Sunday 13 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Slovenia 1 Algeria 0
Inaelekea Kundi C ni la balaa kwa Makipa kwani baada ya jana Kipa wa England kufanya kosa kubwa na kuwazawadia USA bao la kusawzisha leo Kipa wa Algeria, Faouzi Chaouchi, katika dakika ya 79 alifanya kosa kama la Kipa wa England, Robert Green, na kuwapa ushindi wasiotegemea Slovenia.
Shuti la mbali la Koren ambalo lilielekea halina madhara lilimponyoka Kipa huyo wa Algeria na kutinga wavuni.
Dakika mbili kabla ya bao hilo, Kipa wa Slovenia, Samir Handanovic, nusura awape zawadi Algeria pale pasi yake kwa Beki Suler ilinaswa na Karim Ziani lakini Mchezaji huyo itabidi ajilaumu kwani alishindwa kuukontroli mpira wakati akiwa pekee na Kipa.
Algeria ilimaliza mechi hii ikiwa Mtu 10 baada ya Ghezzal kupewa Kadi Nyekundu dakika ya 74 kufuatia Kadi za Njano mbili, ya kwanza aliyoipata dakika moja tu tangu aingizwe toka benchi dakika ya 60 na dakika ya 74 akalambwa Kadi ya pili ya Njano baada ya kuushika mpira kwa makusudi.
Mechi zinazofuata kwa Timu hizi ni Algeria v England na USA v Slovenia.
Timu:
Algeria: Chaouchi, Yahia, Bougherra, Halliche, Belhadj, Kadir, Lacen, Ziani, Yebda, Djebbour, Matmour.
Akiba: Gaouaoui, Mansouri, Boudebouz, Ghezzal, Saifi, Bellaid, Laifaoui, Guedioura, Medjani, Mesbah, Abdoun, M'Bohli.
Slovenia: Samir Handanovic, Brecko, Suler, Cesar, Jokic, Kirm, Koren, Radosavljevic, Birsa, Novakovic, Dedic.
Akiba: Jasmin Handanovic, Dzinic, Ilic, Pecnik, Ljubijankic, Krhin, Filekovic, Komac, Stevanovic, Mavric, Matavz, Seliga.
Refa: Carlos Batres (Guatemala).

No comments:

Powered By Blogger