Tuesday 15 June 2010

PITIA: www.sokainbongo.com

Dalkurd ya Sweden yatoa ofa ya Tegete Mtandaoni!
Klabu ya Daraja la Kwanza ya huko Sweden, Dalkurd FF, imetoa ofa rasmi kwa Yanga kupitia mtandaoni kwa kutumia mtindo mpya wa uhamisho wa FIFA ili imchukue kwa mkopo wa Mwaka mmoja straika wa Yanga Jerry Tegete.
Ili kuondoa utata na ubabaishaji Dalkurd FF imetumia mtindo mpya wa FIFA wa kumuombea Uhamisho Tegete na utaratibu huo unatumia njia za elektroniki kupitia mtandaoni na unaitwa ‘Transfer Matching System’ [TMS] na hivyo kuondoa utaratibu wa sasa wa kutumia faksi na makaratasi ili kuhamisha Wachezaji na hivyo kuondoa dosari nyingi.
Katika mfumo wa TMS uanaotumia mtandao, ili kukamilisha uhamisho wa Mchezaji inabidi Klabu zinazouza na kununua Mchezaji ziingize kwenye mtandao taarifa zote zinazotakiwa kuhusiana na Mchezaji anaehamishwa zikiwemo Ada ya Uhamisho, Mshahara wa Mchezaji huyo, Wakala wake au Mwanasheria wake na muda wa Mkataba wake.
Pia, ada ya uhamisho ni lazima itoke Benki moja kwenda nyingine na Benki zote ziwe zinatambulika halali kisheria.
Habari za kutoa ofa hiyo rasmi zimethibitishwa na Wakala wa Tegete, Damas Ndumbaro.
Wakati wa uzinduzi wa Mradi huo mpya wa FIFA wa Uhamisho Miezi kadhaa iliyopita, Meneja Mkuu wa TMS, Mark Goddard, alisema: “Mpaka sasa mtindo uliokuwa ukitumiwa ni wa makaratasi kama ilivyokuwa miaka 100 nyuma! Ilikuwa ngumu kufuatilia Wachezaji gani wamehamishwa. Kulikuwa na uhamisho feki, kulikuwa na uuzwaji wa Wachezaji ambao hawapo ili mradi Watu mafisadi wahamishe pesa zao toka Nchi moja hadi nyingine kinyume cha sheria!”
Goddard aliongeza: “Huu ni mradi mkubwa wa FIFA. Haujabadilisha sheria za uhamisho bali unadhibiti uhamisho na kuondoa kasoro na dosari nyingi.”
Mdau mmoja wa Bongo aliunga mkono TMS kwa kuamini mtindo huo utawakata maini Mafisadi wa Soka waliokuwa wakidhulumu Wachezaji na Klabu za Bongo.

No comments:

Powered By Blogger