Saturday 26 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Uruguay Timu ya kwanza ndani ya Robo Fainali
Bao mbili za Mchezaji kutoka Klabu ya Ajax, Luis Suarez, zimewaingiza Uruguay Robo Fainali wakiwa ndio Timu ya kwanza kufuzu baada ya kuifunga Korea Kusini 2-1.
Suarez alifunga bao lake la kwanza dakika ya 8 kufuatia uzembe wa Difensi ya Korea na kumkuta mpira pembeni na kufunga kilaini.
Kipindi cha Pili dakika ya 68, Korea walirudisha baada ya frikiki kuunganishwa na Lee Chung-young.
Kona iliyopigwa dakika ya 80 ilimkuta Luis Suarez akiwa kushoto mwa goli na akapiga shuti la kupinda likagonga posti na kuipa ushindi Uruguay.
Robo Fainali, Uruguay itacheza na Mshindi kati ya USA v Ghana.
Maradona: “Veron ni Kocha wangu Uwanjani!’
Kocha wa Argentina Diego Maradona amesema Mchezaji Mkongwe Juan Sebastian Veron ndie Kocha wake akicheza Uwanjani.
Maradona na Veron walikutana Boca Juniors Mwaka 1996 wakati Maradona akikaribia kustaafu na Veron ndio kwanza anaanza kuchipukia.
Veron, Miaka 35, aliandika kwenye kitabu chake: “Ukweli kwamba nilicheza na Maradona ni heshima kubwa!”
Veron kwa sasa anachezea Klabu ya kwao huko Argentina, Estudiantes, baada ya kushindwa kuwika akiwa na Manchester United na baadae Chelsea lakini tangu arudi Estudiantes, Klabu aliyocheza nayo akianza Soka lake, Veron amewika na kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora Marekani ya Kusini mara mbili na pia kushinda Kombe la Klabu Bingwa Marekani ya Kusini, Libertadores na vilevile kurudishwa Kikosi cha Argentina ambacho hakuchukuliwa Fainali za Kombe la Dunia za huko Ujerumani Mwaka 2006 baada ya kutupiwa lawama ya kusababisha Argentina itolewe Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2002 Raundi ya Kwanza.
Ingawa Nahodha wa Argentina ni Javier Mascherano wa Liverpool, Maradona ameonyesha imani kubwa kwa Veron alipotamka: “Yeye ni Mchezaji wa Argentina anaejua Soka sana na ndio maana akicheza yeye ni Kocha wangu Uwanjani!”
Maradona aliongeza kwa kusema kuwa anamuhitaji sana Veron kwa vile anawahamasisha na kuwapigia kelele wenzake wakicheza Uwanjani.
Pia Maradona alinena: “Namuhitaji Veron kwa sababu ni Mtu pekee anaeweza kumkontroli Messi. Messi anamsikiliza sana Veron! Hilo ni jambo kubwa sana!”

No comments:

Powered By Blogger