9 wenye umri zaidi ya Miaka 30.
Kustaafu kwa Cannavaro kunamfanya Kipa Gianluigi Buffon awe ndio Kepteni mpya wa Italy.
Pia Cannavaro anaenda Dubai kuchezea Klabu yake mpya Al-Ahli ya huko.
Italia itakuwa na Kocha mpya Cesare Prandelli kuanzia Julai 1.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Brazil, Ureno zaingia Raundi ya Pili!
Ivory Coast 3 North Korea 0
Brazil na Ureno zimetoka sare 0-0 na zote zimeweza kuingia Raundi ya Pili ya Mtoano ya Timu 16 ya Kombe la Dunia na watakutana na Timu toka Kundi H ambalo lina Chile, Spain, Honduras na Uswisi ambazo zinacheza baadae leo kuamua hatma ya Kundi hilo na nani atacheza na Brazil na Ureno.
Licha ya kuifunga North Korea 3-0, Ivory Coast imeyaaga mashindano
haya kwa kumaliza nafasi ya 3.
Hivyo, kwa Afrika, ni Ghana pekee ndio iko Raundi ya Pili.
RATIBA: Jumamosi Juni 26
Raundi ya Pili Mtoano wa Timu 16
[saa za bongo]
Saa 11 jioni: Uruguay v South Korea Nelson Mandela, Port Elizabeth
Saa 3.30: USA v Ghana Royal Bafokeng, Rustenburg
Dunga na Bifu lake na Mapaparazi wa Brazil
Timu ya Brazil siku zote huandamwa na kundi kubwa la Wanahabari popote wanapoenda na huko Afrika Kusini waliko kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia hali si tofauti.
Kuna Waandishi zaidi ya 700 wanaotoka Brazil kuifuatilia Timu yao.
Lakini safari hii, tofauti na miaka ya nyuma, kazi yao imekuwa ngumu mno kwani walikuwa wamezoea kuongea na Timu na Mchezaji yeyote wakati wowote wanaotaka lakini safari hii wamewekewa ngumu na Kocha wa Brazil Dunga ambae ameiondoa kabisa fursa hiyo na hivyo kuleta msuguano mkubwa kati yake na Wanahabari hao.
Dunga amewaamrisha Wachezaji kutoongea na Wanahabari na pia amewazuia kufika kwenye mazoezi na maamuzi hayo yamewastua na kuwakera Waandishi wa Habari.
Huko Ujerumani, kwenye Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2006, kundi la Wanahabari walikuwa na uhuru mkubwa wa kuongea na Wachezaji na ilifika siku Ronaldo na Roberto Carlos walihojiwa alfajiri ili wawe laivu kwenye TV kubwa huko kwao Brazil.
Baada ya Brazil kubwagwa nje ya Mashindano hayo yakaanza malalamiko toka kila upande kuwalaumu Wanahabari kwa kuwaandama Wachezaji masaa 24.
Ndipo alipoingia Dunga kama Kocha wa Brazil na kufutilia mbali hiyo sarakasi ya Wanahabari.
Huko Afrika Kusini, Brazil inaruhusu Waandishi kuongea na Wachezaji wawili tu kwa siku na mazoezi hufanywa bila ya Wanahabari kuwepo.
Hata Mashabiki wamezuiwa kwenda mazoezini na ni mara moja tu, kama FIFA inavyotaka, ndio mazoezi yalikuwa wazi kwa Waandishi na Mashabiki.
Hali hii imeleta manung’uniko makubwa toka kwa hao Waandishi kutoka Brazil lakini Dunga ameshikilia msimamo wake na amesema: “
Kuna Waandishi 300 toka Brazil wanangojea tu Selecao ifungwe!”
Katika mkutano mmoja na Wanahabari mara baada ya Brazil kuifunga Korea Kaskazini 2-1 katika mechi ya ufunguzi yao ya Kombe la Dunia, Dunga alizozana na mmoja wa Waandishi na akamwambia: “Mwaka jana, Robinho alipokuwa akichezea Manchester City, wengi hawakutaka achezee Brazil! Na wewe ulikuwa mmoja wao!”
Kuhusu kutoruhusu Wanahabari mazoezini, Dunga aliwaambia: “Nyie siku zote mnalalamika Wachezaji sio wabunifu sasa kama humuoni mazoezi basi kuweni wabunifu na mtunge stori zenu!”
Ballack ajiunga Bayer Leverkusen
Kiungo wa zamani wa Chelsea Michael Ballack amerudi kwao Ujerumani na kujiunga na Klabu aliyowahi kuichezea zamani Bayer Leverkusen kwa mkataba wa Miaka miwili.
Ballack, Miaka 33, ambae amezikosa Fainali za Kombe la Dunia kwa kuumia, hakuongezewa Mkataba na Chelsea na hivyo amejiunga Bayer Leverkusen kama Mchezaji huru.
Ballack aliwahi kuichezea Bayer Leverkusen kati ya 1999 na 2002 na alifika nayo Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI Mwaka 2002.
Kisha akahamia Bayern Munich hadi Mwaka 2006 alipojiunga na Chelsea.
PITIA: www.sokainbongo.com

Fergie adai Kombe linaenda Marekani ya Kusini
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amebashiri kuwa Kombe la Dunia litaenda katika moja ya Nchi za Marekani ya Kusini.
Hadi sasa Timu 5 za Marekani ya Kusini hazijafungwa na huenda zote zikatinga Raundi ya Pili ya Timu 16.
Nchi hizo ni Uruguay, Chile, Brazil, Paraguay na Argentina.
Ferguson amesema: “Nahisi Brazil. Paraguay ni hatari wana nguvu na kasi. Chile wamefanya vizuri na Argentina ni wazuri. Lakini Brazil bado wana ule uchawi! Ukianza kufikiria hii si ile Brazil ya zamani, wao ndio hubadilika!”
Kuhusu England, Ferguson amesema Timu hiyo bado ipo kwenye kinyang’anyiro ingawa mategemeo makubwa ya Washabiki ndio yanaiathiri Timu kwa kuipa presha kubwa.
Alipoulizwa kuhusu Mchezaji wake Patrice Evra ambae ni Nahodha wa France iliyotolewa kwenye Kombe la Dunia na ambayo imekumbwa na matatizo makubwa kambini kwake ilipokuwa Afrika Kusini hadi Mchezaji Nicolas Anelka akafukuzwa, Ferguson amesema alibadilishana meseji na Evra ambae kwa sasa anaenda vakesheni.
Ferguson amezungumza: “Hatujui nini hasa kilitokea lakini inasikitisha. Kitu cha mwisho unachotaka ni mgomo kambini. Inaweza kuwa walikuwa na sababu za msingi lakini wangefikiria wale maelfu waliosafiri hadi Afrika Kusini kuwashangilia!”
CHEKI: www.sokainbongo.com

