Sunday 20 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Cameroun baibai Kombe la Dunia
Cameroun jana Jumamosi Juni 19 ilitandikwa bao 2-1 na Denmark, baada ya kuongoza 1-0, na kuwa Nchi ya kwanza kutolewa nje ya Fainali za Kombe la Dunia 2010 na pia kuihakikishia Uholanzi kuwa Timu ya kwanza kuingia Raundi ya Pili.
Cameroun walitangulia kupata bao dakika ya 10 kupitia Nahodha wao Samuel Eto’o kufuatia kosa la Difensi ya Denmark.
Lakini Denmark hawakukata tama na Straika kutoka Arsenal, Nicklas Bendtner, alisawazisha dakika ya 33 kwa shuti kali baada ya pasi murua toka kwa Rommedahl.
Kipindi cha Pili, Denmark waliibuka vizuri na dakika ya 61 Rommedahl, akitumia juhudi binafsi, aliipa ushindi Denmark kwa bao safi.
Mechi ya mwisho, Denmark wataivaa Japan huko Royal Bafokeng, Rustenburg Siku ya Alhamisi kuamua nani wanaungana na Holland kucheza Raundi ya Pili.
Cameroon: 16-Hamidou Souleymanou; 19-Stephane Mbia, 5-Sebastien Bassong, 3-Nicolas Nkoulou, 2-Benoit Assou-Ekotto; 8-Geremi, 18-Enoh Eyong, 6-Alexandre Song, 10-Achille Emana; 15-Achille Webo, 9-Samuel Eto'o.
Denmark: 1-Thomas Sorensen; 15-Simon Poulsen, 4-Daniel Agger, 3-Simon Kjaer, 6-Lars Jacobsen; 19-Dennis Rommedahl, 2-Christian Poulsen, 10-Martin Jorgensen, 8-Jesper Gronkjaer; 9-Jon Dahl Tomasson, 11-Nicklas Bendtner.
Refa: Jorge Larrionda [Uruguay]

No comments:

Powered By Blogger