Saturday 26 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

FIFA yaionya Ufaransa
**Waziri ataka kuangusha kisago kwa walioleta aibu!!
FIFA imewasiliana na Serikali ya Ufaransa na kuwakumbusha kuwa wasiingilie masuala ya FFF, Chama cha Soka cha Ufaransa, kufuatia kutupwa nje ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini na Timu yao kukumbwa na mzozo mkubwa uliosababisha Mchezaji Nicolas Anelka atimuliwe toka kwenye Timu baada ya ugomvi na Kocha Raymond Domenech.
Kufuatia kuaibishwa kwa kumaliza Kundi lao wakiwa mkiani, Wizara ya Michezo ikiongozwa na Waziri, Bibi Roselyne Bachelot, imetaka serikali iingilie kati uozo uliokuwepo FFF.
Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, amesema wameijulisha Ufaransa kuhusu msimamo wa FIFA kuhusiana na masuala ya Soka kutoingiliwa na Serikali.
FIFA imewahi kuwasimamisha Uanachama baadhi ya Vyama vya Soka vya Nchi kwa kuingiliwa na Serikali katika uendeshaji wake na Valcke ametamka: “Tumeongea na Waziri na tumemjulisha wajibu wao. Wana uhuru wa kukutana nao, kujadiliana, kutaka Watu waombe radhi lakini wasiingilie uendeshaji na kutaka Watu wajiuzulu. FIFA itachukua hatua kama zilivyochukuliwa Nchi nyingine.”

No comments:

Powered By Blogger