Kanu ang’atuka Nigeria
Nahodha wa Nigeria, Kanu, ametangaza rasmi kujiuzulu kuichezea Timu ya Taifa ya Nigeria baada ya kuichezea kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini na kutolewa Raundi ya Kwanza.
Hata hivyo Kanu alidokeza kabla ya kushiriki Mashindano hayo atajiuzulu na alianza kuichezea Nigeria tangu Mwaka 1994 na kucheza mechi 80.
Kanu amewahi kushinda Kombe la Dunia kwa Vijana Chini ya Miaka 17, Medali ya Dhahabu ya Olimpiki na pia kumaliza wakiwa Washindi wa Pili na wa Tatu Kombe la Mataifa ya Afrika.
Kanu ameshawahi kuwa Mchezaji Bora Afrika mara mbili Mwaka 1996 na 1999.
Kanu amechezea Fainali za Kombe la Dunia mara tatu Mwaka 1998, 2002 na 2010.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Japan yaingia Raundi ya Pili pamoja na Holland,  yaipiga Denmark 3-1
Holland imeifunga Cameroun bao 2-1 na kujihakikishia kuongoza Kundi E na hivyo kukutana na Slovakia hapo Jumatatu Juni 28 kwenye Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.
Katika mechi hii Robin Van Persie alifunga bao la kwanza dakika ya 36 na Samuel Eto'o akasawazisha kwa Cameroun dakika ya 65 kwa penalti.
Huntelaar akafunga bao la pili kwa Uholanzi dakika ya 83 na kuwapa ushindi wao wa 3 kwenye Kundi lao.
Katika mechi nyingine, Japan ilichukua nafasi ya pili walipoifunga Denmark bao 3-1.
Japan watacheza na Paraguay Raundi ya Pili.
Magoli ya Japan yalufungwa na Honda dakika ya 17, Endo dakika ya 30 na Okazaki dakika ya 87.
Goli la Denmark alifunga Tomasson dakika ya 81.
PITIA: www.sokainbongo.com

Magazeti Ufaransa yamchamba Domenech na Les Bleus……
Magazeti Bondeni yaisifia Bafana Bafana!!!!!!!!!!!!!!
Ufaransa ilisafirishwa kurudi kwao kwa fedheha kubwa baada ya kutolewa raundi ya Kwanza ya Kombe la Dunia na Wachezaji kupandishwa Daraja la chini kwenye Ndege huku wakiandamwa kwa maneno mabovu toka kila Gzeti la Nchi hiyo ambayo mengi yalimtoa kafara Kocha wake Raymond Domenech.
Licha ya kubwagwa nje ya Kombe la Dunia na kuweka historia ya kuwa Mwenyeji wa kwanza wa Fainali za Kombe la Dunia kutolewa Raundi ya Kwanza, Bafana Bafana imezoa sifa toka kila Gazeti la Afrika Kusini.
Huko Ufaransa, Gazeti la Michezo, L’Equipe, liliandika bango kubwa: ‘Mwisho wa Dunia Moja!” wakimlenga Kocha Raymond Domenech na kumkebehi baada ya kunukuliwa akiongea na Wanahabari mara baada ya kupigwa 3-2 na Bafana Bafana katika mechi ya mwisho akisema: “Mimi natoka Dunia nyingine.”
Gazeti jingine Le Parisien lilitoa kichwa: ‘Ahsante na Kwa heri!’
Kuna Gazeti moja, Liberation, lilihoji hata kuwepo kwa Ufaransa huko Afrika Kusini na kudai walidhulumu nafasi ya Ireland baada ya ile skandali ya Thierry Henry ya kushika mpira katika mechi na Ireland na kumpasia Gallas aliesawazisha na kuipeleka Ufaransa Fainali za Kombe la Dunia.
Gazeti hilo lilidai sasa haki imetendeka kwa Ufaransa kuaibishwa na kufedheheshwa.
Huko Afrika Kusini, Magazeti yameisifia Bafana Bafana kwa kuyaaga Mashindano hayo kwa ushindi dhidi ya vigogo Ufaransa

Thursday, 24 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Mabingwa wa Dunia Italy NJEEE, wavuliwa Taji!!!!!!
Himaya ya Italia kama Mabingwa wa Dunia leo imemalizwa rasmi kwenye Uwanja wa Ellis Park, Johannesburg waliponyukwa bao 3-2 na Timu ‘ndogo’ toka Nchi ndogo sana, Slovakia.
Mbali ya kutupwa nje ya Kombe la Dunia, Italia wameaibishwa kwa kumaliza Kundi F wakiwa mkiani wakipitwa na hata Timu ‘kibonde’ New Zealand.
Aliekuwa mwiba mkubwa na alieongoza kipigo cha Italy ni Straika Vittek wa Slovakia aliefunga bao mbili, dakika ya 25 na 73.
Kopunek alifunga bao la 3 dakika ya 89.
Mabao ya Italy yalifungwa na Di Natale dakika ya 81 na Quagliarella dakika ya 90.
Ushindi huu umeifanya Slovakia iingie Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia na itacheza na Mshindi wa Kundi E ambae nafasi kubwa ipo kwa Uholanzi.
Timu:
Italy:
Marchetti, Zambrotta, Cannavaro, Chiellini, Criscito, Gattuso, De Rossi, Montolivo, Pepe, Iaquinta, Di Natale.
Akiba: Buffon, Maggio, Gilardino, Bocchetti, Marchisio, Camoranesi, Palombo, Quagliarella, Pazzini, Pirlo, Bonucci, De Sanctis.
Slovakia:
Mucha, Pekarik, Skrtel, Durica, Zabavnik, Hamsik, Strba, Kucka, Stoch, Vittek, Jendrisek.
Akiba: Pernis, Cech, Weiss, Kozak, Sestak, Sapara, Holosko, Jakubko, Kopunek, Salata, Petras, Kuciak.
Refa: Howard Webb [Italy]
Paraguay yatinga Raundi ya Pili
Paraguay imetoka sare ya 0-0 na New Zealand na hivyo kuongoza Kundi F na kuingia Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia ikiungana na Slovakia ambao wamemaliza nafasi ya pili.
New Zealand wamemaliza wakiwa nafasi ya 3, juu ya waliokuwa Mabingwa wa Dunia Italy ambao wameshika mkia na kutupwa nje ya Kombe la Dunia.
New Zealand wametoka sare mechi zao zote za Kundi F.
Raundi ya Pili, Paraguay watacheza na Mshindi wa Pili wa Kundi E.
Scholes kustaafu 2011
Kiungo wa Manchester United, Paul Scholes, Miaka 35, amesema atacheza Soka Msimu mmoja tu na kisha kustaafu.
Scholes nusura ajiunge na Timu ya England iliyoko huko Afrika Kusini kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuombwa na Kocha wa England Fabio Capello afute uamuzi wa kustaafu kucheza Mechi za Kimataifa lakini akakataa ingawa baadae alikiri kama angeombwa mapema angekubali.
Veterani huyo amesema: “Ndio namaliza miaka yangu kwenye Soka na ntacheza Mwaka mmoja zaidi. Nimeanza kuchukua Beji za Ukocha na siku moja ntafundisha Watoto au Timu. “
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, bado ana imani Scholes kiwango na uwezo upo wa kuendelea kucheza kwa muda mrefu.
Akionyesha shukrani zake kwa Ferguson kumlea tangu utoto kwenye maisha yake ya Soka, Scholes amenena: “Ferguson ni Mtu Bora kabisa! Bila ya kutamka, yeye ni Meneja Bora na mzuri sana! Amewaendeleza Chipukizi wengi na anatoa matumaini kwa kila Kijana kwenye Timu zao kuwa wakiwa wazuri watapewa nafasi. Ni mtu muhimu sana kwenye maisha yangu.”
CHEKI: www.sokainbongo.com

