Sunday 20 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

RAUNDI YA PILI YA MTOANO TIMU 16 kuanza Kesho!!
Timu 16 zitakazocheza Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini zitakamilika baada ya Kundi la mwisho Kundi H, lenye Timu za Chile, Spain, Uswisi na Honduras, kumaliza mechi zao leo usiku Ijumaa Juni 25.
Mechi za Raundi hii ya Pili zinanaanza Jumamosi Juni 26.
Ratiba ya Jumamosi Juni 26
Saa 11 jioni:
URUGUAY v SOUTH KOREA
Nelson Mandela, Port Elizabeth
Saa 3.30 usiku:
2] USA v GHANA
Royal Bafokeng, Rustenburg
TATHMINI:
Uruguay v South Korea
Uruguay walifuzu kuingia Raundi hii baada ya kutwaa uongozi wa Kundi A waliposhinda mechi mbili na kutoka sare moja.
South Korea, wakiongozwa na Nahodha Park Ji-Sung toka Manchester United, wametoka Kundi B ambako walishinda mechi moja, sare moja na kufungwa moja.
Timu hizi zimewahi kukutana mara 4 hapo nyuma na Uruguay wameshinda mechi 3 na sare moja.
Huko Afrika Kusini, Uruguay walitoka sare na Ufaransa na kuzitungua Bafana Bafana na Mexico.
Korea walishinda mechi ya kwanza dhidi ya Ugiriki, wakafungwa na Argentina na kutoka sare na Nigeria.
Mshindi wa mechi hii atakutana na Mshindi wa mechi kati ya USA v Ghana kwenye Robo Fainali.
Wakati Korea hupenda kutumia fomesheni ya 4-4-2 huku Park Ji-Sung na Lee Chung-yong wakileta moto toka kwenye Winga, Uruguay hupenda kutumia 4-3-3 inayoongozwa na Washambuliaji Edinson Cavani wa Klabu ya Palermo, Italia na Luis Suarez na Diego Forlan.
USA v Ghana
Meneja wa USA, Bob Bradley, ambae mwanawe Michael Bradley ni mmoja wa Wachezaji shupavu wa USA, ana imani ya hali ya juu na Timu yake akiamini itafika Fainali hapo Julai 11.
USA walimaliza Kundi C wakiwa sawa na England kwa pointi 5 kila mmoja lakini waliukwaa uongozi kwa kufunga goli nyingi.
Ghana walimaliza Kundi D nyuma ya Germany na ndio Timu pekee toka Afrika iliyobaki kwenye Mashindano haya makubwa yanayofanyika Afrika kwa mara ya kwanza.
Bradley ameizungumza Ghana: “Timu hii Ghana chini ya Kocha Milovan Rajevac ni nzuri sana! Wametulia, wana vipaji na pia wana nguvu!”
Wakati USA watawategemea sana Altidore, Clint Dempsey na Landon Donovan, Ghana wapo kina Asamoah Gwyan, Ayew [Mtoto wa Abedi Pele], Mensah na Kipa Kingston ambae ni imara mno.

No comments:

Powered By Blogger