Friday 18 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com


Ufaransa......inasikitisha!!!
Wengi walijua Ufaransa, wakiongozwa na Meneja Raymond Domenech ambae huko kwao hawezi hata siku moja kuwa Bingwa wa Mtu anaependwa, ni bomu  na jana Alhamisi Juni 17 imetandikwa 2-0 na Mexico.
Kipigo hiki kimewaacha Ufaransa kukosa kabisa matumaini ya kusonga Raundi ya Pili kwani wamecheza mechi mbili na wana pointi moja tu na Timu za juu Kundi lao ni Mexico na Uruguay zenye pointi 4 kila moja na zinamaliza kwa kucheza pamoja.
Ufaransa watamaliza na Mwenyeji Afrika Kusini na wote wana pointi moja kila mmoja.
Ni Mchezaji mpya wa Manchester United, Hernandez aka Chicharito, aliefunga bao la kwanza dakika ya 64 alipopenyezewa ndefu na Marquez na akakontroli kifuani na kumzunguka Kipa Lloris.
Goli la pili la Mexico ni kazi ya Pablo Barrero aliemtambuka Kepteni wa Ufaransa, Patrice Evra, na kuangushwa na Eric Abidal na kuzaa penalti iliyofungwa na Mkongwe Blanco, umri Miaka 37, alietoka umbali wa Mita kama 15 toka mpira wa penalti ulikowekwa.
Les Bleus walia na El Tri furaha.
Timu:
France: Lloris, Sagna, Gallas, Abidal, Evra, Govou, Toulalan,
Diaby, Malouda, Ribery, Anelka.
Akiba: Mandanda, Reveillere, Planus, Gourcuff, Cisse, Gignac, Henry, Squillaci, Diarra, Valbuena, Clichy.
Mexico: Perez, Osorio, Moreno, Rodriguez, Salcido, Marquez,
Giovani, Juarez, Torrado, Vela, Franco.
Akiba: Ochoa, Barrera, Castro, Blanco, Aguilar, Hernandez, Guardado, Magallon, Torres, Bautista, Medina, Michel.
Refa: Khalil Al Ghamdi (Saudi Arabia)

No comments:

Powered By Blogger