Beckenbaauer achochea uhasama England na Germany
Franz Beckenbauer ameiponda England na kuwaita wapumbavu kwa kushindwa kumaliza Kundi lao wakiwa vinara na hivyo kukwepa kucheza na Germany Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.
England walimaliza Kundi C wakiwa nafasi ya pili nyuma ya USA ambao watacheza na Ghana.
Beckenbauer, aliekuwa akiitwa ‘Der Kaiser’ enzi zaki akichezea Germany, amesema anaamini pambano la England v Germany halipaswi kuchezwa Raundi ya Pili na badala yake lingefaa kabisa kuwa Fainali.
Katika Fainali za Kombe la Dunia, England na Germany zimewahi kukutana mara 3 zikiwa ni Fainali Mwaka 1966 ambayo England waliifunga Germany 4-2 na kutwaa Ubingwa wa Dunia, na mara nyingine ni Robo Fainali Mwaka 1970 na Nusu Fainali Mwaka 1990.
Akizidi kutia utambi, Beckenbauer amesema Wachezaji wa England ni wachovu kwa kushindwa kuzifunga USA na Algeria.
Beckenbauer amesema: “Gemu ya England v Germany haifai kuwa ya Raundi ya Pili. Ni gemu kubwa sana na haisahauliki kwenye historia! Huu ni upumbavu wa England kwa kumaliza wa pili kwenye Kundi lao!”
CHEKI: www.sokainbongo.com

Bia zawatia stimu England!!
Wachezaji wa England waliruhusiwa kunywa bia katika mkesha wa Siku ambayo walitakiwa kucheza mechi muhimu na Slovenia ambayo ilibidi washinde ili kusonga mbele Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.
Hilo limethibitishwa na Kocha wa England, Fabio Capello, ambae alisema: “Tuliwaruhusu wanywe Bia. Na kweli siku ya pili Timu ilibadilika na ile ari yao ya zamani ilirudi tena! Walicheza vizuri na kujituma sana kupita mechi za USA na Algeria!”
England iliifunga Slovenia 1-0 na kutinga Raundi ya Pili kucheza na Germany Jumapili Juni 27
CHEKI: www.sokainbongo.com

RAUNDI YA PILI: Germany v England!!
Ghana yafungwa, yatinga Raundi ya Pili!
Ghana imefungwa na Ujerumani bao 1-0 lakini imeitoa kimasomaso Afrika kwa kutinga Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia na itakutana na USA kwenye Raundi hiyo Jumamosi Juni 26.
Bao la Ujerumani lilifungwa kipindi cha pili na Mezut Ozil dakika ya 60.
Utamu mwingine wa pambano hili ni kwa Ndugu wawili kuwa Timu tofauti kwa Jerome Boateng kuichezea Ujerumani na Kevin-Prince Boateng kucheza Ghana, Nchi ambayo Baba yake alitoka.
Ujerumani itakutana na Watani zake wa Jadi, England, kwenye Raundi ya Pili.
Australia 2 Serbia 1
Australia wameitwanga Serbia bao 2-1 na kuhakikisha Nchi zote mbili zinarudi kwao mapema baada ya Ghana na Ujerumani kufuzu kwenye Kundi lao.
Mabao ya Australia yalifungwa na Tim Cahill, alierudi Uwanjani leo baada ya kukosa mechi moja kwa kutumia kifungo alipopewa Kadi Nyekundu ya uonevu katika mechi ya kwanza dhidi ya Ujerumani, na la pili na Holman.
Bao la Serbia alipachika Pantelic.
RAUNDI YA PILI: MTOANO TIMU 16 yaanza kukamilika!!
Jumamosi Juni 26
Saa 11 jioni:
URUGUAY v SOUTH KOREA
Nelson Mandela, Port Elizabeth
Saa 3.30 usiku:
USA v GHANA
Royal Bafokeng, Rustenburg
Jumapili Juni 27
Saa 11 jioni:
GERMANY v ENGLAND
Free State, Bloemfontein
Saa 3.30 usiku:
ARGENTINA v MEXICO
Soccer City, Soweto

Wednesday, 23 June 2010

FIKA: www.sokainbongo.com

Okocha alia, alaumu Afrika kwa uzembe!
Jay-Jay Okocha, Supastaa wa zamani wa Nigeria, amelalamika kuwa Soka la Afrika haliwezi kufanikiwa mpaka Watu wakae chini na kutafakari upya nini kifanyike ili tufanikiwe katika Fainali za Makombe ya Dunia yajayo.
Okocha, Miaka 36, ambae aliwahi kuwa Mchezaji Ligi Kuu England akiwa na Bolton Wanderers na kisha Hull City, amedai Afrika tunatumia njia za mkato za kujitayarisha na Mashindano yaliyo mbele yetu badala ya kuwekeza katika kutafuta, kukuza na kuendeleza vipaji vya Watoto na Wachezaji chipukizi.
Pia, amesema hatufanyi jitihada za kutosha za kuwaendeleza Makocha Wazalendo.
Okocha akawageukia Masupastaa wa leo wa Afrika wanaochezea Nchi zao huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia na kudai hawajaonyesha moyo thabiti wa kuchezea Nchi zao kama wanavyofanya wakiwa na Klabu zao huko Ulaya.
Okocha alilalama: “Hii ni hulka ya mtu. Wachezaji wetu hawakuonyesha ari ya kutosha. Haya Mashindano yako Afrika na tulidhani tutanufaika lakini sivyo!”
Mbali ya kubwagwa nje Cameroun, Algeria, Nigeria na Afrika Kusini, wakiwa Wenyeji wa kwanza wa Fainali za Kombe la Dunia kubwagwa nje Raundi ya Kwanza tu, tumebakiwa na Ivory Coast, wenye nafasi finyu, na Ghana pekee ndio kidogo wamegangamala.
Okocha alimaliza kwa kusema kwa msisitizo Afrika ni lazima ijifunze toka Ligi za juu za huko Ulaya na Watu wawe na nidhamu ya kuendesha Soka kitaaluma na sio kwa kulipua na ubabaishaji.
PITIA: www.sokainbongo.com

KOMBE LA DUNIA:
Kimbembe cha Kesho cha kuingia Raundi ya 2
KUNDI E:
Msimamo:
-Holland pointi 6
-Japan pointi 3
-Denmark pointi 3
-Cameroun pointi 0
Mechi: Holland v Cameroun na Denmark v Japan
Holland tayari wako Raundi ya Pili na watajihakikishia kuwa vinara wa Kundi ikiwa hawatafungwa na Cameroun ambayo tayari ishaaga Kombe la Dunia.
Japan, wasipofungwa na Denmark, wataungana na Holland kusonga Raundi ya Pili.
Denmark lazima waifunge Japan ili watinge Raundi ijayo.
KUNDI F:
Msimamo:
-Paraguay pointi 4
-Italy pointi 2
-New Zealand pointi 2
-Slovakia pointi 1
Mechi: Slovakia v Italy na Paraguay v New Zealand
Kundi hili linahitaji mahesabu kidogo.
Paraguay wanahitaji sare tu dhidi ya New Zealand ili watinge Raundi ya Pili lakini New Zealand wakishinda wao ndio watasonga ingawa Paraguay wanaweza kusonga kutegemea na matokeo ya mechi nyingine ya Slovakia v Italy.
Italy lazima wawafunge Slovakia lakini sare inaweza kuwa sawa kwao ikiwa New Zealand watafungwa na Paraguay.
Ikiwa Slovakia wataifunga Italy wanaweza wakapenya ikiwa tu New Zealand wataifunga Paraguay na tofauti ya magoli itawasaidia.
Ni chemsha bongo hii!!
CHEKI: http://www.sokainbongo.com/

