Wednesday, 23 June 2010

CHEKI: http://www.sokainbongo.com/

England yapenya, USA yajipenyeza Raundi ya Pili!!!
England ilitakiwa ishinde mechi yake na Slovenia ili wafuzu kuingia Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia na alikuwa ni Jermaine Defoe ndie aliewabeba kwa kufunga bao moja na la ushindi katika mechi iliyochezwa leo Jumatano Juni 23 huko Uwanja wa Nelson Mandela, Port Elizabeth.
Bao la ushindi la Defoe lilipatikana dakika ya 23 baada ya krosi tamu ya James Milner kukutwa na Defoe alieunganisha.
Kwa ushindi huo England imepata pointi 5 sawa na USA lakini USA, aliemfunga Algeria 1-0 pia leo, amefunga bao zaidi ya England na hivyo kuchukua uongozi wa Kundi C.
USA watacheza na Mshindi wa Pili wa Kundi D na England atacheza na Mshindi wa Kundi D.
Kundi D ni Ghana, Germany, Serbia na Australia.
Timu;
England: 1-David James; 2-Glen Johnson, 15-Matthew Upson, 6-John Terry, 3-Ashley Cole; 16-James Milner, 4-Steven Gerrard, 8-Frank Lampard, 14-Gareth Barry; 19-Jermain Defoe, 10-Wayne Rooney.
Slovenia: 1-Samir Handanovic; 2-Miso Brecko, 4-Marko Suler, 5-Bostjan Cesar, 13-Bojan Jokic; 10-Valter Birsa, 8-Robert Koren, 18-Aleksandar Radosavljevic, 17-Andraz Kirm; 9-Zlatan Ljubijankic, 11-Milivoje Novakovic.
Refa: Wolfgang Stark (Germany)
USA 1 Algeria 0
Dakika 90 ziliyoyoma na USA aliekuwa kabanwa mbavu na Algeria kwa kuwa sare 0-0 alikuwa ndio anaelekea nje ya Kombe la Dunia huku Slovenia ingawa alikuwa kafungwa na England 1-0 ndie alikuwa anasonga mbele lakini katika dakika ya kwanza tu ya dakika 4 za nyongeza USA wakafunga bao na kuwapiku Slovenia na pia kuwa ndio vinara wa Kundi C.
Goli hilo la dakika ya 91 lilifungwa na Landon Donovan kufuatia kaunta ataki na Altidore kumpenyezea Dempsey ambae shuti lake liliokolewa na Kipa wa Algeria Mbouli na kutua kwa Donovan alieuvurumisha mpira wavuni.
Katika Raundi ya Pili, USA watacheza na Mshindi wa Pili wa Kundi D ambae ni ama Ghana, Germany, Serbia au Australia.
Timu:
USA Tim Howard; Steve Cherundolo, Jay DeMerit, Jonathan Bornstein, Carlos Bocanegra; Landon Donovan, Michael Bradley, Maurice Edu, Clint Dempsey; Jozy Altidore, Hercules Gomez.
Algeria Rais Ouheb Mbouli; Majid Bougherra, Rafik Halliche, Antar Yahia, Nader Belhadj, Fouad Kadir, Hassan Yebda, Medhi Lacen, Karim Ziani, Rafik Djebbour, Karim Matmour.
Refa: Frank De Bleeckere (Belgium

No comments:

Powered By Blogger