Saturday 19 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Rooney awataka radhi Mashabiki England
Straika wa England Wayne Rooney amewaomba radhi Mashabiki wa England kufuatia maneno yake yaliyonaswa kwenye kamera ya pembeni mwa Uwanja aliyoyatoa mara tu baada ya filimbi ya mwisho ya mechi ya Ijumaa Juni 18 ambayo England ilienda sare 0-0 na Algeria.
Rooney alinaswa na kamera hiyo akisema: “Ni vizuri kuwaona Mashabiki wako wakikuzomea…….!”
Katika stetimenti ya FA, Rooney anakaririwa akiomba radhi na kusema alitoa matamshi yake huku akiwa amezongwa na hasira za kucheza vibaya na kutoka sare.
Kiwango cha Rooney katika mechi mbili walizocheza huko Afrika Kusini kwenye Kundi lao kimeonekana kuporomoka na hajaifungia goli England katika mechi 8 sasa. Hali hiyo imempa wasiwasi Kocha wa England Fabio Capello aliekiri uchezaji wa Rooney sio wa yule Rooney wanaemjua.

No comments:

Powered By Blogger