Sunday 20 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Kuyt asikitika kuondoka Benitez Liverpool
Straika wa Liverpool Dirk Kuyt ambae yuko Afrika Kusini na Nchi yake Uholanzi ambayo tayari imefuzu kuingia Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia ameelezea kusikitishwa kwake kwa kuondoka aliekuwa Meneja wa Klabu hiyo Rafael Benitez.
Benitez tayari ameshajiunga na Inter Milan ya Italia.
Kuyt, aliesainiwa na Benitez toka Feyernoord Mwaka 2006, amesema: “Nimesikitika kwa kuondoka Benitez. Ni Meneja mzuri na namshkuru kwa kunipeleka Liverpool na kunifikisha hapa.”
Pia Kuyt amesema hataki kumwona Nahodha wake Steven Gerrard akihama kwani kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu hilo.
Kuyt ametamka: “Sitopenda Gerrard ahame. Yeye ni Nahodha wetu na ni muhimu kwetu. Yeye ana damu ya Liverpool. Akitaka kuondoka basi ofa hiyo itakuwa ni nzuri sana au ataenda Klabu bora sana.”
Kuyt amekiri kuwa huko Afrika Kusini wanaongea na Gerrard na wanatakiana heri kabla ya mechi.
Neville amtaka Capello asibebe Wachezaji wasiofaa!
Difenda wa zamani wa England ambae ni Nahodha wa Manchester United, Gary Neville, amemtaka Kocha Fabio Capello aache kuwabeba Wachezaji wasiofaa na kuwapanga Watu katika namba wazomudu vyema kila siku kwenye Klabu zao.
Neville, ambae ameichezea England mara 85 na ya mwisho ikiwa Februari 2007, pia ametaka Timu hiyo iachane na Mfumo wa 4-4-2 ambao ameusema ni wa kizamani.
Nahodha huyo wa Man United amesema ni bora Gerrard acheza mbele zaidi akiwa nyuma ya Wayne Rooney badala ya kuwekwa Kiungo pembeni kushoto kama alivyochezeshwa mechi na Algeria.
Neville alisema: “Nilishangaa kuona tunacheza 4-4-2 na Algeria! Rooney alionekana kukerwa na kutopata mipira na kutochezeshwa!”
Neville amemtaka Capello amchezesha Rooney kama Sentafowadi kama anavyocheza Man United na Gerrard achezeshwa nafasi ile ile anayocheza Liverpool, yaani nyuma tu ya Sentafowadi.
Gerrard huko Liverpool hucheza nyuma tu ya Straika wao Fernando Torres.
Aliongeza pia ikibidi kuubadili Mfumo ubadilishwe na Emile Heskey akae nje kumpisha Gerrard awe patna na Rooney mbele na pia ili Kiungo kuwe na Watu watatu.

No comments:

Powered By Blogger