Sunday 20 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Sakata la Anelka
Kocha Raymond Domenech wa Ufaransa amejaribu kuzima sakata la Nikolas Anelka kutimuliwa toka Kikosi cha Ufaransa kilichopo huko Afrika Kusini kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa kusema kuwa Anelka angebaki kwenye Timu kama angekubali kuomba radhi.
Domenech alisema: “Niliongea na Anelka baadae na nikajaribu kumtaka aombe radhi lakini hakutaka.”
Domenech amedai sakata la Anelka lingemalizika ndani ya Timu lakini kwa bahati mbaya kuna Mtu akalivujisha Magazetini na likalipuka kupita ilivyotegemewa.
Wakati huohuo, Nahodha wa Anelka huko Chelsea, John Terry, amejitokeza kumtetea Anelka kwa kudai Viongozi wa Ufaransa wamekosea kumfukuza Anelka toka kwenye Timu.
Terry amedai: “Huwezi kupata Mtu bora kwenye Soka kama Anelka. Ni mtu mkimya mno na siku zote akitaka kuzungumza kitu ntamsikiliza. Ni kosa kumfukuza. Yeye ni Mchezaji bora!”
Domenech amekuwa Kocha wa Ufaransa kwa Miaka 6 sasa lakini utawala wake umekuwa ukigubikwa na matatizo mara kwa mara na kumfanya asipendwe huko kwao.
Baada ya Kombe la Dunia Domenech atang’atuka na nafasi yake kuchukuliwa na Kepteni wa zamani wa Ufaransa, Laurent Blanc aliewahi pia kuwa Mchezaji wa Manchester United kabla hajastaafu.
Msimu uliokwisha Blanc alikuwa Meneja wa Mabingwa wa zamani wa Ufaransa Bordeaux.

No comments:

Powered By Blogger