Saturday 26 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

RATIBA: Jumapili, Juni 27
Saa 11 jioni: Uwanja Free State, Bloemfontein
England v Germany
Katika historia England na Germany zimeshakutana mara 31 na England wameshinda mechi 15, Germany mara 10, na sare 6.
England, chini ya Fabio Capello, imeshawahi kuifunga Germany bao 2-1 walipokutana Novemba 2008 Uwanja wa Olimpiki huko Berlin, Ujerumani.
Timu hizi mbili ni Mahasimu wakubwa na hii itakuwa mara ya 3 kukutana kwenye Mashindano makubwa katika Miaka 20 iliyopita.
Kwenye Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 1990 huko Italia na EURO 96, Germany iliibwaga England kwa penalti kwenye hatua ya Nusu Fainali.
Kwenye Fainali hizi huko Afrika Kusini, Germany walianza kwa kutisha walipoidunda Australia 4-0 lakini nao wakatwangwa 1-0 na Serbia kisha wakaifunga Ghana 1-0 kwa mbinde na kufuzu kuingia Raundi ya Pili.
England walianza kwa kusuasua kwenye Kundi lao kwa kupata sare za 1-1 na USA na 0-0 na Algeria na ikabidi waifunge Slovenia ili wafuzu na kweli walishinda 1-0.
Lakini, kwa ujumla, kiwango cha England kipo chini.
Wakati England hawana majeruhi kambini mwao, Germany inasemekana wana majeruhi wakiwemo Cacau, Bastian Schweinsteiger, Jerome Boateng, Mesut Ozil na Miroslav Klose ingawa baadhi wanategemewa kucheza.
Timu:
England: David James, Johnson, Ashley Cole, Terry, Upson, Barry, Lampard, Milner, Gerrard, Defoe, Rooney
Germany: Neuer, Friedrich, Mertesacker, Lahm, Badstuber, Scheinsteiger, Ozil, Khedira, Muller, Klose, Podolski.
Refa: J. Larrionda [Uruguay]
-------------------------------------------------------------------
Saa 3.30 usiku: Soccer City, Soweto, Johannesburg
Argentina v Mexico
Argentina na Mexico zimewahi kukutana mara 10 kwenye Fainali za Kombe la Dunia na Argentina wameshinda mara 7 kati ya hizo.
Mexico wataingia mechi hii wakitoka Kundi B ambako walitoka sare na Afrika Kusini 1-1, kuitandika Ufaransa 2-0 na kufungwa na Uruguay 1-0.
Argentina wao walishinda mechi zao zote kwa kuifunga Nigeria 1-0, Korea Kusini 4-1 na Ugiriki 2-0.
Wakati Mexico hawana uhakika kama Straika wa Arsenal Carlos Vela atakuwa fiti kucheza, Argentina hawana Mchezaji yeyote majeruhi.
Timu:
Argentina: Romero, Samuel, Demichelis, Gutierrez, Mascherano, Heinze, Veron, Di Maria, Tevez, Messi, Higuain.
Mexico: Perez, Moreno, Rodriguez, Osorio, Marquez, Salcido, Torrado, Guardado, Giovani, Franco, Hernandez.
Refa: Roberto Rosetti [Italy]

No comments:

Powered By Blogger