Tuesday 22 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Kesho Terry uso kwa uso na Refa aliemsema hana adabu
Beki wa England, John Terry, kesho Jumatano Juni 23 England watakapocheza na Slovenia atakumbana na Refa kutoka Ujerumani Wolfgang Stark ambae alimlaumu kwa kutomwonyeshea heshima Mwezi Machi Klabu yake Chelsea ilipotolewa na Inter Milan Uwanjani Stamford Bridge kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI.
Wakati huo Terry alikasirishwa na Refa Wolfgang Stark kukataa kumsikiliza Terry alipokuwa akimfuata Uwanjani wakati wa mechi ili kutaka maelezo ya maamuzi ya Refa huyo lakini kila mara alikataa kumsikiliza na baada ya mechi Terry akalalamika: “Mie kama Kepteni nilikwenda kuongea nae lakini akakataa akanipa mgongo. Hakutaka kuongea na mimi. Hilo ni kutokuwa na heshima!”
Mechi hii ya England v Slovenia ni muhimu kwa England ambao ni lazima washinde ili wasonge Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.
Refa Wolfgang Stark ameshawahi kuichezesha England mara 3 na zote England wameshinda.
Kwa John Terry hii ni wiki ya balaa kwake kwa vile pia amejikuta yuko kwenye mgogoro na Kocha wake Fabio Capello.

No comments:

Powered By Blogger