England yapenya, USA yajipenyeza Raundi ya Pili!!!
England ilitakiwa ishinde mechi yake na Slovenia ili wafuzu kuingia Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia na alikuwa ni Jermaine Defoe ndie aliewabeba kwa kufunga bao moja na la ushindi katika mechi iliyochezwa leo Jumatano Juni 23 huko Uwanja wa Nelson Mandela, Port Elizabeth.
Bao la ushindi la Defoe lilipatikana dakika ya 23 baada ya krosi tamu ya James Milner kukutwa na Defoe alieunganisha.
Kwa ushindi huo England imepata pointi 5 sawa na USA lakini USA, aliemfunga Algeria 1-0 pia leo, amefunga bao zaidi ya England na hivyo kuchukua uongozi wa Kundi C.
USA watacheza na Mshindi wa Pili wa Kundi D na England atacheza na Mshindi wa Kundi D.
Kundi D ni Ghana, Germany, Serbia na Australia.
Timu;
England: 1-David James; 2-Glen Johnson, 15-Matthew Upson, 6-John Terry, 3-Ashley Cole; 16-James Milner, 4-Steven Gerrard, 8-Frank Lampard, 14-Gareth Barry; 19-Jermain Defoe, 10-Wayne Rooney.
Slovenia: 1-Samir Handanovic; 2-Miso Brecko, 4-Marko Suler, 5-Bostjan Cesar, 13-Bojan Jokic; 10-Valter Birsa, 8-Robert Koren, 18-Aleksandar Radosavljevic, 17-Andraz Kirm; 9-Zlatan Ljubijankic, 11-Milivoje Novakovic.
Refa: Wolfgang Stark (Germany)
USA 1 Algeria 0
Dakika 90 ziliyoyoma na USA aliekuwa kabanwa mbavu na Algeria kwa kuwa sare 0-0 alikuwa ndio anaelekea nje ya Kombe la Dunia huku Slovenia ingawa alikuwa kafungwa na England 1-0 ndie alikuwa anasonga mbele lakini katika dakika ya kwanza tu ya dakika 4 za nyongeza USA wakafunga bao na kuwapiku Slovenia na pia kuwa ndio vinara wa Kundi C.
Goli hilo la dakika ya 91 lilifungwa na Landon Donovan kufuatia kaunta ataki na Altidore kumpenyezea Dempsey ambae shuti lake liliokolewa na Kipa wa Algeria Mbouli na kutua kwa Donovan alieuvurumisha mpira wavuni.
Katika Raundi ya Pili, USA watacheza na Mshindi wa Pili wa Kundi D ambae ni ama Ghana, Germany, Serbia au Australia.
Timu:
USA Tim Howard; Steve Cherundolo, Jay DeMerit, Jonathan Bornstein, Carlos Bocanegra; Landon Donovan, Michael Bradley, Maurice Edu, Clint Dempsey; Jozy Altidore, Hercules Gomez.
Algeria Rais Ouheb Mbouli; Majid Bougherra, Rafik Halliche, Antar Yahia, Nader Belhadj, Fouad Kadir, Hassan Yebda, Medhi Lacen, Karim Ziani, Rafik Djebbour, Karim Matmour.
Refa: Frank De Bleeckere (Belgium
CHEKI: www.sokainbongo.com

Man United yatoa nje kwa Cole
Manchester United wametangaza kuwa hawana nia ya kumchukua Joe Cole ambae sasa ni Mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake na Chelsea mwanzoni mwa Mwezi Juni.
Afisa wa ngazi za juu wa Man United amethibitisha kuwa hawana nia ya kumchukua Joe Cole, Miaka 28, ingawa kulikuwa na habari nyingi za kumhusisha na Old Trafford.
Klabu nyingine ambazo zinadaiwa zina nia ya kumchukua Cole ni Arsenal na Tottenham.
Cole kwa sasa yuko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia pamoja na Kikosi cha England.
Cole alianza Soka lake huko West Ham kisha akahamia Chelsea Mwaka 2003 ambako amecheza mechi 396 na kuifungia Chelsea bao 52.
KOMBE LA DUNIA:
RATIBA-Alhamisi Juni 24
[saa za bongo]
Saa 11 jioni: KUNDI F
Paraguay v New Zealand Peter Mokaba, Polokwane
Slovokia v Italy Ellis Park, Johannesburg
Saa 3.30 usiku: KUNDI E
Denmark v Japan Royal Bafokeng, Rustenburg
Cameroun v Netherlands Green Point, Cape Town
Villa kupona rungu la FIFA
FIFA imethibitisha kuwa David Villa wa Spain hatachukuliwa hatua yeyote baada ya kunaswa na kamera akimpiga Beki wa Honduras Emilio Izaguirre tukio ambalo Refa toka Japan Yuichi Nishimura hakuliona.
Villa ndie alieifungia Spain bao zote mbili dhidi ya Honduras na pia alikosa penalti kwa kuipiga nje.
Msemaje wa FIFA amesema wamelichunguza tukio la Villa na hamna msingi wowote wa kufungua kesi.
Hivyo Villa yuko huru kucheza mechi ya mwisho ya Spain ya Kundi H watakapocheza na Chile ijumaa Juni 25.

Tuesday, 22 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Ni Argentina v Mexico & Uruguay v South Korea Raundi ya Pili!
-Nigeria NJE!!!
Katika mechi za leo Jumanne Juni 22, Argentina na Korea Korea Kusini zimetinga Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia na Argentina watacheza na Mexico na Korea Kusini wataivaa Uruguay katika Raundi hiyo.
Argentina waliibwaga Ugiriki kwa bao 2-0 kwa bao za Kipindi cha Pili zilizofungwa na Demichelis na Palermo.
South Korea walitoka sare na Nigeria ya goli 2-2.
Mabao ya Nigeria yamefungwa na Uche na Yakubu, kwa penalti.
South Korea walipata bao zao toka kwa Lii Jung-Soo na Park Chu-Young.
Kwa Afrika, Nigeria imeungana na Wenyeji Afrika Kusini na Cameroun kuwa nje ya Kombe la Dunia na kuwabakisha Ghana, Algeria na Ivory Coast huku Ghana ikiwa pekee ndio yenye nafasi kubwa kuingia Raundi inayofuata.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Kesho Terry uso kwa uso na Refa aliemsema hana adabu
Beki wa England, John Terry, kesho Jumatano Juni 23 England watakapocheza na Slovenia atakumbana na Refa kutoka Ujerumani Wolfgang Stark ambae alimlaumu kwa kutomwonyeshea heshima Mwezi Machi Klabu yake Chelsea ilipotolewa na Inter Milan Uwanjani Stamford Bridge kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI.
Wakati huo Terry alikasirishwa na Refa Wolfgang Stark kukataa kumsikiliza Terry alipokuwa akimfuata Uwanjani wakati wa mechi ili kutaka maelezo ya maamuzi ya Refa huyo lakini kila mara alikataa kumsikiliza na baada ya mechi Terry akalalamika: “Mie kama Kepteni nilikwenda kuongea nae lakini akakataa akanipa mgongo. Hakutaka kuongea na mimi. Hilo ni kutokuwa na heshima!”
Mechi hii ya England v Slovenia ni muhimu kwa England ambao ni lazima washinde ili wasonge Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.
Refa Wolfgang Stark ameshawahi kuichezesha England mara 3 na zote England wameshinda.
Kwa John Terry hii ni wiki ya balaa kwake kwa vile pia amejikuta yuko kwenye mgogoro na Kocha wake Fabio Capello.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Uruguay na Mexico ZAFUZU, Bafana na Ufaransa NJE!!!
Wenyeji wa Kombe la Dunia, Afrika Kusini, licha wa kuifunga Ufaransa goigoi kwa bao 2-1 wametupwa nje ya Mashindano hayo kwa tofauti ya magoli na kuiruhusu Mexico kusonga mbele licha ya kufungwa bao 1-0.
Mechi zote hizi mbili zimechezwa leo Jumanne Juni 22 kwa wakati mmoja Afrika Kusini v Ufaransa ikichezwa huko Uwanja wa Free State Mjini Blomfentein na Uruguay v Mexico ikiwa Royal Bafokeng, Rustenburg.
Afrika Kusini walipata mabao yao kupitia Bongani Khumalo dakika ya 20 na Mphela dakika ya 37.
Ufaransa walipata pigo dakika ya 26baada ya Mchezaji wao Gourcuff kupewa Kadi Nyekundu kwa kumpiga kipepsi Sibaya.
Kwenye mechi ya Uruguay v Mexico, Uruguay walipata bao lao la ushindi dakika ya 43 kupitia Suarez.
Uruguay ndie ameshika uongozi wa Kundi A na atacheza mechi yake ya Raundi ya Pili ya Mtoano hapo Juni 26 dhidi ya Mshindi wa Pili kundi B.
Mexico wameshika nafasi ya Pili Kundi A na watapambana na Mshindi wa Kwanza Kundi B hapo Juni 27 na uwezekano mkubwa mpinzani wake atakuwa Argentina.
CHEKI: www.sokainbongo.com

