Saturday 19 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

USA walia: ‘TUMEIBIWA!”
Timu ya USA imepiga kelele za kuibiwa baada ya goli lao la 3 kukataliwa na Refa Koman Coulibaly kutoka Mali kwenye mechi dhidi ya Slovenia hapo Ijumaa Juni 18 ambayo iliisha 2-2 huku USA wakitoka mapumziko wakiwa bao 2-0 nyuma na wakasawazisha na pia kufunga bao ‘safi’ lililokataliwa.
Mchezaji wa USA Landon Donovan alisema: “Tumeibiwa! Sijui kwa nini halikukubaliwa!”
Nae Kocha Bob Bradley, ambae Mtoto wake Michae Bradley ndie aliefunga bao la pili la USA la kusawazisha, alisema: “Mpaka sasa sijui ni kwanini limekataliwa!”
Goli hilo la 3 lilifungwa dakika ya 85 huku ngoma ikiwa 2-2 kufuatia frikiki iliyodondoshwa ndani ya boksi na Maurice Edu akaushindilia mpira wavuni.
Kuna taarifa kuwa FIFA wanachunguza bao hilo na huenda wakamwadhibu Refa Coulibaly endapo atakuwa amekosea kwenye uamuzi wake.

No comments:

Powered By Blogger