Sunday 20 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Brazil yamgalagaza Drogba, yajikita Raundi ya Pili!!!
Ndani ya Soccer City, Soweto, Johannesburg, Brazil leo Jumapili Juni 20 waliweza kuifunga Ivory Coast mabao 3-1 na kujizolea Pointi 6 katika mechi mbili walizocheza na kutinga Raundi ya Pili huku wakiwa kileleni kwenye Kundi G wakisubiri mechi yao ya mwisho na Ureno.
Ureno Jumatatu Juni 21 watacheza na Korea Kaskazini huko Uwanja wa Green Point, Cape Town.
Tangu mpira uanze Ivory Coast walionekana kutulia na Brazil walianza polepole.
Ilipotimu katikati ya Kipindi cha kwanza, Brazil walipanda na mpira toka upande wao na walianza gonga safi toka nyuma na hatimae kuwashirikisha Felipe Melo, Kaka na Robinho na mwishowe mpira kupenyezwa kwa Luis Fabiano aliefumua shuti kali na kumpita Kipa Boubacar juu na kutinga wavuni hiyo ikiwa ni dakika ya 25.
Hadi mapumziko Brazil 1 Ivory Coast 0.
Dakika 5 tu baada ya Kipindi cha Pili kuanza, alikuwa Luis Fabiano tena akiwa katikati ya Madifenda watatu, na pengine kwa msaada wa mkono, aliukontroli mpira na kuwapita Mabeki hao na kukutana uso kwa uso na Kipa Boubacar na kwa mara ya pili akamshinda kwa kigongo kingine.
Dakika ya 62, kazi njema ya Kaka kwenye winga ya kushoto aliyoimaliza kwa pande maridadi kwa Elano aliefunga bao la 3 na hilo likiwa bao lake la pili katika mechi mbili.
Drogba aliipatia Ivory Coast bao lao moja huku Difensi ya Brazil ikizubaa wakidhani yuko ofsaidi lakini marudio yalionyesha lilikuwa bao safi.
Keita wa Ivory Coast alileta udanganyifu mkubwa alipojidai amepigwa na Kaka wakati si kweli na Refa Lannoy akadanganyika na kumpa Kaka Kadi ya Njano ya pili na hivyo kutolewa nje.
Timu:
Brazil : Julio Cesar; Maicon, Lucio, Juan, Michel Bastos; Felipe Melo, Gilberto Silva; Elano, Kaka, Robinho; Luis Fabiano.
Ivory Coast: Boubacar Barry; Emmanuel Eboue, Kolo Toure, Guy Demel, Siaka Tiene; Didier Zokora, Yaya Toure, Cheik Tiote; Salomon Kalou, Didier Drogba, Aruna Dindane.
Refa: Stephane Lannoy [France]

No comments:

Powered By Blogger