KOMBE LA DUNIA:
RATIBA-Jumatano Juni 23
Saa 11 jioni: KUNDI C
Slovenia v England Nelson Mandela, Port Elizabeth
USA v Algeria Loftus Versfed, Pretoria
Saa 3.30 usiku: KUNDI D
Ghana v Germany Soccer City, Soweto, Johannesburg
Australia v Serbia Mbombela, Nelspruit
PATASHIKA YA KUINGIA RAUNDI YA PILI: Makundi C & D wacheza mechi za mwisho kesho Jumatano Juni 23
KUNDI C:
Msimamo:
-Slovenia pointi 4
-USA pointi 2
-England pointi 2
-Algeria pointi 1
Mechi: Slovenia v England na Algeria v USA
Slovenia wanahitaji sare na England ili wafuzu kuingia Raundi ya Pili lakini wanaweza pia kufuzu hata kama wakifungwa endapo USA na Algeria zitatoka sare.
England lazima washinde ili wasonge mbele.
Ikiwa England na USA watatoka sare katika mechi zao, tofauti ya magoli itahesabiwa ili kumpata Mshindi atakaeungana na Slovenia kutinga Raundi ya Pili na ikiwa hata magoli ni sawa basi itapigwa kura ili kuamua nani ataendelea.
Algeria watasonga mbele tu iwapo wataifunga USA kwa zaidi ya bao mbili.
Hakika ni hesabu kali mno.
KUNDI D:
Msimamo:
- Ghana pointi 4
-Germany pointi 3
-Serbia pointi 3
-Australia pointi 1
Mechi: Ghana v Germany na Serbia v Australia
Ghana na Ujerumani zitaingia Raundi ya Pili zikitoka sare kwenye mechi yao na Serbia wakitoka sare na Australia.
Ushindi kwa Ujerumani au Ghana na Serbia una maana Timu hizo zitasonga mbele.
Lakini Serbia wanaweza kufuzu hata wakitoka droo ikiwa tu Ujerumani itaifunga Ghana kwa zaidi ya bao moja au Ghana ikiifunga Ujerumani.
Australia wanahitaji waifunge Serbia ushindi mnono huku wakiomba mechi nyingine ya Ghana v Ujerumani inaisha sare au Timu moja inafungwa vibaya sana.
Haya ni mahesabu magumu mno.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Sokomoko kambi ya England: Bifu Capello na Terry
Kufuatia mwendo wa kusuasua katika mechi zao mbili za awali ambazo zote wametoka sare na sasa inabidi waifunge Slovenia katika mechi yao ya mwisho ikiwa watataka kufuzu kuingia Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia, kumezuka mtafaruku mkubwa ndani ya Kambi ya England baada ya kwanza Nahodha wa zamani John Terry kujitokeza na kudai Wachezaji hawafurahii jinsi Timu inavyoendeshwa na Capello, kisha akatokea Capello mwenyewe akijibu mapigo na kusema Terry amefanya kosa kubwa kutoa madai yake.
England ilianza kampeni yake kwa sare na USA ya bao 1-1 kisha droo ya 0-0 na Algeria.
Kocha Fabio Capello amesema siku zote mlango wake uko wazi kwa Mchezaji yeyote kuongea nae na ameshangazwa na kauli za Terry kwenye kadamnasi.
Terry ndie alikuwa Nahodha wa kwanza chini ya Capello lakini alitimuliwa baada ya kupatwa na skandali ya kutembea na Gelfrendi wa Mchezaji mwenzake Wayne Bridge.
Hata hivyo, John Terry amejitokeza na kuomba msamaha kwa kusema kauli zake zilikuwa ni kutaka kufafanua ukweli na hakuwa na nia ya kumponda Capello.
Ingawa inaaminika Terry atacheza mechi hiyo ya mwisho ya Kundi C na Slovenia hapo Jumatano Juni 23 lakini inaonekana siku zake kuichezea England chini ya mamlaka ya Capello zimeanza kuhesabika.
Spain 2 Honduras 0
FIFA wasubiri ripoti ya Refa kuhusu Villa
Ingawa Spain jana Jumatatu Juni 21 waliifunga Honduras 2-0 na hivyo kujiongezea matumaini ya kuingia Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia huenda Straika wao wa kutumainiwa David Villa akawa matatani ikiwa Refa wa pambano hilo Yuichi Nishimura ataamua achukuliwe hatua kwa kosa la kumpiga Beki wa Honduras Emilio Izaguirre.
Villa alimpiga Beki huyo wakati wakisubiri frikiki ipigwe lakini Refa hakuchukuwa hatua yeyote wakati huo na sasa ataonyeshwa video ya tukio na atatakiwa aamue hatua ipi angechukua kama angeliliona tukio hilo.
Katika mechi hiyo, David Villa ndie aliefunga bao 2 za Spain na pia kukosa penalti aliyoipiga nje.

