Tuesday 22 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Uruguay na Mexico ZAFUZU, Bafana na Ufaransa NJE!!!
Wenyeji wa Kombe la Dunia, Afrika Kusini, licha wa kuifunga Ufaransa goigoi kwa bao 2-1 wametupwa nje ya Mashindano hayo kwa tofauti ya magoli na kuiruhusu Mexico kusonga mbele licha ya kufungwa bao 1-0.
Mechi zote hizi mbili zimechezwa leo Jumanne Juni 22 kwa wakati mmoja Afrika Kusini v Ufaransa ikichezwa huko Uwanja wa Free State Mjini Blomfentein na Uruguay v Mexico ikiwa Royal Bafokeng, Rustenburg.
Afrika Kusini walipata mabao yao kupitia Bongani Khumalo dakika ya 20 na Mphela dakika ya 37.
Ufaransa walipata pigo dakika ya 26baada ya Mchezaji wao Gourcuff kupewa Kadi Nyekundu kwa kumpiga kipepsi Sibaya.
Kwenye mechi ya Uruguay v Mexico, Uruguay walipata bao lao la ushindi dakika ya 43 kupitia Suarez.
Uruguay ndie ameshika uongozi wa Kundi A na atacheza mechi yake ya Raundi ya Pili ya Mtoano hapo Juni 26 dhidi ya Mshindi wa Pili kundi B.
Mexico wameshika nafasi ya Pili Kundi A na watapambana na Mshindi wa Kwanza Kundi B hapo Juni 27 na uwezekano mkubwa mpinzani wake atakuwa Argentina.

No comments:

Powered By Blogger