Friday, 25 June 2010

PITIA: www.sokainbongo.com

Fergie adai Kombe linaenda Marekani ya Kusini
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amebashiri kuwa Kombe la Dunia litaenda katika moja ya Nchi za Marekani ya Kusini.
Hadi sasa Timu 5 za Marekani ya Kusini hazijafungwa na huenda zote zikatinga Raundi ya Pili ya Timu 16.
Nchi hizo ni Uruguay, Chile, Brazil, Paraguay na Argentina.
Ferguson amesema: “Nahisi Brazil. Paraguay ni hatari wana nguvu na kasi. Chile wamefanya vizuri na Argentina ni wazuri. Lakini Brazil bado wana ule uchawi! Ukianza kufikiria hii si ile Brazil ya zamani, wao ndio hubadilika!”
Kuhusu England, Ferguson amesema Timu hiyo bado ipo kwenye kinyang’anyiro ingawa mategemeo makubwa ya Washabiki ndio yanaiathiri Timu kwa kuipa presha kubwa.
Alipoulizwa kuhusu Mchezaji wake Patrice Evra ambae ni Nahodha wa France iliyotolewa kwenye Kombe la Dunia na ambayo imekumbwa na matatizo makubwa kambini kwake ilipokuwa Afrika Kusini hadi Mchezaji Nicolas Anelka akafukuzwa, Ferguson amesema alibadilishana meseji na Evra ambae kwa sasa anaenda vakesheni.
Ferguson amezungumza: “Hatujui nini hasa kilitokea lakini inasikitisha. Kitu cha mwisho unachotaka ni mgomo kambini. Inaweza kuwa walikuwa na sababu za msingi lakini wangefikiria wale maelfu waliosafiri hadi Afrika Kusini kuwashangilia!”

No comments:

Powered By Blogger