Monday, 21 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

KOMBE LA DUNIA:
PATASHIKA KUINGIA RAUNDI YA PILI: Makundi A & B wacheza mechi za mwisho kesho Jumanne Juni 22
KUNDI A:
Msimamo:
-Uruguay pointi 4
-Mexico pointi 4
-France pointi 1
-South Africa pointi 1
Mechi za mwisho za Kundi hili ni Uruguay v Mexico na France v South Africa.
Uruguay na Mexico zinataka suluhu tu ili zitinge Raundi ya Pili na hilo limeleta minong’ono ya pengine Timu hizo zitafanya njama ya kuipata hiyo sare ili wote wasonge mbele.
Kwa Ufaransa na Bafana Bafana hamna njia ya mkato.
Ni lazima kila mmoja ashinde mechi yake na kisha aombe Mungu mechi ya Mexico v Uruguay imalizike kwa mmoja kufungwa.
Lakini hata maombi hayo pengine yasiwe yanatosha kwani vilevile ni lazima ushindi wa Ufaransa au Afrika Kusini uwe na magoli mazuri ili kuzipiku Mexico na Uruguay.
Ni kimbembe.
KUNDI B:
Msimamo:
-Argentina pointi 6
-South Korea pointi 3
-Nigeria pointi 1
-Greece pointi 1
Argentina tayari yuko Raundi ya Pili.
Kimbembe ni nani kati ya South Korea, Nigeria au Ugiriki ataungana na Argentina kutoka Kundi hili kwenda Raundi ya Pili.
Mechi za mwisho ni Argentina v Greece na Nigeria v South Korea.
Kwa Korea Kusini hata sare inaweza kuwasaidia ikiwa tu Ugiriki itatoka sare au kufungwa na Argentina.
Kwa kila hali, kwa South Korea, Nigeria na Ugiriki, ushindi ni kitu cha kwanza muhimu na mengine baadae.
Muntari aonywa na Ghana FA
Kiungo Sulley Muntari almanusura afungishwe virago toka huko Afrika Kusini ambako yuko na Ghana kwenye Kombe la Dunia lakini akapona kwa kupewa onyo kali na Chama cha Soka cha Ghana baada ya kukwaruzana na Kocha wa Ghana Milovan Rajevac anaetoka Serbia.
Muntari amekuwa hana rekodi nzuri na Timu ya Ghana na mara nyingi amekuwa akikwaruzana na Uongozi na visa kama hivyo vilimfanya asichukuliwe kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko Angola mapema Mwaka huu.
Ghana ndio wanaoongoza Kundi D na wanacheza mechi ya mwisho Jumatano na Ujerumani na sare tu itawatosha kutinga Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Maradona amshangaa Refa mechi ya Brazil
Diego Maradona amelielezea goli la pili la Brazil alilofunga Luis Fabiano dhidi ya Ivory Coast katika ushindi wa 3-1 kuwa la ‘mikono dabo’ na pia ilimstua kumwona Refa Stephane Lannoy kutoka Ufaransa akicheka na Luis Fabiano mara baada ya goli hilo.
Maradona, ambae ni Kocha wa Argentina, aliwahi kufunga goli kwa mkono katika Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 1986 huko Mexico Argentina ilipocheza na England na akaliita goli hilo kuwa ni goli la ‘mkono wa Mungu’ ameonyesha kushangazwa na goli la Fabiano na pia kitendo cha Refa huyo akicheka na Fabiano mara baada ya goli hilo.
UEFA yatoa Ratiba ya Raundi za Mtoano za Awali za UEFA CHAMPIONS LIGI
UEFA imetangaza Ratiba ya Raundi mbili za awali za Mtoano wa UEFA CHAMPIONS LIGI ambazo hushirikisha Timu ndogo.
Ratiba hiyo ni:
Raundi ya Kwanza ya Mtoano [Juni 29/30 na marudio Julai 6/7]
Tre Fiori v Rudar
Santa Coloma v Birkirkara
Raundi ya Pili ya Mtoano [Julai 13/14 na marudio Julai 20/21]
Liepajas Metalurgs v Sparta Prague
Aktobe v Olimpi Rustavi
Levadia Tallinn v Debrecen
Partizan Belgrade v Pyunik
Inter Baku v Lech Poznan
Dinamo Zagreb v Koper
Liteks Lovetch v Tre Fiori/Rudar
Santa Coloma/Birkirkara v MSK Zilina
FC Sheriff v Dinamo Tirana
Hapoel Tel-Aviv v Zeljeznicar
Omonia Nicosia v Renova
Red Bull Salzburg v HB
Bohemians v TNS
BATE v FH
AIK v Jeunesse Esch
Linfield v Rosenborg
Ekranas v HJK Helsinki
CHEKI: www.sokainbongo.com

Ureno 7 Korea Kaskazini 0
Ureno imejipa matumaini makubwa ya kuungana na Brazil kucheza Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia walipoibamiza Korea Kaskazini kwa mabao 7-0 katika mechi ya Kundi G iliyochezwa Green Point huko Cape Town.
Hadi mapumziko, Ureno walikuwa mbele kwa bao 1-0 alilofunga Raul Meireles.
Kipindi cha Pili Ureno walicharuka na ndani ya dakika 7 waliongeza mabao kupitia Simao, Hugo Almeida na Tiago.
Baadae Liedson, Ronaldo na Tiago waliongeza mabao mengine.
Katika Kundi hili Brazil wanaongoza wakiwa na Pointi 6, Ureno Pointi 4, Ivory Coast moja na Korea Kaskazini hawana pointi.
Mechi za mwisho ni Brazil v Ureno na Ivory Coast v Korea Kaskazini.
Chile 1 Uswisi 0
Chile wamefanikiwa kujikita kwenye kilele cha Kundi H walipoifunga Uswisi 1-0 huku Uswisi ikicheza Mtu 10 kwa zaidi ya Saa nzima kufuatia Kadi Nyekundu kwa Behrami.
Hadi mapumziko ngoma ilikuwa 0-0.
Kwenye dakika ya 75 Paredes wa Chile aliiua ofsaidi triki ya Uswisi na kupokea pasi nzuri toka kwa Valdivar kasha akampelekea Gonzalez aliefunga kwa kichwa.
Chile wanaongoza Kundi H wakiwa na pointi 6 na wanafuata Uswisi wenye 3.
Mechi inayofuata baadae leo ya Kundi hili ni kati ya Spain na Honduras.
Timu:
Chile:-Claudio Bravo; Mauricio Isla, Waldo Ponce, Arturo Vidal; Gary Medel, Carlos Carmona, Gonzalo Jara; Matias Fernandez; Alexis Sanchez, Humberto Suazo, Jean Beausejour.
Switzerland: Diego Benaglio; Stephan Lichtsteiner, Stephane Grichting, Steve Von Bergen, Reto Ziegler; Valon Behrami, Gokhan Inler, Benjamin Huggel, Gelson Fernandes; Alexander Frei, Blaise Nkufo.
Refa: Khalil Al-Ghamdi (Saudi Arabia)
Dunga aishangaa Kadi Nyekundu kwa Kaka
Kocha wa Brazil Dunga ameielezea Kadi Nyekundu aliyopewa Kaka katika mechi ya Jumapili Juni 20 Brazil walipoichapa Ivory Coast mabao 3-1 kuwa si haki.
Ushindi huo umeifanya Brazil itinge Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.
Dunga alilalamika: “Mchezaji aliecheza faulo anapewa Kadi ya Njano na asiekuwa na hatia Kadi Nyekundu!”
Kaka alipewa Kadi ya Pili ya Njano na hivyo kupata Kadi Nyekundu baada ya Kader Keita kumgonga Kaka na kudanganya amepigwa.
Dunga pia alilalamikia uchezeshaji wa Refa Stephane Lannoy kutoka Ufaransa kwa kutoa Kadi nyingi kwa Brazil wakati Ivory Coast ndio waliocheza rafu zaidi na nyingi zikiwa mbaya na za Kadi Nyekundu.

