Mabingwa wa Dunia Italy NJEEE, wavuliwa Taji!!!!!!
Himaya ya Italia kama Mabingwa wa Dunia leo imemalizwa rasmi kwenye Uwanja wa Ellis Park, Johannesburg waliponyukwa bao 3-2 na Timu ‘ndogo’ toka Nchi ndogo sana, Slovakia.
Mbali ya kutupwa nje ya Kombe la Dunia, Italia wameaibishwa kwa kumaliza Kundi F wakiwa mkiani wakipitwa na hata Timu ‘kibonde’ New Zealand.
Aliekuwa mwiba mkubwa na alieongoza kipigo cha Italy ni Straika Vittek wa Slovakia aliefunga bao mbili, dakika ya 25 na 73.
Kopunek alifunga bao la 3 dakika ya 89.
Mabao ya Italy yalifungwa na Di Natale dakika ya 81 na Quagliarella dakika ya 90.
Ushindi huu umeifanya Slovakia iingie Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia na itacheza na Mshindi wa Kundi E ambae nafasi kubwa ipo kwa Uholanzi.
Timu:
Italy:
Marchetti, Zambrotta, Cannavaro, Chiellini, Criscito, Gattuso, De Rossi, Montolivo, Pepe, Iaquinta, Di Natale.
Akiba: Buffon, Maggio, Gilardino, Bocchetti, Marchisio, Camoranesi, Palombo, Quagliarella, Pazzini, Pirlo, Bonucci, De Sanctis.
Slovakia:
Mucha, Pekarik, Skrtel, Durica, Zabavnik, Hamsik, Strba, Kucka, Stoch, Vittek, Jendrisek.
Akiba: Pernis, Cech, Weiss, Kozak, Sestak, Sapara, Holosko, Jakubko, Kopunek, Salata, Petras, Kuciak.
Refa: Howard Webb [Italy]
Paraguay yatinga Raundi ya Pili
Paraguay imetoka sare ya 0-0 na New Zealand na hivyo kuongoza Kundi F na kuingia Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia ikiungana na Slovakia ambao wamemaliza nafasi ya pili.
New Zealand wamemaliza wakiwa nafasi ya 3, juu ya waliokuwa Mabingwa wa Dunia Italy ambao wameshika mkia na kutupwa nje ya Kombe la Dunia.
New Zealand wametoka sare mechi zao zote za Kundi F.
Raundi ya Pili, Paraguay watacheza na Mshindi wa Pili wa Kundi E.
Scholes kustaafu 2011
Kiungo wa Manchester United, Paul Scholes, Miaka 35, amesema atacheza Soka Msimu mmoja tu na kisha kustaafu.
Scholes nusura ajiunge na Timu ya England iliyoko huko Afrika Kusini kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuombwa na Kocha wa England Fabio Capello afute uamuzi wa kustaafu kucheza Mechi za Kimataifa lakini akakataa ingawa baadae alikiri kama angeombwa mapema angekubali.Veterani huyo amesema: “Ndio namaliza miaka yangu kwenye Soka na ntacheza Mwaka mmoja zaidi. Nimeanza kuchukua Beji za Ukocha na siku moja ntafundisha Watoto au Timu. “
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, bado ana imani Scholes kiwango na uwezo upo wa kuendelea kucheza kwa muda mrefu.
Akionyesha shukrani zake kwa Ferguson kumlea tangu utoto kwenye maisha yake ya Soka, Scholes amenena: “Ferguson ni Mtu Bora kabisa! Bila ya kutamka, yeye ni Meneja Bora na mzuri sana! Amewaendeleza Chipukizi wengi na anatoa matumaini kwa kila Kijana kwenye Timu zao kuwa wakiwa wazuri watapewa nafasi. Ni mtu muhimu sana kwenye maisha yangu.”
No comments:
Post a Comment