Thursday 17 June 2010

PITIA: www.sokainbongo.com


Argentina 4 Korea Kusini 1
Leo Argentina wamijasafishia njia ya kutinga Raundi ijayo ya Kombe la Dunia walipoichapa Korea Kusini mabao 4-1 huko Soka City, Soweto na kuwafanya wawe wanaongoza Kundi B wakiwa na pointi 6 baada ya pia kushinda mechi yao ya kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya Nigeria.
Mechi ya mwisho Argentina watacheza na Ugiriki.
Shujaa kwa Argentina alikuwa ni Straika wa Real Madrid, Gonzalo Higuain, aliepachika bao 3 na bao moja Korea walijifunga wenyewe.
Argentina ndio waliotangulia kupata bao dakika ya 16 baada ya frikiki ya Lionel Messi kumbabatiza Park Chu-young.
Bao la pili lifungwa na Gonzalo Higuain dakika ya 33.
Korea Kusini walipata bao la sekunde chache kabla ya haftaimu baada ya Difenda Demichelis kuporwa mpira na Lee Chung-yong na kwenda kufunga.
Huku wakijikakamua, Korea Kusini walijikuta wakipigwa bao mbili toka kwa Higuain ndani ya dakika 4, dakika ya 76 na 80, na hivyo kumalizwa kabisa.
Timu:
Argentina: 22-Sergio Romero; 2-Martin Demichelis, 13-Walter Samuel, 6-Gabriel Heinze, 17-Jonas Gutierrez; 14-Javier Mascherano, 20-Maxi Rodriguez, 7-Angel Di Maria; 10-Lionel Messi, 11-Carlos Tevez, 9-Gonzalo Higuain.
South Korea: 18-Jung Sung-ryong; 2-Oh Beom-seok, 12-Lee Young-pyo, 4-Cho Yong-hyung, 14-Lee Jung-soo, 8-Kim Jung-woo, 16-Ki Sung-yong, 7-Park Ji-sung, 17-Lee Chung-yong, 10-Park Chu-young, 19-Yeom Ki-hun.
Refa: Frank De Bleeckere (Belgium)

No comments:

Powered By Blogger