Monday 14 June 2010

TEMBELEA: www.sokainbongo.com

Rufaa ya Mutu yatupwa, kuilipa Pauni Milioni 14 Ze Bluzi!!
Adrian Mutu ameamriwa kuilipa Chelsea fidia ya Pauni Milioni 14.3 baada ya rufaa yake kutupwa na Mahakama ya Juu huko Uswisi.
Chelsea walimfukuza Mutu Mwaka 2004 alipofungiwa kucheza Soka baada ya kugundulika akitumia kokeni na pia kumdai fidia kwa kukiuka Mkataba wake.
FIFA walimwamuru Mutu ailipe fidia Chelsea lakini Mutu akagoma na kukata rufaa CAS [Court of Arbitration for Sports], yaani Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, lakini huko nako Mutu akagonga mwamba na ndipo akakata rufaa Mahakama ya Juu ya Uswisi.
Kwa sasa Mutu yupo kwenye kifungo kingine cha Miezi 9 baada ya kugundulika anatumai dawa aina ya ‘Sibutramine’ wakati akiichezea Fiorentina Mwezi Februari na dawa hiyo ipo kwenye listi ya madawa marufuku.
Cahill alizwa na Kadi Nyekundu
Kiungo wa Australia Tim Cahill alidondokwa machozi wakati akielezea kupewa Kadi Nyekundu na hivyo kutolewa nje katika mechi ya jana ambayo Ujerumani iliichabanga Australia 4-0 katika Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia.
Cahill, Mchezaji wa Everton huko England, alionyeshwa Kadi hiyo baada ya kuvaana na Bastian Schweinsteiger lakini Watu wengi wanadai Refa Marco Rodriguez kutoka Mexico alikosea kwa kumpa Kadi hiyo na sana sana angepewa Kadi ya Njano.
Cahil amenung’unika: “Ndoto huwepo na zinateketezwa kwa muda mchache tu! Lakini nimefarijika kumsikia Schweinsteiger akisema ile si Kadi Nyekundu!”
Cahill ataikosa mechi ijayo na Ghana Siku ya Jumamosi.

No comments:

Powered By Blogger