Friday 25 June 2010

PITIA: www.sokainbongo.com

Magazeti Ufaransa yamchamba Domenech na Les Bleus……
Magazeti Bondeni yaisifia Bafana Bafana!!!!!!!!!!!!!!
Ufaransa ilisafirishwa kurudi kwao kwa fedheha kubwa baada ya kutolewa raundi ya Kwanza ya Kombe la Dunia na Wachezaji kupandishwa Daraja la chini kwenye Ndege huku wakiandamwa kwa maneno mabovu toka kila Gzeti la Nchi hiyo ambayo mengi yalimtoa kafara Kocha wake Raymond Domenech.
Licha ya kubwagwa nje ya Kombe la Dunia na kuweka historia ya kuwa Mwenyeji wa kwanza wa Fainali za Kombe la Dunia kutolewa Raundi ya Kwanza, Bafana Bafana imezoa sifa toka kila Gazeti la Afrika Kusini.
Huko Ufaransa, Gazeti la Michezo, L’Equipe, liliandika bango kubwa: ‘Mwisho wa Dunia Moja!” wakimlenga Kocha Raymond Domenech na kumkebehi baada ya kunukuliwa akiongea na Wanahabari mara baada ya kupigwa 3-2 na Bafana Bafana katika mechi ya mwisho akisema: “Mimi natoka Dunia nyingine.”
Gazeti jingine Le Parisien lilitoa kichwa: ‘Ahsante na Kwa heri!’
Kuna Gazeti moja, Liberation, lilihoji hata kuwepo kwa Ufaransa huko Afrika Kusini na kudai walidhulumu nafasi ya Ireland baada ya ile skandali ya Thierry Henry ya kushika mpira katika mechi na Ireland na kumpasia Gallas aliesawazisha na kuipeleka Ufaransa Fainali za Kombe la Dunia.
Gazeti hilo lilidai sasa haki imetendeka kwa Ufaransa kuaibishwa na kufedheheshwa.
Huko Afrika Kusini, Magazeti yameisifia Bafana Bafana kwa kuyaaga Mashindano hayo kwa ushindi dhidi ya vigogo Ufaransa

No comments:

Powered By Blogger