Sunday, 20 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Brazil yamgalagaza Drogba, yajikita Raundi ya Pili!!!
Ndani ya Soccer City, Soweto, Johannesburg, Brazil leo Jumapili Juni 20 waliweza kuifunga Ivory Coast mabao 3-1 na kujizolea Pointi 6 katika mechi mbili walizocheza na kutinga Raundi ya Pili huku wakiwa kileleni kwenye Kundi G wakisubiri mechi yao ya mwisho na Ureno.
Ureno Jumatatu Juni 21 watacheza na Korea Kaskazini huko Uwanja wa Green Point, Cape Town.
Tangu mpira uanze Ivory Coast walionekana kutulia na Brazil walianza polepole.
Ilipotimu katikati ya Kipindi cha kwanza, Brazil walipanda na mpira toka upande wao na walianza gonga safi toka nyuma na hatimae kuwashirikisha Felipe Melo, Kaka na Robinho na mwishowe mpira kupenyezwa kwa Luis Fabiano aliefumua shuti kali na kumpita Kipa Boubacar juu na kutinga wavuni hiyo ikiwa ni dakika ya 25.
Hadi mapumziko Brazil 1 Ivory Coast 0.
Dakika 5 tu baada ya Kipindi cha Pili kuanza, alikuwa Luis Fabiano tena akiwa katikati ya Madifenda watatu, na pengine kwa msaada wa mkono, aliukontroli mpira na kuwapita Mabeki hao na kukutana uso kwa uso na Kipa Boubacar na kwa mara ya pili akamshinda kwa kigongo kingine.
Dakika ya 62, kazi njema ya Kaka kwenye winga ya kushoto aliyoimaliza kwa pande maridadi kwa Elano aliefunga bao la 3 na hilo likiwa bao lake la pili katika mechi mbili.
Drogba aliipatia Ivory Coast bao lao moja huku Difensi ya Brazil ikizubaa wakidhani yuko ofsaidi lakini marudio yalionyesha lilikuwa bao safi.
Keita wa Ivory Coast alileta udanganyifu mkubwa alipojidai amepigwa na Kaka wakati si kweli na Refa Lannoy akadanganyika na kumpa Kaka Kadi ya Njano ya pili na hivyo kutolewa nje.
Timu:
Brazil : Julio Cesar; Maicon, Lucio, Juan, Michel Bastos; Felipe Melo, Gilberto Silva; Elano, Kaka, Robinho; Luis Fabiano.
Ivory Coast: Boubacar Barry; Emmanuel Eboue, Kolo Toure, Guy Demel, Siaka Tiene; Didier Zokora, Yaya Toure, Cheik Tiote; Salomon Kalou, Didier Drogba, Aruna Dindane.
Refa: Stephane Lannoy [France]
CHEKI: www.sokainbongo.com

Kuyt asikitika kuondoka Benitez Liverpool
Straika wa Liverpool Dirk Kuyt ambae yuko Afrika Kusini na Nchi yake Uholanzi ambayo tayari imefuzu kuingia Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia ameelezea kusikitishwa kwake kwa kuondoka aliekuwa Meneja wa Klabu hiyo Rafael Benitez.
Benitez tayari ameshajiunga na Inter Milan ya Italia.
Kuyt, aliesainiwa na Benitez toka Feyernoord Mwaka 2006, amesema: “Nimesikitika kwa kuondoka Benitez. Ni Meneja mzuri na namshkuru kwa kunipeleka Liverpool na kunifikisha hapa.”
Pia Kuyt amesema hataki kumwona Nahodha wake Steven Gerrard akihama kwani kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu hilo.
Kuyt ametamka: “Sitopenda Gerrard ahame. Yeye ni Nahodha wetu na ni muhimu kwetu. Yeye ana damu ya Liverpool. Akitaka kuondoka basi ofa hiyo itakuwa ni nzuri sana au ataenda Klabu bora sana.”
Kuyt amekiri kuwa huko Afrika Kusini wanaongea na Gerrard na wanatakiana heri kabla ya mechi.
Neville amtaka Capello asibebe Wachezaji wasiofaa!
Difenda wa zamani wa England ambae ni Nahodha wa Manchester United, Gary Neville, amemtaka Kocha Fabio Capello aache kuwabeba Wachezaji wasiofaa na kuwapanga Watu katika namba wazomudu vyema kila siku kwenye Klabu zao.
Neville, ambae ameichezea England mara 85 na ya mwisho ikiwa Februari 2007, pia ametaka Timu hiyo iachane na Mfumo wa 4-4-2 ambao ameusema ni wa kizamani.
Nahodha huyo wa Man United amesema ni bora Gerrard acheza mbele zaidi akiwa nyuma ya Wayne Rooney badala ya kuwekwa Kiungo pembeni kushoto kama alivyochezeshwa mechi na Algeria.
Neville alisema: “Nilishangaa kuona tunacheza 4-4-2 na Algeria! Rooney alionekana kukerwa na kutopata mipira na kutochezeshwa!”
Neville amemtaka Capello amchezesha Rooney kama Sentafowadi kama anavyocheza Man United na Gerrard achezeshwa nafasi ile ile anayocheza Liverpool, yaani nyuma tu ya Sentafowadi.
Gerrard huko Liverpool hucheza nyuma tu ya Straika wao Fernando Torres.
Aliongeza pia ikibidi kuubadili Mfumo ubadilishwe na Emile Heskey akae nje kumpisha Gerrard awe patna na Rooney mbele na pia ili Kiungo kuwe na Watu watatu.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Mabingwa wa Dunia Italy ulimi nje!!
Leo Jumapili Juni 20 huko Uwanja wa Mbombela, Nelspruit, Mabingwa wa Dunia Italia wameenda sare 1-1 na New Zealand, Timu ambayo wengi hawakuipa nafasi yeyote, lakini ilichachamaa vibaya.
Hii ni sare ya pili kwa Italia baada ya kutoka droo mechi ya kwanza na Paraguay na sasa watamaliza mechi iliyobaki kwa kucheza na Slovakia.
New Zealand watacheza na Paraguay ambao ndio wanaongoza Kundi hili wakiwa na pointi 4.
Katika mechi ya pili sasa, Mabingwa hao wa Dunia walijikuta wako nyuma kwa bao 1-0 dakika ya 7 baada ya frikiki ya Shane Elliot kuparazwa kichwa na Reid na kumgonga Nahodha wa Italia Cannavaro kifuani na kumkuta Mfungaji Smeltz alieudokoa kumpita Kipa Marchetti.
Italia walicharuka baada ya kufungwa na kuishambulia New Zealand mfululizo na hatimaye presha yao ilizaa penalti dakika ya 28 baada ya Beki Tommy Smith kumshika jezi De Rossi ingawa ilionekana De Rossi alijirusha kuitafuta hiyo penalti.
Iaquinta akamchambua Kipa Paston na kufanya ngoma iwe 1-1.
Licha ya kutawala mechi Kipindi cha Pili, Italia walishindwa kupata bao la pili na kuna wakati ‘kaunta ataki’ ya Ne Zealand nusura iwape bao la pili.
Timu:
Italy: 12-Federico Marchetti; 19-Gianluca Zambrotta, 5-Fabio Cannavaro, 4-Giorgio Chiellini, 3-Domenico Criscito; 15-Claudio Marchisio, 22-Riccardo Montolivo, 6-Daniele De Rossi, 7-Simone Pepe; 9-Vincenzo Iaquinta; 11-Alberto Gilardino.
New Zealand: 1-Mark Paston; 4-Winston Reid, 19-Tommy Smith, 6-Ryan Nelsen; 11-Leo Bertos, 5-Ivan Vicelich; 7-Simon Elliot, 3-Tony Lochhead; 9-Shane Smeltz; 10-Chris Killen, 14-Rory Fallon.
Refa: Carlos Batres (Guatemala)
Ufaransa yasambaratika!!!
Kuna taarifa kuwa Timu ya Ufaransa leo mchana ilishindwa kufanya mazoezi baada ya kuzuka zogo kati ya Mkufunzi wa Mazoezi ya Viungo na Kocha wa Ufaransa, Raymond Domenech, na Wachezaji wote wakaondoka Uwanjani na kuingia ndani ya Basi lao.
Baada ya hapo zikaibuka habari kuwa Mkurugenzi wa Timu, Jean-Loius Valentin amejiuzulu kwa hasira.
Balaa lote hili limezuka baada ya Straika Nicolas Anelka kutimuliwa kwenye Timu baada ya kugombana na Kocha Domenech.
Hata hivyo Domenech amedai Anelka alipewa nafasi ya kubaki kwenye Timu ikiwa ataomba radhi lakini alikataa.
Kaita atishiwa maisha baada ya Kadi Nyekundu
Kiungo wa Nigeria, Sani Kaita, ambae alitolewa kwa Kadi Nyekundu Siku ya Alhamisi Ugiriki ilipoifunga Nigeria 2-1 kwenye Kombe la Dunia ameshapokea vitisho vingi vya maisha yake.
Msemaje wa Timu ya Nigeria, Peterside Idah, amesema Kaita ameletewa zaidi ya barua pepe 1,000 zinazotishia maisha yake toka kwao Nigeria.
Mseamaje huyo ameongeza kuwa washatoa taarifa kwa Serikali ya Nigeria na FIFA kuhusu matukio hayo ya vitisho.
Kaita alipewa Kadi Nyekundu baada ya kumrushia teke Vassillis Torosidis wa Ugiriki dakika ya 33 huku Nigeria wakiongoza 1-0 lakini wkicheza pungufu wakafungwa 2-1 na sasa nafasi yao ya kuendelea Raundi ya Pili ni finyu na pia ni lazima waifunge Timu ngumu Korea ya Kusini katika mechi ya mwisho Siku ya Jumanne ili wawe na matumaini.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Sakata la Anelka
Kocha Raymond Domenech wa Ufaransa amejaribu kuzima sakata la Nikolas Anelka kutimuliwa toka Kikosi cha Ufaransa kilichopo huko Afrika Kusini kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa kusema kuwa Anelka angebaki kwenye Timu kama angekubali kuomba radhi.
Domenech alisema: “Niliongea na Anelka baadae na nikajaribu kumtaka aombe radhi lakini hakutaka.”
Domenech amedai sakata la Anelka lingemalizika ndani ya Timu lakini kwa bahati mbaya kuna Mtu akalivujisha Magazetini na likalipuka kupita ilivyotegemewa.
Wakati huohuo, Nahodha wa Anelka huko Chelsea, John Terry, amejitokeza kumtetea Anelka kwa kudai Viongozi wa Ufaransa wamekosea kumfukuza Anelka toka kwenye Timu.
Terry amedai: “Huwezi kupata Mtu bora kwenye Soka kama Anelka. Ni mtu mkimya mno na siku zote akitaka kuzungumza kitu ntamsikiliza. Ni kosa kumfukuza. Yeye ni Mchezaji bora!”
Domenech amekuwa Kocha wa Ufaransa kwa Miaka 6 sasa lakini utawala wake umekuwa ukigubikwa na matatizo mara kwa mara na kumfanya asipendwe huko kwao.
Baada ya Kombe la Dunia Domenech atang’atuka na nafasi yake kuchukuliwa na Kepteni wa zamani wa Ufaransa, Laurent Blanc aliewahi pia kuwa Mchezaji wa Manchester United kabla hajastaafu.
Msimu uliokwisha Blanc alikuwa Meneja wa Mabingwa wa zamani wa Ufaransa Bordeaux.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Cameroun baibai Kombe la Dunia
Cameroun jana Jumamosi Juni 19 ilitandikwa bao 2-1 na Denmark, baada ya kuongoza 1-0, na kuwa Nchi ya kwanza kutolewa nje ya Fainali za Kombe la Dunia 2010 na pia kuihakikishia Uholanzi kuwa Timu ya kwanza kuingia Raundi ya Pili.
Cameroun walitangulia kupata bao dakika ya 10 kupitia Nahodha wao Samuel Eto’o kufuatia kosa la Difensi ya Denmark.
Lakini Denmark hawakukata tama na Straika kutoka Arsenal, Nicklas Bendtner, alisawazisha dakika ya 33 kwa shuti kali baada ya pasi murua toka kwa Rommedahl.
Kipindi cha Pili, Denmark waliibuka vizuri na dakika ya 61 Rommedahl, akitumia juhudi binafsi, aliipa ushindi Denmark kwa bao safi.
Mechi ya mwisho, Denmark wataivaa Japan huko Royal Bafokeng, Rustenburg Siku ya Alhamisi kuamua nani wanaungana na Holland kucheza Raundi ya Pili.
Cameroon: 16-Hamidou Souleymanou; 19-Stephane Mbia, 5-Sebastien Bassong, 3-Nicolas Nkoulou, 2-Benoit Assou-Ekotto; 8-Geremi, 18-Enoh Eyong, 6-Alexandre Song, 10-Achille Emana; 15-Achille Webo, 9-Samuel Eto'o.
Denmark: 1-Thomas Sorensen; 15-Simon Poulsen, 4-Daniel Agger, 3-Simon Kjaer, 6-Lars Jacobsen; 19-Dennis Rommedahl, 2-Christian Poulsen, 10-Martin Jorgensen, 8-Jesper Gronkjaer; 9-Jon Dahl Tomasson, 11-Nicklas Bendtner.
Refa: Jorge Larrionda [Uruguay]
CHEKI: www.sokainbongo.com

