Monday 21 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Ureno 7 Korea Kaskazini 0
Ureno imejipa matumaini makubwa ya kuungana na Brazil kucheza Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia walipoibamiza Korea Kaskazini kwa mabao 7-0 katika mechi ya Kundi G iliyochezwa Green Point huko Cape Town.
Hadi mapumziko, Ureno walikuwa mbele kwa bao 1-0 alilofunga Raul Meireles.
Kipindi cha Pili Ureno walicharuka na ndani ya dakika 7 waliongeza mabao kupitia Simao, Hugo Almeida na Tiago.
Baadae Liedson, Ronaldo na Tiago waliongeza mabao mengine.
Katika Kundi hili Brazil wanaongoza wakiwa na Pointi 6, Ureno Pointi 4, Ivory Coast moja na Korea Kaskazini hawana pointi.
Mechi za mwisho ni Brazil v Ureno na Ivory Coast v Korea Kaskazini.
Chile 1 Uswisi 0
Chile wamefanikiwa kujikita kwenye kilele cha Kundi H walipoifunga Uswisi 1-0 huku Uswisi ikicheza Mtu 10 kwa zaidi ya Saa nzima kufuatia Kadi Nyekundu kwa Behrami.
Hadi mapumziko ngoma ilikuwa 0-0.
Kwenye dakika ya 75 Paredes wa Chile aliiua ofsaidi triki ya Uswisi na kupokea pasi nzuri toka kwa Valdivar kasha akampelekea Gonzalez aliefunga kwa kichwa.
Chile wanaongoza Kundi H wakiwa na pointi 6 na wanafuata Uswisi wenye 3.
Mechi inayofuata baadae leo ya Kundi hili ni kati ya Spain na Honduras.
Timu:
Chile:-Claudio Bravo; Mauricio Isla, Waldo Ponce, Arturo Vidal; Gary Medel, Carlos Carmona, Gonzalo Jara; Matias Fernandez; Alexis Sanchez, Humberto Suazo, Jean Beausejour.
Switzerland: Diego Benaglio; Stephan Lichtsteiner, Stephane Grichting, Steve Von Bergen, Reto Ziegler; Valon Behrami, Gokhan Inler, Benjamin Huggel, Gelson Fernandes; Alexander Frei, Blaise Nkufo.
Refa: Khalil Al-Ghamdi (Saudi Arabia)
Dunga aishangaa Kadi Nyekundu kwa Kaka
Kocha wa Brazil Dunga ameielezea Kadi Nyekundu aliyopewa Kaka katika mechi ya Jumapili Juni 20 Brazil walipoichapa Ivory Coast mabao 3-1 kuwa si haki.
Ushindi huo umeifanya Brazil itinge Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.
Dunga alilalamika: “Mchezaji aliecheza faulo anapewa Kadi ya Njano na asiekuwa na hatia Kadi Nyekundu!”
Kaka alipewa Kadi ya Pili ya Njano na hivyo kupata Kadi Nyekundu baada ya Kader Keita kumgonga Kaka na kudanganya amepigwa.
Dunga pia alilalamikia uchezeshaji wa Refa Stephane Lannoy kutoka Ufaransa kwa kutoa Kadi nyingi kwa Brazil wakati Ivory Coast ndio waliocheza rafu zaidi na nyingi zikiwa mbaya na za Kadi Nyekundu.

No comments:

Powered By Blogger