Friday, 18 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

USA 2 Slovenia 2
USA ilitoka nyuma wakiwa bao 2-0 hadi haftaimu leo Ijumaa Juni 18 huko Uwanja wa Ellis Park, Johannesburg na kusawazisha na pengine wangeshinda mechi hii lakini Refa Koman Coulibaly toka Mali kulikataa bao la 3 ‘safi’.
Slovenia walipata bao lao la kwanza dakika ya 13 kupitia Birsa aliefumua mkwaju toka Mita 25 na bao la pili walifunga dakika ya 41 kupitia Ljubijankic baada ya uzembe wa Difensi ya USA kumruhusu Novakovic kupokea pasi akiwa peke yake na kumpenyezea Ljubijankic aliefunga.
Hadi mapumziko Slovenia 2 USA 0.
Dakika ya 48 Cesar alifanya makosa katika kuokoa na Donovan akaingia haraka ndani ya boksi na kufunga toka engo mbaya.
Ndipo ilipowadia dakika ya 82 wakati Mtoto wa Kocha Bob Bradley wa USA, Bradley aliposawazisha baada ya pasi ya Altidore.
USA walifunga goli zuri baada ya hapo lakini likakataliwa.
Timu:
Slovenia: Samir Handanovic; Miso Brecko, Marko Suler, Bostjan Cesar, Bojan Jokic, Valter Birsa, Robert Koren, Aleksandar Radosavljevic, Andraz Kirm, Zlatan Ljubijankic, Milivoje Novakovic
USA: Tim Howard; Steve Cherundolo, Jay DeMerit, Oguchi Onyewu, Carlos Bocanegra; Landon Donovan, Michael Bradley, Jose Torres, Clint Dempsey; Jozy Altidore, Robbie Findley.
RefA: Koman Coulibaly (Mali)
Serbia 1 Germany 0
Serbia wamefufua matumaini yao baada ya kufungwa nechi yao ya kwanza na Ghana 1-0 walipowatungua vigogo Ujerumani 1-0 huko Uwanja wa Nelson Mandela, Port Elizabeth leo Ijumaa Juni 18 na staa mkubwa wa mechi hii alikuwa Refa toka Spain alietoa Kadi kama njugu.
Ujerumani ilicheza mechi hii ikiwa pungufu baada ya Miroslav Klose kutolewa kwa Kadi Nyekundu dakika ya 37 kufuatia Kadi za Njano mbili za papo kwa papo.
Dakika moja baada ya Klose kutolewa Milan Jovanovic akafunga alipopewa pasi na Nikola Zigic.
Ujeruamani walipoteza nafasi ya kurudisha dakika ya 60 walipokosa penalti iliyopigwa na Lukas Podolski kuokolewa na Kipa Vladimir.
Adhabu hiyo ilitolewa Beki Nemanja Vidic alipounawa mpira.
Serbia walikosa chansi mbili za kuongeza bao walipogonga mwamba mara mili kupitia Jovanovic na Zigic.
Ujerumani walishinda mechi yao ya kwanza walipoikung’uta Australia 4-0.

No comments:

Powered By Blogger