RAUNDI YA PILI YA MTOANO TIMU 16 kuanza Kesho!!
Timu 16 zitakazocheza Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini zitakamilika baada ya Kundi la mwisho Kundi H, lenye Timu za Chile, Spain, Uswisi na Honduras, kumaliza mechi zao leo usiku Ijumaa Juni 25.
Mechi za Raundi hii ya Pili zinanaanza Jumamosi Juni 26.
Ratiba ya Jumamosi Juni 26
Saa 11 jioni:
URUGUAY v SOUTH KOREA
Nelson Mandela, Port Elizabeth
Saa 3.30 usiku:
2] USA v GHANA
Royal Bafokeng, Rustenburg
TATHMINI:
Uruguay v South Korea
Uruguay walifuzu kuingia Raundi hii baada ya kutwaa uongozi wa Kundi A waliposhinda mechi mbili na kutoka sare moja.
South Korea, wakiongozwa na Nahodha Park Ji-Sung toka Manchester United, wametoka Kundi B ambako walishinda mechi moja, sare moja na kufungwa moja.
Timu hizi zimewahi kukutana mara 4 hapo nyuma na Uruguay wameshinda mechi 3 na sare moja.
Huko Afrika Kusini, Uruguay walitoka sare na Ufaransa na kuzitungua Bafana Bafana na Mexico.
Korea walishinda mechi ya kwanza dhidi ya Ugiriki, wakafungwa na Argentina na kutoka sare na Nigeria.
Mshindi wa mechi hii atakutana na Mshindi wa mechi kati ya USA v Ghana kwenye Robo Fainali.
Wakati Korea hupenda kutumia fomesheni ya 4-4-2 huku Park Ji-Sung na Lee Chung-yong wakileta moto toka kwenye Winga, Uruguay hupenda kutumia 4-3-3 inayoongozwa na Washambuliaji Edinson Cavani wa Klabu ya Palermo, Italia na Luis Suarez na Diego Forlan.
USA v Ghana
Meneja wa USA, Bob Bradley, ambae mwanawe Michael Bradley ni mmoja wa Wachezaji shupavu wa USA, ana imani ya hali ya juu na Timu yake akiamini itafika Fainali hapo Julai 11.
USA walimaliza Kundi C wakiwa sawa na England kwa pointi 5 kila mmoja lakini waliukwaa uongozi kwa kufunga goli nyingi.
Ghana walimaliza Kundi D nyuma ya Germany na ndio Timu pekee toka Afrika iliyobaki kwenye Mashindano haya makubwa yanayofanyika Afrika kwa mara ya kwanza.
Bradley ameizungumza Ghana: “Timu hii Ghana chini ya Kocha Milovan Rajevac ni nzuri sana! Wametulia, wana vipaji na pia wana nguvu!”
Wakati USA watawategemea sana Altidore, Clint Dempsey na Landon Donovan, Ghana wapo kina Asamoah Gwyan, Ayew [Mtoto wa Abedi Pele], Mensah na Kipa Kingston ambae ni imara mno.
Powered By Blogger